Wolle Melkas Fernando
JF-Expert Member
- May 4, 2016
- 253
- 360
Fikra/Akili ni muhimu sana huhusishwa katika kujinasua kwenye minyororo ya kitumwa.
Tanzania na Afrika kwa ujumla tunapenda kutuliza matatizo na sio kuyatatua Yaani tunameza 'pain killers' tu na sio dawa za kutibu. Tumefungwa kwenye minyororo ya Utumwa wa Fikra na Utumwa wa Kiuchumi.
Tatizo likitusumbua tunakopa kulituliza huku tukitengeneza tatizo kubwa zaidi la baadaye! Kutoboa sio kazi ndogo kama Taifa, endapo tutaendelea kuamini kwamba mataifa ya Kibepari yana dhamira njema ya kutaka tupige hatua Kimaendeleo na kuondokana na umaskini, umaskini utaondolewa na sisi wenyewe Kwa matumizi Bora ya rasilimali zetu.
Ubaya wa Mikopo ya Kibepari sio kama mikopo ya mtu binafsi anapokopa bank kwaajili ya biashara yake, hii mikopo ya nchi za Kibepari ina masharti magumu sana. Ukisikia viongozi wanasema huu mkopo ni wa masharti nafuu basi ujue nyuma ya pazia Kuna ajenda mbaya zitapenyezwa ambazo ni za muda mrefu (viongozi wanaweza wakawa hawajui au wanajua), mikopo inasababisha tusiwe na maamuzi yetu wenyewe.
Maamuzi ya hovyo yakitolewa na wanaotupa mikopo na misaada sisi tunakuwa hatuna nguvu ya kukataa, mfano haya mataifa yanapoleta ajenda za LGBT, utathubutu vipi kukataa maana anayekulisha ndiye atakayekutawala.
Mfano mdogo, anayekununulia lanchi akiwa timu ya Simba na wewe ni Yanga na timu hizi zikacheza, inabidi eidha uungane naye uwe Simba au useme hufungamani na timu yoyote.
Na ndio maana hata msimamo wa nchi za Afrika kuhusu vita ya Russia vs. Ukraine, Viongozi wengi wa Afrika wanasema hawafungamani na upande wowote. Kiukweli hakunaga msimamo wa kutofungamana upande wowote ila wanajua wakichagua upande mmoja, chamoto watakiona upande wa pili.