Matatizo mengi tuliyonayo nchini leo yameanzia na awamu ya tano; hapakuwepo na uhuru wa kusema wala kurekebisha mambo, sasa tunalipa kwa maumivu

Hizi ndio zile akili nyepesi nyepesi za watanzania kama nilivyoandika katika uzi wangu na sijui kama uliusoma au umerukia tu kukomenti.
Ulichoandika ni sahii
Tatizo lolote lile lilianzia mahali ni kama kupanda mti utakaa baada ya miaka kadhaa ndo utaanza matunda

Sawa na tatizo ukilifumbia macho ni swala la mda tu litaanza kuonekana matatizo mengi ya sahivi chanzo ni magufuli

Na angekuwepo watu wangeumia sana sababu angetumia nguvu badala ya akili kuyakabili
 
Kuna mtu alikua fisadi kama magufuli
Magufuli alishaingia mitini na trillion 1.5 kwa mara moja hujawah tokea uwizi mkubwa namna hiyo
Another AI generated post.

CAG hakusema zile hela ni unaccounted for hazipo, alichosema ni matumizi yake ayajakaguliwa (audited). Kwa sababu ofisi ya raisi aikaguliwi.

Baadae ikaja fahamika zimenunulia ndege kadhaa (unbudgeted for). Ndege ambazo kutwa huyo mama yenu kiguu njia anadhurura nazo leo, na walewale wengine waliokuwa vinara wa uongo wa wizi wakipakia na kunyoosha miguu first class kwenye hizo ziara.
 
Naona wewe ndio akili yako nyepesi kabisa. Sasa kama machine hazikufanyiwa service kwa wakati, na zimeshaharibika, unadhani kinachohitajika sasa ni service au kununua mashine mya? Umewahi kumiliki mashine yoyote inayohitaji regular service eg gari?
 
Naona wewe ndio akili yako nyepesi kabisa. Sasa kama machine hazikufanyiwa service kwa wakati, na zimeshaharibika, unadhani kinachohitajika sasa ni service au kununua mashine mya? Umewahi kumiliki mashine yoyote inayohitaji regular service eg gari?
Which is which machine ziliharibika au zilikuwa hazina services?

Kama ziliharibika mbona kafa ‘electricity plants’ bado zinazalisha umeme? Unaweza kutueleza walikuwa wanatumia mitambo gani kuzalishia umeme kama aliharibu mashine zote wakati yupo hai?

Ebu muwe mnafikiria kwanza unapotunga uongo walau uwe na elements za logic.
 
Tukiacha unafiki na utimu, kuna hoja nzito kwenye hii post. Ni kama tatizo la sukari lilipoibuka baada ya BAKWATA kunyimwa kibali cha kuagiza sukari.

Haikuzingatiwa kwamba kupewa kwao kibali kulikuwa kukisaidia kuua mfumuko wa bei kwa kufichwa sukari kipindi cha kukaribia Ramadhan.

Na tatizo la sukari lilianzia tangu yeye akiwepo, ila liliendelea kukua kwa kadri siku zinavyokwenda na matokeo mabaya zaidi yametokea mwaka huu.

Ova
 
Mashine za aina yoyote ile ikiwa hazijafanyiwa service kwa wakati, baada ya muda huwa zinaenda kufa kabisa.

Yaani matokeo huwezi kuyapata wakati huo kama kutia chumvi kwenye mboga, yatakuja baada ya muda. Na yataumiza.

Ova
 
Lakini magufuli ndiye alituletea samia kama sio magu samia asingekuepo!

Kwa ligha rahisi magu alimchagua makamu kimeo.
 
Mkuu unatumia silaha nzito kwa adui asiyestahili. Vijana wengi hawatumii mantiki na fikra tunduizi katika kujenga hoja.

Wanachofanya ni kutoa pumzi mdomoni tu;Sauti itakayotoka ndio hiyo hiyo.

Jichukulie kama mkufunzi, usichoke kutoa elimu.

Nchi hii itaharibika zaidi endapo watu wema kama wewe mtakapo amua kukaa kimya.
 
Mashine za aina yoyote ile ikiwa hazijafanyiwa service kwa wakati, baada ya muda huwa zinaenda kufa kabisa.

Yaani matokeo huwezi kuyapata wakati huo kama kutia chumvi kwenye mboga, yatakuja baada ya muda. Na yataumiza.

Ova
Kwa hivyo Kinyerezi hakuna kitu pale wanaenda kushinda na kupokea mishahara ya bure tu maana machine zote chalii.

Sasa Maharage Chande na Makamba zile habari zao za pick demand na sijui miundombinu ya kusafirishia ni tatizo zilikuwa porojo tu hata hiyo mitambo yenyewe ya kufulia umeme hawana.

Uongo una expiry date

Mvua zikinyesha hadithi zinaamia kwenye mitambo chakavu, nyaya kukatika, hujuma sijui za watu kuharibu transformers wakiiba mafuta na story zingine. Mvua zisipo nyesha mabwawa hayana maji.

Ni story kila kukicha ambazo sio constant kabisa zinabadilika na mazingira; kukikosekana utunzi kabisa wa kutunga Magufuli aliharibu.
 
Lakini magufuli ndiye alituletea samia kama sio magu samia asingekuepo!

Kwa ligha rahisi magu alimchagua makamu kimeo.
Uzuri wake aliliweka wazi kabla ya kuitwa chaguo lake binafsi lilikuwa Hussein Mwinyi.

Mengine ya CCM ndio walimuweka Samia na sidhani kama kuna mtu alijua huyo mjomba atomaliza vipindi viwili kawaida yao VP uwa ni ceremonial post ya kukata utepe tu.
 
🙏🙏🙏
 
Kuna mtu alikua fisadi kama magufuli
Magufuli alishaingia mitini na trillion 1.5 kwa mara moja hujawah tokea uwizi mkubwa namna hiyo
Acha ngebe wewe pachipachi ya kinyeo.
 
Tatizo unajadili sana nje ya muktadha hadi unaharibu mtiririko wa mjadala wenyewe. Unajiundia hoja & maswali na kujijibu mwenyewe.

Kujadili kwa namna hii huwa siwezi, kwa maana ya kama kuanza mjadala mpya kwenye kila comments. So, nikuache uendelee na wengine.

Ova
 
Tunachokiweza kuzalisha chawa wakimpigia chapuo kila kukicha
 
Umefanya reference ya UVIKO?
 
Watanzania sijui mnafikiri vipi. Unajua matatizo makubwa huanzia mbali sana. Kuna matatizo tunapata saa hii kwasababu ya vita ya Kagera, unajua hilo na huwa inakuwaje? Mmezoea sana kufikiri leo tu, mambo yanaanzia mbali sana. Kuna mambo Tanzania tunateseka hadi leo kwasababu ya siasa za Mwalimu za Ujamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…