Matatizo mengi tuliyonayo nchini leo yameanzia na awamu ya tano; hapakuwepo na uhuru wa kusema wala kurekebisha mambo, sasa tunalipa kwa maumivu

Matatizo mengi tuliyonayo nchini leo yameanzia na awamu ya tano; hapakuwepo na uhuru wa kusema wala kurekebisha mambo, sasa tunalipa kwa maumivu

Hizi ndio zile akili nyepesi nyepesi za watanzania kama nilivyoandika katika uzi wangu na sijui kama uliusoma au umerukia tu kukomenti.
Ulichoandika ni sahii
Tatizo lolote lile lilianzia mahali ni kama kupanda mti utakaa baada ya miaka kadhaa ndo utaanza matunda

Sawa na tatizo ukilifumbia macho ni swala la mda tu litaanza kuonekana matatizo mengi ya sahivi chanzo ni magufuli

Na angekuwepo watu wangeumia sana sababu angetumia nguvu badala ya akili kuyakabili
 
Kuna mtu alikua fisadi kama magufuli
Magufuli alishaingia mitini na trillion 1.5 kwa mara moja hujawah tokea uwizi mkubwa namna hiyo
Another AI generated post.

CAG hakusema zile hela ni unaccounted for hazipo, alichosema ni matumizi yake ayajakaguliwa (audited). Kwa sababu ofisi ya raisi aikaguliwi.

Baadae ikaja fahamika zimenunulia ndege kadhaa (unbudgeted for). Ndege ambazo kutwa huyo mama yenu kiguu njia anadhurura nazo leo, na walewale wengine waliokuwa vinara wa uongo wa wizi wakipakia na kunyoosha miguu first class kwenye hizo ziara.
 
Kitu gani cha maana ulichoandika AI

Nimekuuliza umeona wapi duniani services ya mashine ya kufulia umeme inafanyika kwa miaka kwa miaka mitatu. Umekazana Magufuli alikuwa analazimisha. Ina maana Magufuli ana miezi sita toka afe au? Toka hizo hadithi za Magufuli alikuwa afanyi services mitambo January alipo pata uwaziri sasa hivi ni miaka mingapi?

Unataka kutuambia services ya mitambo ni zaidi ya miaka mitatu; sasa kujenga itakuwa miaka mingapi.

Kwa kifupi mambo uliyoandika ni ya kukaririshwa tu programmed, but hakuna logic ya hoja given the time pass toka kifo cha Magufuli kupokea hizo lawama tena za kutunga.

Uongo una expiry date
Naona wewe ndio akili yako nyepesi kabisa. Sasa kama machine hazikufanyiwa service kwa wakati, na zimeshaharibika, unadhani kinachohitajika sasa ni service au kununua mashine mya? Umewahi kumiliki mashine yoyote inayohitaji regular service eg gari?
 
Which is which machine ziliharibika au zilikuwa hazina services?

Kama ziliharibika mbona kafa ‘electricity plants’ bado zinazalisha umeme? Unaweza kutueleza walikuwa wanatumia mitambo gani kuzalishia umeme kama aliharibu mashine zote wakati yupo hai?

Ebu muwe mnafikiria kwanza unapotunga uongo walau uwe na elements za logic.
 
Sorry ni awamu ya 5 ya bullzoda sio ya nne! Awamu ya 4 ilikuwa baba wa demokrasia.

Kabla ya 2015 angalau kulikuwa na uhuru wa kusema, ukweli ulijulikana na uliachwa usemwe kwa kiasi kikubwa, na wataalamu waliachwa watumie taaluma yao kutoa miongozo, lakini alipokuja Magufuli yeye aligeuka kuwa engineer, docta, mwanauchumi, na kila kitu.

Kuna mambo mengi watanzania wenye akili nyepesi nyepesi hawawezi kuyaona. Matatizo mengi tuliyonayo sasa hivi kama uhaba wa dola, umeme, ukosefu wa sukari n.k. yalitokana na utawala wa kuburuza mambo wa awamu ya tano.

Mfano umeme: Wakati wa Magufuli mashine nyingi za kufua umeme kwa kutumia gesi zilifanya kazi na kupitiliza wakati wake wa kufanyiwa ukarabati. Tanesco walilazimika kuendelea kufua umeme na mashine zilizokuwa zinahitaji kufanyiwa ukarabati kwani Tanesco wangeondoa baadhi ya machine ili kufanya ukarabati kungesababisha upungufu wa umeme na mgao kitu ambacho kingepelekea wao kufukuzwa kazi mara moja. Hivyo waliendelea kuzalisha umeme na mashine zilizokuwa hoi.

Leo karibu nusu nzima ya mashine za kufua umeme wa gesi pale Ubungo na Kinyerezi zimeharibika kwa mkupuo baada ya kulazimishwa kufanya kazi zikiwa mbovu! Matokeo yake leo hii tuna mgao ambao hata viongozi wetu hawana lugha nzuri ya kuulezea; watasema ni upungufu wa mvua hata pale ambapo El Nino zilikuwa tele kuanzia mwaka jana mwishoni. Hutasikia wakisema ukweli huu kuhusu ubovu wa mashine zitu, utawasikia wakisema ni ongezeko la matumizi ya umeme, hilo nalo ni uongo tu.

Matatizo ya sukari na dola yana mkondo huo huo. Nani asiyejua namna Magufuli alivyoharibu biashara kwa kuwabambikizia kodi wafanyabiashara, kuwapora mitaji na kuwalazimisha kufunga biashara zao kwa visingizio vya kodi? Matokeo ya hayo ndio leo tunayaona. Biashara kati ya Tanzania na nchi za nje ilidorora mno wakati wa Magufuli. Si mnakumbuka jinsi Magufuli alivyowachukia "mabeberu"? Unategemea nini kibiashara unapowachukia bussiness partners na kufunga biashara zao nchini?

Ila kwakuwa watanzania wengi wamelishwa uongo na hawana jinsi ya kugundua uongo huo basi wataamini kuwa Magufuli angekuwepo mambo yangekuwa mazuri. Nawaambia, saa hii tungekuwa kwenye hali ya tahadhari na majanga makubwa kiuchumi na kijamii. Magufuli hakuwa na upeo mkubwa kiuchumi, yeye alilazimisha kila kitu kama alivyopenda bila kujali matokeo yake. Leo tunateswa na matatizo ambayo chimbuko lake ni awamu ya 5 na hakuna kiongozi atakayetuambia ukweli huu!
Tukiacha unafiki na utimu, kuna hoja nzito kwenye hii post. Ni kama tatizo la sukari lilipoibuka baada ya BAKWATA kunyimwa kibali cha kuagiza sukari.

Haikuzingatiwa kwamba kupewa kwao kibali kulikuwa kukisaidia kuua mfumuko wa bei kwa kufichwa sukari kipindi cha kukaribia Ramadhan.

Na tatizo la sukari lilianzia tangu yeye akiwepo, ila liliendelea kukua kwa kadri siku zinavyokwenda na matokeo mabaya zaidi yametokea mwaka huu.

Ova
 
Which is which machine ziliharibika au zilikuwa hazina services?

Kama ziliharibika mbona kafa ‘electricity plants’ bado zinazalisha umeme? Unaweza kutueleza walikuwa wanatumia mitambo gani kuzalishia umeme kama aliharibu mashine zote wakati yupo hai?

Ebu muwe mnafikiria kwanza unapotunga uongo walau uwe na elements za logic.
Mashine za aina yoyote ile ikiwa hazijafanyiwa service kwa wakati, baada ya muda huwa zinaenda kufa kabisa.

Yaani matokeo huwezi kuyapata wakati huo kama kutia chumvi kwenye mboga, yatakuja baada ya muda. Na yataumiza.

Ova
 
Kwa hivyo Magufuli ndio aliemtuma aache watu wapige hela za serikali kufa mtu. Halafu wakishapata hiyo mihela wakanunue midola na kuleta upungufu.

Magufuli ndio aliemfundisha kulea wazembe serikalini.

Magufuli ndio aliemfundisha kuchekea watu wanao sabotage uchumi na mipango ya serikali

Magufuli kaacha mitambo yote ya umeme inafanya kazi, umeona services ya mitambo inachukua miaka 3 ya matengenezo

Magufuli ndio aliemtuma Bashe kugawa vibali kwa watu wasio na mitaji wala uwezo wa kuagiza sukari na kuwaletea shida.

Magufuli ndio aliemwambia Bashe asizingatie lead ya kuagiza; yaani utoe sukari Brazil kwa miezi miwili; wakati Uganda na Zambia unaipata kwa siku tu given the dire situation.

I can go and on

Acha kutumia akili za AI wewe ni binadamu you’re a reasonable being.
Lakini magufuli ndiye alituletea samia kama sio magu samia asingekuepo!

Kwa ligha rahisi magu alimchagua makamu kimeo.
 
Another AI generated post.

CAG hakusema zile hela ni accounted for hazipo, alichosema ni matumizi yake ayajakaguliwa (audited). Kwa sababu ofisi ya raisi aikaguliwi.

Baadae ikaja fahamika zimenunulia ndege kadhaa (unbudgeted for). Ndege ambazo kutwa huyo mama yenu kiguu njia anadhurura nazo leo na walewale wengine waliokuwa vinara wa uongo wa wizi wakipakia na kunyoosha miguu first class kwenye hizo ziara.
Mkuu unatumia silaha nzito kwa adui asiyestahili. Vijana wengi hawatumii mantiki na fikra tunduizi katika kujenga hoja.

Wanachofanya ni kutoa pumzi mdomoni tu;Sauti itakayotoka ndio hiyo hiyo.

Jichukulie kama mkufunzi, usichoke kutoa elimu.

Nchi hii itaharibika zaidi endapo watu wema kama wewe mtakapo amua kukaa kimya.
 
Mashine za aina yoyote ile ikiwa hazijafanyiwa service kwa wakati, baada ya muda huwa zinaenda kufa kabisa.

Yaani matokeo huwezi kuyapata wakati huo kama kutia chumvi kwenye mboga, yatakuja baada ya muda. Na yataumiza.

Ova
Kwa hivyo Kinyerezi hakuna kitu pale wanaenda kushinda na kupokea mishahara ya bure tu maana machine zote chalii.

Sasa Maharage Chande na Makamba zile habari zao za pick demand na sijui miundombinu ya kusafirishia ni tatizo zilikuwa porojo tu hata hiyo mitambo yenyewe ya kufulia umeme hawana.

Uongo una expiry date

Mvua zikinyesha hadithi zinaamia kwenye mitambo chakavu, nyaya kukatika, hujuma sijui za watu kuharibu transformers wakiiba mafuta na story zingine. Mvua zisipo nyesha mabwawa hayana maji.

Ni story kila kukicha ambazo sio constant kabisa zinabadilika na mazingira; kukikosekana utunzi kabisa wa kutunga Magufuli aliharibu.
 
Lakini magufuli ndiye alituletea samia kama sio magu samia asingekuepo!

Kwa ligha rahisi magu alimchagua makamu kimeo.
Uzuri wake aliliweka wazi kabla ya kuitwa chaguo lake binafsi lilikuwa Hussein Mwinyi.

Mengine ya CCM ndio walimuweka Samia na sidhani kama kuna mtu alijua huyo mjomba atomaliza vipindi viwili kawaida yao VP uwa ni ceremonial post ya kukata utepe tu.
 
Mkuu unatumia silaha nzito kwa adui asiyestahili. Vijana wengi hawatumii mantiki na fikra tunduizi katika kujenga hoja.

Wanachofanya ni kutoa pumzi mdomoni tu;Sauti itakayotoka ndio hiyo hiyo.

Jichukulie kama mkufunzi, usichoke kutoa elimu.

Nchi hii itaharibika zaidi endapo watu wema kama wewe mtakapo amua kukaa kimya.
🙏🙏🙏
 
Kuna mtu alikua fisadi kama magufuli
Magufuli alishaingia mitini na trillion 1.5 kwa mara moja hujawah tokea uwizi mkubwa namna hiyo
Acha ngebe wewe pachipachi ya kinyeo.
 
Kwa hivyo Kinyerezi hakuna kitu pale wanaenda kushinda na kupokea mishahara ya bure tu maana machine zote chalii.

Sasa Maharage Chande na Makamba zile habari zao za pick demand na sijui miundombinu ya kusafirishia ni tatizo zilikuwa porojo tu hata hiyo mitambo yenyewe ya kufulia umeme hawana.

Uongo una expiry date

Mvua zikinyesha hadithi zinaamia kwenye mitambo chakavu, nyaya kukatika, hujuma sijui za watu kuharibu transformers wakiiba mafuta na story zingine. Mvua zisipo nyesha mabwawa hayana maji.

Ni story kila kukicha ambazo sio constant kabisa zinabadilika na mazingira; kukikosekana utunzi kabisa wa kutunga Magufuli aliharibu.
Tatizo unajadili sana nje ya muktadha hadi unaharibu mtiririko wa mjadala wenyewe. Unajiundia hoja & maswali na kujijibu mwenyewe.

Kujadili kwa namna hii huwa siwezi, kwa maana ya kama kuanza mjadala mpya kwenye kila comments. So, nikuache uendelee na wengine.

Ova
 
Tunachokiweza kuzalisha chawa wakimpigia chapuo kila kukicha
 
Ulichoandika ni sahii
Tatizo lolote lile lilianzia mahali ni kama kupanda mti utakaa baada ya miaka kadhaa ndo utaanza matunda

Sawa na tatizo ukilifumbia macho ni swala la mda tu litaanza kuonekana matatizo mengi ya sahivi chanzo ni magufuli

Na angekuwepo watu wangeumia sana sababu angetumia nguvu badala ya akili kuyakabili
Umefanya reference ya UVIKO?
 
Kitu gani cha maana ulichoandika AI

Nimekuuliza umeona wapi duniani services ya mashine ya kufulia umeme inafanyika kwa miaka mitatu. Umekazana Magufuli alikuwa analazimisha. Ina maana Magufuli ana miezi sita toka afe au? Toka hizo hadithi za Magufuli alikuwa afanyi services mitambo January alipo pata uwaziri sasa hivi ni miaka mingapi?

Unataka kutuambia services ya mitambo ni zaidi ya miaka mitatu; sasa kujenga itakuwa miaka mingapi.

Kwa kifupi mambo uliyoandika ni ya kukaririshwa tu programmed, but hakuna logic ya hoja given the time pass toka kifo cha Magufuli kupokea hizo lawama tena za kutunga.

Uongo una expiry date
Watanzania sijui mnafikiri vipi. Unajua matatizo makubwa huanzia mbali sana. Kuna matatizo tunapata saa hii kwasababu ya vita ya Kagera, unajua hilo na huwa inakuwaje? Mmezoea sana kufikiri leo tu, mambo yanaanzia mbali sana. Kuna mambo Tanzania tunateseka hadi leo kwasababu ya siasa za Mwalimu za Ujamaa.
 
Back
Top Bottom