Matatizo mengi tuliyonayo nchini leo yameanzia na awamu ya tano; hapakuwepo na uhuru wa kusema wala kurekebisha mambo, sasa tunalipa kwa maumivu

Matatizo mengi tuliyonayo nchini leo yameanzia na awamu ya tano; hapakuwepo na uhuru wa kusema wala kurekebisha mambo, sasa tunalipa kwa maumivu

Tatizo la uhaba wa sukari sio la kuanzia December mwaka jana kama unavyofikiri! Ni tatizo la kitambo kidogo na linatokana na kuyumba kwa sekta ya biashara na viwanda iliyotokana na uongozi mbovu miaka 7 iliyopita! Nani asiyejua jinsi biashara na wafanyabiashara walivyoharibiwa biashara zao na mitaji yao wakati wa Magufuli? Biasahara nying zilifungwa ikiwa ni pamoja na mipaka yetu. Uhusiano wetu na majirani zetu ndio Samia amepambana na sasa unaanza kurudi. Uongozi wa Mgful ulisababisha matatizo mengi na mengine bado tutayashuhudia miaka ijayo.
Mimi nafikiri utakuwa na shida kidogo kichwani mwako hakika kuna kitu huyo Magufuli kakufanya si bure yani hadi akili za kusikiliza kaondoka nazo?Kwa hiyo sio kuzidi kwa mvua tena 😂😂😂 na sio matengenezo ya mashine za viwanda vya TPC na Mtimbwa? Kwa hiyo Bashe ni muongo kabisa?😂😂 Sio kuzudi kwa maji kutokana na mvua?
Aisee naomba niishie hapa kwakweli!
 
Mapumbavu yaliyoshindwa siku zote hutafuta wa kumlaumu au sababu ya kuhalalisha kushindwa kwao .
 
Mimi nafikiri utakuwa na shida kidogo kichwani mwako hakika kuna kitu huyo Magufuli kakufanya si bure yani hadi akili za kusikiliza kaondoka nazo?Kwa hiyo sio kuzidi kwa mvua tena 😂😂😂 na sio matengenezo ya mashine za viwanda vya TPC na Mtimbwa? Kwa hiyo Bashe ni muongo kabisa?😂😂 Sio kuzudi kwa maji kutokana na mvua?
Aisee naomba niishie hapa kwakweli!
Sijui kama unafahamu kuwa Kilombero Sugar walikuwa na wakati mgumu sana wakati wa Magufuli na sasa ndio wanarudi tena katika hali ya kawaida.
 
Sorry ni awamu ya 5 ya bullzoda sio ya nne! Awamu ya 4 ilikuwa baba wa demokrasia.

Kabla ya 2015 angalau kulikuwa na uhuru wa kusema, ukweli ulijulikana na uliachwa usemwe kwa kiasi kikubwa, na wataalamu waliachwa watumie taaluma yao kutoa miongozo, lakini alipokuja Magufuli yeye aligeuka kuwa engineer, docta, mchumi, na kila kitu.

Kuna mambo mengi watanzania wenye akili nyepesi nyepesi hawawezi kuyaona. Matatizo mengi tuliyonayo sasa hivi kama uhaba wa dola, umeme, ukosefu wa sukari n.k. yalitokana na utawala wa kuburuza mambo wa awamu ya tano.

Mfano umeme: Wakati wa Magufuli mashine nyingi za kufua umeme kwa kutumia gesi zilifanya kazi na kupitiliza wakati wake wa kufanyiwa ukarabati. Tanesco walilazimika kuendelea kufua umeme na mashine zilizokuwa zinahitaji kufanyiwa ukarabati kwani Tanesco wangeondoa baadhi ya machine ili kufanya ukarabati kungesababisha upungufu wa umeme na mgao kitu ambacho kingepelekea wao kufukuzwa kazi mara moja. Hivyo waliendelea kuzalisha umeme na mashine zilizokuwa hoi.

Leo karibu nusu nzima ya mashine za kufua umeme wa gesi pale Ubungo na Kinyerezi zimeharibika kwa mkupuo baada ya kulazimishwa kufanya kazi zikiwa mbovu! Matokeo yake leo hii tuna mgao ambao hata viongozi wetu hawana lugha nzuri ya kuulezea; watasema ni upungufu wa mvua hata pale ambapo El Nino zilikuwa tele kuanzia mwaka jana mwishoni. Hutasikia wakisema ukweli huu kuhusu ubovu wa mashine zitu, utawasikia wakisema ni ongezeko la matumizi ya umeme, hilo nalo ni uongo tu.

Matatizo ya sukari na dola yana mkondo huo huo. Nani asiyejua namna Magufuli alivyoharibu biashara kwa kuwabambikizia kodi wafanyabiashara, kuwapora mitaji na kuwalazimisha kufunga biashara zao kwa visingizio vya kodi? Matokeo ya hayo ndio leo tunayaona. Biashara kati ya Tanzania na nchi za nje ilidorora mno wakati wa Magufuli. Si mnakumbuka jinsi Magufuli alivyowachukia "mabeberu"? Unategemea nini kibiashara unapowachukia bussiness partners na kufunga biashara zao nchini?

Ila kwakuwa watanzania wengi wamelishwa uongo na hawana jinsi ya kugundua uongo huo basi wataamini kuwa Magufuli angekuwepo mambo yangekuwa mazuri. Nawaambia, saa hii tungekuwa kwenye hali ya tahadhari na majanga makubwa kiuchumi na kijamii. Magufuli hakuwa na upeo mkubwa kiuchumi, yeye alilazimisha kila kitu kama alivyopenda bila kujali matokeo yake. Leo tunateswa na matatizo ambayo chimbuko lake ni awamu ya 5 na hakuna kiongozi atakayetuambia ukweli huu!
Nakazia
 
Back
Top Bottom