Tatizo letu kubwa bongo ni kukosa respect kwa rule of law, ninaaamini siku tutakapoelewa hilo na kulitimiza, the rest vitafuata vyenyewe.
Law ipi?
ya serikali inayotumia mabilioni COMORO huku inashindwa kuchonga bara bara kule mufindi?
hili vugu vugu unaloliona katika jf, na katika duru mbali mbali za wananchi ni miongoni mwa viashiria chanya kwamba jamii ya watanzania imeanza kuona kwamba some thing must be done.Ndugu Gamba la nyoka,
Nakubaliana na wewe kuhusu ubovu wa systems(mifumo) tuliyonayo na haja ya kuisuka upya(hapo waweza rejea mada yangu ya pasaka ya Tanzania haijawadia bado,ambamo nilidokeza baadhi ya mifumo ya kubadilishwa). Hata hivyo swali kuu linabaki, ni nani atafanya huo usukaji upya? Katika mchango wako unasema inabidi tu...je, ni watanzania wote tuhusike katika hili, tuanzie wapi tuanzeje na lini tuanze, na tena wako wapi hao wa kuongoza mageuzi hayo? kwa ufupi bila watendaji hapo huoni tutabaki kuwa na good wishes tu?
Tanzania bado hatujajifunza kuheshimu sheria, in fact inaonekana kuna sheria mbili, moja ya matajiri na viongozi, nyingine ya masikini, as the results waliotuibia kwenye Richimonduli, wameishia kujiuzulu tu, huko BOT wameambiwa kuzirudisha tu hela walizoiba, that is what I am talking about, maana tukiendelea hivi, hata siku moja hatutakuja kupata maendeleo wala mabadiliko muhimu kwa taifa letu, na ni kwenye hiki kipengele cha kukosa respect kwa rule of law, ndipo tunapoishia kupata viongozi wengi wabovu ambao wanavizia weakness zetu kwa sheria na kununua uongozi, ndio maana ninasema Tanzania tunahitaji only one big step forward, nayo ni kuheshimu utawala wa kisheria.
Nafikiri hiii sio mahali pake hapa, si kuna thread yake tayari mkuu, au?
GT Comoro AU inafoot bill, kwa hiyo hakuna issue ya Tanzania kutumia hela.
GT Comoro AU inafoot bill, kwa hiyo hakuna issue ya Tanzania kutumia hela.
mzizi ni malezi!.Aidha,kama tuna watawala na wanajamii wasioheshimu sheria, chimbuko la tatizo hilo ni nini(mzizi wa fitina) ili tuuchimbue usiendelee kulitesa taifa?
hili vugu vugu unaloliona katika jf, na katika duru mbali mbali za wananchi ni miongoni mwa viashiria chanya kwamba jamii ya watanzania imeanza kuona kwamba some thing must be done.
kwa kuanzia tu, lazima tufanye reform kubwa katika suala la Chakula nchini. wananchi wakishiba hawatababaishwa na wanasiasa uchwara na takrima zao, wakishiba watafanya kazi zenye tija, wakishiba watafikiri na kuvumbua au kuboresha.
then lazima tufanye reform katika elimu, elimu yetu inageza mifumo ya kizungu na output ni watu wachache wenye theory nyingi kichwani lakini mchango usiotosha katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo, watu wanashabikia vyeti badala ya uwezo, ndo maana watu wako radhi kuchongesha vyeti bila kujali kuulizwa utaalamu wao ni upi?.
hizi front mbili ukianza nazo utagundua kwamba nyingine zinategemea sana hizi mbili.
tunaweza pia kuwa na jeshi dogo lakini la kisasa, ambalo tutalipa vifaa vya kutosha na vya kisasa, halafu gharama itakayopunguzwa iingizwe katika elimu bora.
Ndugu mahesabu,
Ahsante sana kwa kuchangia mada.Jambo ulilolitaja la ajira ni kweli ni moja ya mambo ambayo yanapaswa kutazamwa sana. Ni kweli pia kwamba serikali inao wajibu wa kutimiza hapa. Lakini hapo kuna tatizo ndani ya tatizo,serikali ya viongozi hawa hawa ambao co mission yao ni kujinufaisha tu wao wenyewe. Labda useme wazi serikali ipi ya watu wapi.Aidha, nikudokeze kuwa mbali na sekta ya umma ambayo inaongozwa na serikali, katika sekta binafsi,hususan ile inayooshikiriwa na wawekezaji toka nje,wamekuwa wakitaja kwamba nchini kwetu kuna uhaba wa raslimaliwatu wenye ujuzi unaoendana na shughuli ambazo wawekezaji hawa wanakuja kufanya.Tatizo linadaiwa kuwa kubwa kiasi kwamba wanalazimika kuja na watu wao toka ng'ambo. Hapo napo lazima tutafute dawa.
Vile vile fikiria juu ya sekta kuu inayowaajiri vijana wetu kwa sasa hasa hasa mijini(uchuuzi au umachinga), je hii ni sekta sahihi na kama si sahihi mbadala ni nini, je,tuwaelekeze vijana wetu katika sekta kama vile kilimo?
Hatujachelewa sana, tunaweza tukaamka tukiamua. Tunapaswa kuanza kuweka mfumo utakaweka bayana wajibu wa serikali na rai wake. Kwa sasa ni kama vile wananchi wanaamini kwamba serikali inapaswa kuwafanyia kila kitu na serikali nayo inafikiri kwamba haiwezi kufanya lolote bila michango ya wananchi. Matokeo yake: wananchi wanailaumu serikali na serikali inawalaumu wananchi. Palipotakiwa kupeleka hela za kodi hatupeleki, pale ambapo hatukutakiwa tupeleke ndipo tunatupeleka.
Ili tuanze safari yetu ya kujikwamua na madubwana tuliyojitengenezea tunahitaji uongozi. Uongozi hauwezi kuwa huu wa CCM ambao wanasema hata chanzo cha umaskini hawajui. Kwa hiyo tunarudi kulekule, hatua yetu ya kwanza kabisa ya kutoka hapa tulipo ni kuiweka CCM pembeni, tuanze na chama kingine. Sasa tutazunguka weeeeeeee, ukweli unabaki palepale bila kubadilisha chama (mfumo), tutaendelea kucheza mdori na hii forum itajaa malalamiko yetu mpaka ipasuke.
Kwa hiyo basi mada hii inapaswa, pamoja na mambo mengine haya, kujadili:
i) namna ya kuwa-mobilise wananchi waelewe hatari wanayozidi kujitengenezea kwa kuendelea kuichagua CCM
ii) namna ya kuwatia ujasiri wanasiasa wenye mwelekeo, uzalendo na uwezo wa kiuongozi kujiunga na upinzani ili kuimarisha na kuvijenge taswira chanya vyama vya upinzani ikiwa ni njia ya kuviandaa kupambana na CCM na hatimaye kuongoza mabadiliko tunayotaka
Summary: adui wetu hapa ni CCM. Fursa peke tuliyo nayo wa kummaliza huyu adui ni uchaguzi. Silaha yetu hapa ni kura za wananchi. Jemadari wetu ni upinzani. Kazi yetu hapa JF ni kumpa mafunzo huyo jemadari ili aje atuongoze katika kumteketeza adui.
Summary: adui wetu hapa ni CCM. Fursa peke tuliyo nayo wa kummaliza huyu adui ni uchaguzi. Silaha yetu hapa ni kura za wananchi. Jemadari wetu ni upinzani. Kazi yetu hapa JF ni kumpa mafunzo huyo jemadari ili aje atuongoze katika kumteketeza adui.