Matatizo ya Tanzania na mapendekezo ya wana JamiiForums

Kyoma,

Ndugu yangu maelezo yako mazito lakini kuna sehemu ambazo kusema kweli siziafiki kwa sababu umechukulia ki juu juu tu bila kuzama zaidi kutazama matatizo ya nchi yetu. Kifupi naweza kusema maelezo yako mengi ni theory ambazo tumejifunza - academic lakini unapokuja kutana na nchi kama Tanzania mshikaji hazifanyi kazi kama hakuna marekebisho ktk kifungu cha tatu na nne.(Ili tuendelee)

Ni kweli kama alivyosema Nyerere ili tuendelee tunahitaji vitu vinne.

WATU, wenye uwezo wa kuzalisha - na sio tena wenye uwezo wa kufanya kazi, maanake leo hii sio tena serikali mwajiri wetu (Investor). Kwa hiyo tunahitaji wananchi wenye kutoa ajira -Uwekeshaji. lakini hutuwezi kupata hili ikiwa la tatu na nne hayafanyi kazi zake.
ARDHI, hii tunayo tena inatisha kwa utajiri wake, ngoma imesimama ktk kifungu cha tatu na nne.

Hivyo basi kama ulivyosema vitu vyote hivi vinategemeana sana na huwezi kupunguza moja hata kidogo. Tunawanyooshea viongozi wetu kwa sababu hilo la tatu SIASA SAFI na nne UONGOZI BORA vyote vinatokana na Utawala uliopo madarakani. Kwa bahati mbaya sana yaliyoandikwa na uwajibikaji wa haya matakwa ya maendeleo ni vitu viwili tofauti kabisa.

Siasa safi kama tunavyoiona leo hii sio tena siasa ya chama kimoja! lakini mengi bado yamekumbatia chama kimoja!.. hakuna changes kubwa toka mfumo wa Nyerere hadi huu uliopo. N kweli wananchi tunao uwezo wa kuchagua ni siasa gani itakayo tuletea maendeleo kulingana na mazingira yetu!..lakini sidhani kama kuna mmoja wetu hapa anaweza kusema kwa Uhakika kama siasa za CCM, Chadema au CUF ndizo bora zaidi kwa sababu kuna mapungufu mengi ktk sheria inayowafunga viongozi ktk utekelezajiwa hizi sera. Siasa za CCM zinasema tofauti na yale wanayoyafanya! - Ujamaa na Kujitegemea imebakia kuwa itikadi isiyobebeka ni mzigo kwao lakini bado inatumika sana ktk harakati zao za uchaguzi na wananchi wanajenga matumaini kuwa labda sasa hivi kweli tumepata viongozi.
Ni ktk ujenzi wa hizi siasa ndipo tunapokutana na sheria ambazo zinawafunga wote VIONGOZI na WANANCHI kuwajibika.
Kyoma sheria zetu ni msumeno butu ambao haufai kabisa ktk ulimwngu huu wa Utandawazi. Sheria nyingi bado zinajenga mfumo wa chama kimoja tawala ambacho hakina makosa. Ikiwa chama hakina makosa basi na wote waliomo ndani yake hawana makosa na hakuna mahakama wala sheria inayojengwa nje ya matakwa ya chama hicho acha mbali utekelezaji wake.

Ndugu Kyoma umezungumzia swala la IPTL na RADA ukalifafanisha na swala la Jack Abramoff. Kyoma Jack kachukua fedha nje na kuziingiza Marekani hakufanya hivyo kuuza mali ya Marekani na wala hakuna uhujumu wa uchumi wa Marekani. Kwa taarifa yako, rais wa Marekani hutoza fedha kumwona na wapo ma - lobbyist ambao kazi yao ni kuunganisha appointment za kumwona rais. Huyu lobbyist anafahamu kiwango kinachotakiwa na Ikulu ama rais kwa hiyo anaweka percent yake, still fedha hizi zinaingia Marekani hazitoki nje.
Hapa sisi tumesimama kama Gabon ambao wana kila haki ya kumuuliza huyo rais wao Omar Bongo kuhusu matumizi ya hizo millioni 9 kumwona Bush. Kifupi ndugu Kyoma huyu rais kashika madaraka toka 1967 hadi leo na kisha kabadilisha kabisa mfumo wa siasa nchini humo (chama kimoja). Gabon hakuna demokrasia kabisa na hatujasikia Bush wala mjomba wake wakisema wataivamia nchi hiyo! wala hakuna mtu anayemzungumzia kabisaaa dunia nzima! Walioumia hapa ni raia wa Gabon ambao wamenyang'anywa haki zao kwa sababu tu Al Ustadhi Bongo anakula na mzee mkubwa.
Viongozi wa nchi za Magharibi wanakiuka sheria ndogo sana na hufanya siri kubwa sana kwa sababu sheria yao ni msemeno kweli, na mara nyingi utakuta matatizo yao ktk RUSHWA haya HUJUMU uchumi wa nchi yao. Tanzania rushwa letu linahujumu Uchumi wa nchi na hakuna sheria wala uharaka wa uwajibikaji. Leo hii scandal za IPTL, Rada, Richmond tunaombwa wananchi tuzisahau ili tugange yanayokuja!..

Mengine yote ndugu yangu nipo nawe mia kwa mia ila nachotaka kusema ni kwamba KATIBA ni sheria ambayo inatuongoza sote na ikiwa katiba yetu ina mapungufu kibao sidhani kama tunaweza kupata SIASA SAFI na pia UONGOZI BORA toka vyama vyetu. Tutapiga kasia weee lakini chombo kinaelekea kwenye maporomoka kwani mshika usukani hafanyi kama inavyotakiwa.
Ebu tazama, ni watanzania hawa hawa kwa mamillioni leo hii wapo nchi za nje na wanafanya kazi kama wajinga vile.. masaa 16 na wanafuata sheria za nchi hizo kama vile hawakutoka Bongo... WHY?... hawa hawa WATU ambao walikuwa wazembe wasiowajibika Tanzania leo hii ni wafanya kazi hodari wanaojituma nchi za nje!..
Nadhani sababu kubwa ni nafasi yao ktk utendaji kazi imejibiwa vizuri kutokana na kuwepo kwa Siasa safi na Uongozi bora.
Navyoamini mimi ndugu yangu mzazi bora ni yule anayetoa malezi mazuri kwa mwanaye kwanza kabla na mtoto ni matunda ya malezi hayo. n kwa sababu hizo nyumba huwa inasifika kwa maendeleo ya watoto wakitazama uwajibikaji wao..
 
Ndugu zangu, leo nina swali. Watanzania tunataka kujenga Taifa la Kisasa, Taifa ambalo watu wake wanafurahia maisha ya kisasa na kufurahia haki sawa na nafasi sawa ya mafanikio. Hata hivyo ukiangalia jinsi Taifa letu linayokwenda ni vigumu kuelewa kama kuna mtu anajua ni wapi tunataka kwenda na tutafika vipi huko.

Mwanzo wa Jamhuri yetu tulikuwa na dira yaani "kujenga Taifa la Kijamaa kwa misingi ya Kujitegemea". Na katiba yetu hadi hii leo bado inatamka lengo hilo hilo. Zaidi ya yote na Katiba ya Chama tawala cha Mapinduzi nayo bado inatangaza kuwa siasa yake ni ya "Kijamaa". Hata hivyo hali halisi ni kinyume na hivyo, hali halisi ni kuwa tumeingia kwenye mfumo wa Kibepari kinyume na Katiba yetu. Kama sivyo, bila ya shaka hatujaweza kisomi kuchanganua na kufafanua ujamaa tunaojenga sisi ni wa aina gani.

Na zaidi ya yote kwa vile hatuna dira inayotuongoza na viongozi wetu wameshindwa kutuambia kama sisi ni wajamaa au mabepari, ni vigumu kujua ni kitu gani tuwekee kipaumbele. Je, sisi ni mabepari na hivyo tuwekee mkazo utafutaji na upatikanaji wa mtaji (mabilioni ya Kikwete???) au sisi ni wajamaa na hivyo tuangalie zaidi ni jinsi gani njia kuu za uzalishaji mali zinaweza kurejeshwa mikononi mwa umma?

Na kama tunataka kujenga uchumi wa kisasa ni eneo gani la uchumi tulilitie mkazo? Je ni kilimo (ambacho hudaiwa kinaajiri watu wengi zaidi) au ni madini (sekta ambayo inaingiza fedha nyingi za kigeni pamoja na utalii)?

Je tutilie mkazo elimu ili tuweze kujenga watu wenye uwezo na ujuzi wa kiteknolojia na hivyo kujenga Taifa ambalo msingi wake ni Teknolojia? Au tuweke kipaumbele chetu kwenye viwanda vikubwa ili na sisi tuwe kama Kenya, Ujerumani, China n.k.

Je, Taifa lisilo na kipaumbele, lisilo na dira linajengwa vipi? Ni nani atupe dira hiyo na ni nani atuchagulie kipaumbele?
 
MKJJ

pasipo na kipaumbele matokeo siku zote huwa mabaya, wana zuoni walishasema kama hujui uendako, haijalishi njia gani utapitia, hi ni sawa na taifa pasi na vipaumbele tataendelea kuongozwa na kauli mbiu, fagio la chuma, ukweli na uwazi, ari nguvu na kasi mpya ........

Kama taifa ni lazima tukubaliane nini vipaumbele kama taifa, pili kila mkoa lazima uweke vipaumbele ambovyo vitakuwa endelevu.

Tukifanikiwa na hilo vyama vya siasa vijenge hoja na mkakati dhabiti kuendeleza vipaumbele hivyo
 
Kipaumbele chetu kwasasa ni kupita kuomba misaada kwa wafadhili kwani hatujitoshelezi hata kwa bajeti ,pamoja na hao tunaowaita wafadhili kupitia makampuni ya kutoka kwao kuchuma matrillioni ya dollars kutokana na vilivyomo kwenye Ardhi yetu.Hapo ndiyo uwezo wetu wa kufikiri ulipokoma kwasasa ,hadi tutakapolielEwa hili na kulitafutia ufumbuzi endelevu basi kipaumbele chetu kitaendelea kuwa Tusaidieni Na Njooni Muekeze tuna masharti nafuu 3% kwa mrahaba............nk!
 
And what is vision 2025? Huwa nasikia tu watu wa quote...kuna yeyote anayo.iwe attached hapa? It common practise ya vitu ambavyo wananchi wanahitaji kuelimishwa kuishia kwenye bookshelves za wakubwa! Please I am serious I have no idea what the vision entails. au kama kuna website naweza ku download..tupatie please
 
Brutus

Nashukuru kwa hii link, nimeisoma ila hii document iko too general, na haijibu swali la MKJJ.

Kitu nilichoarajia kukikuta kwenye hii document, ni Country comparative advatage ni kitu gani watanzania tunaweza kujivunia na kujitangaza duniani kwamba sisi ni mahiri.

Madini tuna hazina kubwaa lakini tumeshapigwa bao, tanzanite yapatiaka tanzania pekee lakini kwenye nchi tatu bora zinazouza tanzanite kwa wing duniani hatumo.

Utalii tunahazina kubwa sana ya mbuga za wanyama, lakini jirani zetu kwnya wameshajiwahi kwa hili, mzee kibaki alipokuwa bara asia mwishoni mwa mwaka jana alikuwa busy kufanya maongezi na wadau wa utalii, na moja ya mikakati ya kuanzisha safari za moja kwa moja kutoka bara asia mpaka kenya, tutaishia kunawa kula hatuli ng'o.

Elimu kwa hili bado tunafanya masihara, chuo kikuu cha dar es saalaam hasa kitivo cha sherila ni lulu, afrika mashariki, wanafunzi wengi wa kenya na uganda wanandoto ya kusoma sheria mlimani, kama tumeliona hilo kwanini tusiimrishe sekta ya elimu, tutengeneze comparative advantage kwenye elimu, ebu angalia nchi kama UK inaaingiza Pound ngapi kwenye elimu.

Kilimo.........................

Maisha baora kwa kila mtanzania hayajengwi kwa kauli mbiu na hotuba majuukwaani, maisha bora yatapatikana kwa kujitoa muhanga na kuwa wabunifu na kuweka vipaumbele
 
kama itawezekana tunaomba mtu aweke na MKUKUTA na MKURABITA ili tuweze kuisoma, inawezekana tukapata majibu huko.
 
Nd. Quarz!
Attached is the copy of MKUKUTA!
I will do my best to find MKURUBITA's copy ASAP!
(Majina yanachekesha huh!)
Just kidding!
 

Attachments

kuna kitu hapa kimejificha nacho ni mfumo nzima wa fedha na utawala ambao ndio msingi wa utekelezaji wa majukumu ya kila siku kwa mtazamo wangu.

1. kimsingi kabisa wananchi kupitia serikali zao za mitaa,kata,hata halimashauri zao zimekuwa hazina mapato yao kama sehemu ya jamii husika.hili limesababisha kuwepo na jamii ambayo aina mbele wala nyuma hata kama sehemu husika wanautajiri wakupindukia.

2. mfumo wa sasa ambao umezoeleka mapato yote wanakusanywa na kupelekwa hazina na kisha serikali kuu kuanza tena kuzigawa kupitia wizara zake.kwa mtindo huo siyo rahisi kwa serikali kuwa na kipaumbele katika kuendeleza jamii husika zaidi ya kununua vitu vya anasa na semina zisizokwisha.(kwa mfano halimashauri ya temeke ni tajiri sana kwa maana ya kuwa na vianzo vingi vya mapato kuliko ilala na kinondoni,lakini ndio wilaya ya mwisho kimaendeleo ktk mkoa wa dar)hili ni eneo moja tu katika maeneo mengi nchini tz.

3. utawala mzuri ambao kwa sasa bado ni kiini macho,ndio tuna serikali za mitaa lakini hazina mamlaka ya kutosha ya kujiendesha(kwa maana ya kuwa na viazo vya mapato na kupanga mambo yao wenyewe bila mkono wa serikali kuu.kwa maana ya kuwashirikisha wananchi husika katika kupanga mambo yao wenyewe na kujua nini waanze katika mwaka na nini wamalizie.hapa ndipo utaona madiwani wanapofanya kazi katika sehemu zao nasio kama ilivyo sasa kazi ni kuwinda posho za vikao tu, na kupandikiza chuki za kisiasa tu.

4.serikali kuu, ingerejesha mikataba yote iwechini ya sehemu kusika(mfano madini kule yanapojimbwa hizo sehemu ndio zinapashwa kuingia hii mikataba kwa niaba ya serikali na sio kama ilivyo hivi sasa.)

5.halimashauri zote zingekuwa zinalipa asilimia fulani ya mapato yake serikali kuu tofauti na ilivyo hivi sasa pamoja na kuwa na jivipato vidogo wanatakiwa kubakia na 2% heti kwa ajili ya maendeleo .
 
Swali lililoletwa na MKJJ Bado halijajibiwa na mkukuta nilipopitia document ya mkukuta kuna mpngo mwingine umeoonyeshwa humo kwa kifupi 'Tanzania min Tiger plan 2020' mwenye hii document naomba aiweke barazania labda itakuwa na majibu
 
Mini-Tiger Plan 2020 haikujibu swali lolote la Nd. Mwanakijiji!
Hii plan ilitumika kutengeneza Special Economic Zones, kama njia mbadala ya kufikia malengo ya VISION 2025. Lakini sina hakika kama inatiliwa mkazo wala kuzungumziwa tena kama ilivyo MKUKUTA na MKURUBITA, hasa katika awamu hii ya nne ya utawala!
 
Hapa kazi ipo, tena si ya kitoto, kuna uwezekano tunakwenda tusiko kujua, kama taifa halina dira na vipaumbele safari yetu kwenye dunia ya utandawazi ni ya mashaka
 
Nd. Mgumu,
Utandawazi ni kama kucheza mduara!
Lazima uangalie tabia na hali ya wachezaji!
Huwezi kucheza na kila mtu, wengine wana tabia mbaya!
Watakushika mak*#@lio!

Inabidi tuwe makini na game la utandawazi!
Kila mtu anaangalia maslahi yake, kama hailipi anakula kona anatafuta panapofaa!
Watendaji wetu inabidi waongeze lenses kwenye glasses zao!
 
Nd. Mwanakijiji!
Labda niongeze kidogo hapa!
Mikakati ipo, sema utekelezaji ndo michosho!
Usanii mwingi!
Kuna mtu humu alitoa wito humu JF kwamba vijana wazalendo wajitokeze kugombea nafasi za uongozi.. nadhani ilikuwa point ya maana sana!
Nchi yetu inahitaji damu mpya!
hatuwezi ku-survive katika karne hii ya 21 iliyojaa ushindani wakati watendaji bado wanaogelea kwenye dunia ya kufikirika ya karne ya 19!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…