Matatizo ya Tanzania na namna ya kuyatatua

Matatizo ya Tanzania na namna ya kuyatatua

salum mbepwa

New Member
Joined
Apr 9, 2020
Posts
3
Reaction score
0
Mapungufu yanayopatikana Tanzania na jinsi ya kuyasuluhisha ni kama ifuatavyo:-

Sekta ya Afya
Kwenye sekta ya afya kina baadhi ya sehemu serikali imefanikiwa ila kwa asilimia kubwa kina mapungufu mfano hospitali nyingi na zahanati zina upungugu wa madaktari, manesi, sawa na upungufu wa vitanda. Pia kwenye sekta ya afya selikali imefeli kwenye utoaji wa huduma kwa watu wanaotumia bima kwani bima inatoa huduma chache wakati malengo sahihi ya bima inatakiwa mtu apate huduma zote za msingi pasipo kuchagua pia kwenye sekta ya afya kuna uhaba wa zahanati upande wa vijijini jambo linalopelekea watu wa kijijini kuteseka pindi wanapokuwa wanaumwa.

Changamoto nyingine ni uhafifu wa magari ya dharura kama vile ambulance.

Sekta ya kilimo
Hii ndiyo sekta mama mana asilimia kubwa ya Watanzania wanatumia na kutegemea kilimo kama ndo chanzo cha mapato, ila sekta ya kilimo ni sekta ambayo imetelekezwa haijachukuliwa kwa umakini sababu ina changamoto nyingi sababu wakulima wanakumbwa na changamoto nyingi sana kama uhaba wa pembejeo, uhaba wa mbegu bora uhaba wa madawa na kubwa kuliko ni wakulima hawana elimu iliyosahihi juu ya kilimo.

Serikali haijawekeza sana kwenye kilimo jambo linalopelekea wakulima kutopata mazao ya kutosha. Kwenye hili suala ni lazima serikali itilie maanani; itasaidia kukuza sekta ya kilimo.

Utawala bora na uwajibikaji
Hii ni katika sehemu ambazo zina maupungufu makubwa. Utawala bora na uwajibikaji hamna kwa viongozi waliopo serikalini. Mfano Mtu anaweza kufanya kosa akiwa kazini badala ya kushitakiwa anahamishwa sehemu ya kazi.

Jambo hili siyo sahihi; mtu aliyekosea inapaswa awajibishwe kwa uzembe wake.

Upatikanaji wa viongozi wa umma
Miongoni mwa changamoto zingine ni upatikanaji wa baadhi ya viongozi kama waziri mkuu, wakurugenzi wa halmashauri, mawaziri, wakuu wa mikoa, makatibu wa mikoa, wakuu wa wilaya. Hawa wote wanateuliwa na Rais, jambo linalopelekea kutopata viongozi walio bora bali watafanya kwa mapenzi aya rais.

Yapaswa Rais kupunguziwa majukumu yake itasaidia kuleta maendeleo.

Uchumi na biashara
Katika nchi ya Tanzania kina mzungumkuti kwenye uchumi viongozi wanasema uchumi umepanda ila kwa wananchi sana hali ngumu uchumi wao unazidi kuzorota; biashara zinafungwa sababu ya makato na kodi nyingi toka selikalini wastani wa biashara10 zinazofunguliwa biashara 7 zinafungwa.

Selikali inabidi ibuni vyanzo vya mapato ila sio kuwskandamiza wananchi jambo hilo linafanya kuzorota uchumi kwa wananchi

Haki za binadamu
Moja ya changamoto kubwa ambayo wananchi wanakumbana nayo ni haki za binadamu sababu viongozi wanapovunja haki za binadamu hukimbilia kujitetea kuwa watu kudai haki sawa ni kulazimisha ndoa za wenyewe kwa wenyewe. Sheria zinatumika vibaya, jambo linalopelekea kupoteza haki zao mwisho wa siku wanafungwa ndani muda mrefu alafu wanaachiwa wakiwa wamepotezewa muda wao.

Mfano mashehe wa Uamsho, Erick Kabendera na kuibuka watu wasiojilikana hii yote ni kuondoa haki za binadamu.

Sayansi na teknolojia
Nchini Tanzania sayansi na teknolojia sio ipo chini ila tatizo selikali haiwainui watu ambayo wanakuwa wabunifu sababu ambayo inapelekea wagunduzi kukata tamaa ila kama hawa watu wangekuwa wanapewa nguvu na selikali wangekuwa mbali sana.

Maendeleo ya jamii
Ili kuwe na maendeleo lazima kwenye jamii kuwa kuba amani na raia wawe wawe wanapatana pia kuwe kina ushirikiano baina ya watu mbalimbali lazima selikali iwaunganishe wawe na umoja.

Demokrasia
Ili nchi yoyote iwe na maendeleo ni lazima kuwa na demokrasia na msingi wa demokrasia lazima iundwe katiba mpya ambayo itasaidia kulindwa kwa demokrasia na kuwepo na uchaguzi wa haki baina ya pande zote mbili kwa Tanzania pasipo katiba mpya hakuna demokrasia.

Serikali ikifanyia mambo kama haya kwa kiwango chake inaweza pelekea maendeleo.
 
Back
Top Bottom