Matatizo yote haya yanatokea, Je! Kazi ya Mungu ni nini?

hazole1

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2015
Posts
4,319
Reaction score
3,916
Kenya wamekufa watu 150 ambao hawana hatia na kuna watu wanasema kumuua kafiri sio dhambi. Je ni Mungu ndio anasema hivyo au watu wanajitungia na ilikuweje mungu aliumba kafiri, kwanini asiwe anawasaidia hata makafiri wasiuwawe?
 
Katika mada ambazo zitakua na wachangiaji wachache ni hii yako mkuu hazole1…ni swali zito sana na ni swali muhimu sana!!ngoja nimalize kazi zangu nitarudi ila kwa kifupi navyojua mm mungu yupo neutral na hana emotions nikimaanisha huruma,furaha,kukasirika, ni sehemu ya emotions(mihemko),kwa sababu mungu hana hiyo sifa ndio maana kila kinachotokea kinatokea katika mechanism yake ya kimaumbile bila kuingiliwa na nguvu kutoka nje…kwa mungu hakuna baya na zuri otherwise mambo kama haya yasingetokea ingawa dini nyingi zinamzungumzia mungu kama kiumbe chenye mihemko kuna time anakasirika kuna time anahuruma kama mungu angekua hivi dunia ingekua safi sana kusingekua na tajiri na masikini,walemavu na wazima,mzuri na mbaya…ila kama nilivyoanza kusema mada hii ni nzuri ila ni ngumu sana kueleweka!!
 
Kenya wamekufa watu. 150 ambao hawana hatia na kuna watu wanasema kumuua kafiri sio dhambi je ni mungu ndio anasema hivyo au watu wanajitungia na ilikuweje mungu aliumba kafiri kwanini asiwe anawasaidia hata makafiri wasiuwawe

Humjui Mungu we2,tatizo ni watu kutotii maagizo yake hayo ndiyo matokeo.Mrudieni Mungu.Ajali zinatokea kwa sababu gani?
 
Usiwe mvivu wa kufikiri wewe!!tafakari kilichowakilishwa ndo uandike!
 
Kama Yesu aliteseka na kufa tena kwa kusingiziwa pasipo na hatia akiwa ni mwana wa Mungu itakuwaje kwangu mimi na wewe? falsafa yake iko wazi,waovu kama akina Baraba wataachwa na kuonekana mashujaa katika utawala wa ibirisi wakati wasio na hatia watateswa na kufanyiwa kila unyama ili maana harisi ya ufalme wa mbinguni ipatikane, kuuona ufalme wa mbinguni si njia nyepesi wala ya huruma,ni lazima mwili uumie na kuumizwa ili uippnye nafsi na ukiogopa kuumizwa mwili tu ukataka kuonewa huruma basi jua nafsi haitapona ...Mimi na wewe yatupasa kuifata njia ya Yesu msalabani,kwani yeye alikuwa na hatia gani?
 
Hii mada inatakiwa ijibiwe Na mtu Mwenye ilimu ya kitabu aswa,,,ila hii ni mitihani ya M/mungu kwetu waja wake,,,ndo maana ht firauni aliwaua watoto wa kiume wa ban Israel kwa kuhofia Tu asije akazaliwa mtt wa kiume akaja poka ufalme wake Kama ilivyosemwa ktk vitabu vya dhama izo,,,lkn kumbe ule ulikuwa mtihani kwa bani Israel Ili Tu mungu atimize ujio wa nabii wake mussa, KWAIYO UENDA HAYA YANAYOTEKEA INAWEZEKANA NABII ISSA AU YESU,,YU KARIBU KURUDI KM ILIVYOSIMULIWA KTK VITABU VYA MUNGU,,,,,,,,PINGA UGAIDI HAUFAI.....
 
Laiti mngalijua yale yaletayo amani...... my people are perish for the lack of knowledge...... Mungu hawezi ingilia uhuru wa mtu tena hasa kwa wale wasio mcha... .. angeingilia uhuru wako imagine leo mngemzungumziaje????
 
Katika mada ambazo zitakua na wachangiaji wachache ni hii yako mkuu hazole1…ni swali zito sana na ni swali muhimu sana!!ngoja nimalize kazi zangu nitarudi ila kwa kifupi navyojua mm mungu yupo neutral na hana emotions nikimaanisha huruma,furaha,kukasirika, ni sehemu ya emotions(mihemko),kwa sababu mungu hana hiyo sifa ndio maana kila kinachotokea kinatokea katika mechanism yake ya kimaumbile bila kuingiliwa na nguvu kutoka nje…kwa mungu hakuna baya na zuri otherwise mambo kama haya yasingetokea ingawa dini nyingi zinamzungumzia mungu kama kiumbe chenye mihemko kuna time anakasirika kuna time anahuruma kama mungu angekua hivi dunia ingekua safi sana kusingekua na tajiri na masikini,walemavu na wazima,mzuri na mbaya…ila kama nilivyoanza kusema mada hii ni nzuri ila ni ngumu sana kueleweka!!
ni kweli mkuu
 
Ugumu zaidi unakuja pale ambapo mtoa mada anajichanganya Pasi na kuonyesha dunia wanayoishi mazombies ambao hawana free will na wenye usawa wa maumbile na fikra pia.
Maana katika dunia hii ambayo wale wavivu wa kufikiri hawaielewi Mungu aliumba na kuweka binadamu walio sawa huku wakiwa na fikra tofauti pamoja na mitazamo tofauti ikishadidiwa na Uhuru wa kuamua na kuchagua.
Na Uhuru wa kifikra ndiyo msingi wa tofauti zilizopo.
 
Kenya wamekufa watu. 150 ambao hawana hatia na kuna watu wanasema kumuua kafiri sio dhambi je ni mungu ndio anasema hivyo au watu wanajitungia na ilikuweje mungu aliumba kafiri kwanini asiwe anawasaidia hata makafiri wasiuwawe

Kumbuka Mungu alisema tuwe waangalifu na manabii wa UONGO .Wewe peke yako uwe na akili ya kuchagua mabaya na mazuri .Usimsikulize au mfurahishe binadamu.Mfurahishe Mungu na fuata masharti Yake ukienda kinyume unajikuta unaangukia mikononi mwa shetani .Kazi ya shetani ni uharibifu
 
wewe ni nani unaehoji kazi ya Mungu? hivi huelewi kuwa matendo ya Mungu hayachunguziki? hivi hujui kuwa Ayubu alikuwa akimwabudu Mungu siku zote but Mungu aliruhusu ajalibiwe na shetani kwa kuuwa mifugo yote, na watoto wote wa ayubu pamoja nakumpa Majibu mwili mzima? ndugu zangu tusijidanganye Mungu haziakiwi.

Swala la kuuwa kwa watu 150 kule kenya inaweza tu ikawa ni njia ambayo Mungu anataka kufundisha Jambo kwa wanadamu ambao bado tupo hai...moja ya mambo muhimu ni TOBA, KUSALI NA KUOMBA KILA WAKATI Maana hatujui siku wala saa ya kuondoka kwetu hapa duniani. Pia kumbuka hapa duniani si mahala salama na sio sehemu sahihi ya kuishi binadamu, bali makao rasmi ya Mwanadamu ni Mbinguni.
 
Laiti mngalijua yale yaletayo amani...... my people are perish for the lack of knowledge...... Mungu hawezi ingilia uhuru wa mtu tena hasa kwa wale wasio mcha... .. angeingilia uhuru wako imagine leo mngemzungumziaje????
Ni kweli mkuu
 
Hii mada inatakiwa ijibiwe Na mtu Mwenye ilimu ya kitabu aswa,,,ila hii ni mitihani ya M/mungu kwetu waja wake,,,ndo maana ht firauni aliwaua watoto wa kiume wa ban Israel kwa kuhofia Tu asije akazaliwa mtt wa kiume akaja poka ufalme wake Kama ilivyosemwa ktk vitabu vya dhama izo,,,lkn kumbe ule ulikuwa mtihani kwa bani Israel Ili Tu mungu atimize ujio wa nabii wake mussa, KWAIYO UENDA HAYA YANAYOTEKEA INAWEZEKANA NABII ISSA AU YESU,,YU KARIBU KURUDI KM ILIVYOSIMULIWA KTK VITABU VYA MUNGU,,,,,,,,PINGA UGAIDI HAUFAI.....

Asante kwa darsa. Ban Israel ndio nini sheikh?
 
Kenya wamekufa watu. 150 ambao hawana hatia na kuna watu wanasema kumuua kafiri sio dhambi je ni mungu ndio anasema hivyo au watu wanajitungia na ilikuweje mungu aliumba kafiri kwanini asiwe anawasaidia hata makafiri wasiuwawe

Acheni kukengeuka vijana.,Mungu ni Idea ya mwanadamu katika harakati za kutafuta asuli yake.There is nothing real exist known as god.
 
Yapo mambo mengi sana yamefichwa ili kupumbaza dunia na ulimwengu kwa ujumla. Ukitafakari sana na kutafuta majibu unaambiwa dhambi hayo ni mambo ya imani. Mfumo ndiyo ushajengwa kihivi ya kwanba ukitaka kutafuta na kujua ukweli ni dhambi. We amini tu bila kuhoji.
 
Kumbuka maneno ya shadrack na garnebo, " wewe haumfahamu mungu wetu na haufahamu mahusiano yetu, mahusiano yetu hayajajengeka kwa kujibu maombi yetu, akijibu nimungu wetu na asipojibu ni mungu wetu" maana yake ni kwamba mumgu ni mungu, ajulikane au asijulikani haimpunguzii yeye kua mungu, ni mungu na atabaki kua mungu
 
Yapo mambo mengi sana yamefichwa ili kupumbaza dunia na ulimwengu kwa ujumla. Ukitafakari sana na kutafuta majibu unaambiwa dhambi hayo ni mambo ya imani. Mfumo ndiyo ushajengwa kihivi ya kwanba ukitaka kutafuta na kujua ukweli ni dhambi. We amini tu bila kuhoji.

Ni wazazi wako wanakwambia upuuzi huo ? Nawe umeambiwa kuhoji ni dhambi kweli umeamini ? Hapo tatizo nilako ndugu...
 
Ugumu zaidi unakuja pale ambapo mtoa mada anajichanganya Pasi na kuonyesha dunia wanayoishi mazombies ambao hawana free will na wenye usawa wa maumbile na fikra pia.
Maana katika dunia hii ambayo wale wavivu wa kufikiri hawaielewi Mungu aliumba na kuweka binadamu walio sawa huku wakiwa na fikra tofauti pamoja na mitazamo tofauti ikishadidiwa na Uhuru wa kuamua na kuchagua.
Na Uhuru wa kifikra ndiyo msingi wa tofauti zilizopo.

Free will is a fraud.

Mtu ambaye kaua na anataka kurudi nyuma katila muda ili ajirudi asiue na yule aliyemuua aendelee kuishi ana free will gani ya kufanya hivyo?

Kama mungu yupo na anapenda sana kuwapa watu free will, mbona hakitupa free will hiyo?

Na kama yupo na hakutupa hiyo, kweli tuna free will?

Kuna watu wanezaliwa na genes zinazowalazimisha kuwa namna fulani, hapo kuna free will?

Wale watoto wanaouawa kwa natural disasters wana free will gani ya kifanya maamuzi ili mabaya yasiwakute?
 
Back
Top Bottom