Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,890
- 26,440
Matendo ya kikatili ya kupiga raia na kuwajeruhi au kuwaumiza ikiwemo kuwapa majeraha ya kudumu au wakati mwingine majeraha yaitwayo "Life changing injuries", yaonyesha mapungufu makubwa yaliyopo katika mafunzo ya polisi hususan chuo cha Polisi Moshi.
Matendo ya kinyama ya askari polisi ya kupiga raia kama wakata kuni na vichaka au kusafisha shamba kwa fimbo, virungu na mateke si matendo ya kibinadamu na yanozingatia weledi hata kidogo.
Imefika wakati sasa kukawepo mwongozo wa kisheria kwa polisi popote pale wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao. Mwongozo huu utakwenda sambamba na sheria ya polisi ambayo itaongoza na kukumbusha nguvu ya polisi na mipaka yao.
Ni jambo la maana sana endapo waziri wa mambo ya ndani akaangalia sheria ya polisi na uhalifu yaani Policing and Crime Act ambapo endapo polisi watapiga raia kwa makusudi au kwa minajili ya kuwasababishia majeraha ni lazima polisi alehsika awajibike kwa kutofuata mwongozo, hapa twazungumzia kitu chaitwa accountability and operational procedures.
Kwa matukio yanoendelea ya kuumiza raia, kuwapiga na kuwasukuma pasipo kuguswa na raia hao ni wazi kwahitajika chombo ambacho kitasimamia na kuangalia utendaji wa shughuli za jeshi la polisi au (police conduct regulation) hivyo polisi akigundulika hakufuata mwongozo na sheria itampasa kuwajika kwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu (hii ni police conduct and disciplinary procedures.).
La mwisho, mwongozo wa kisheria na uendeshaji wa kesi a jinai au makosa ya jinai. Ni kweli polisi wana haki ya kisheria ya kutekeleza majukumu yao (statutory and common law powers) kwenye kuhakikisha kuna utulivu na amani lakini pia sheria hizi ni lazima zihakikishe polisi wetu wanawajibika endapo watavuka mipaka ya utekelezaji wa kazi yao na waheshimu haki za raia pale wanapokuwa wakiwadhibiti raia hao.
Itafika wakati jeshi la polisi khasa chuo cha polisi Moshi kiwajibike kwa kuhakikisha chapata wanafunzi bora wa uaskari polisi na ambao wakitoka chuo hapo huwa wamewiva kwa kuzingatia sheria khasa ile ya kawaida yaani common law,sheria zonoongoza kazi yao (policing laws and regulations) na nguvu ya polisi katika kutekeleza majukumu yao yaani "police powers and Procedures".
Bila kuangalia chuo cha polisi Moshi na mitaala yake kama yazingatia utendaji bora wa askari walofuzu chuoni hapo, basi tutaendelea kushuhudia askari polisi ambao ni kichekesho kwa jamii na wanojenga uadui uso lazima na ambao hawaonekani kuwa ni askari polisi mwenye weledi.