Matengenezo matatu ya magari ambayo kila mwenye gari anapaswa kujua

Matengenezo matatu ya magari ambayo kila mwenye gari anapaswa kujua

Gari kutowaka husababishwa na hitilafu kwenye betri za gari, spark plugs, car starter au pampu ya mafuta.
Sasa kwa issue ya gari yako ambalo linawaka likiwa kwenye Neutral na sio kwenye Parking, basi hapo neutral safety switch inaweza kuwa na tatizo.
Nadhani haujamuelewa, anamaanisha kuwa anapokuwa amewasha gari yake.... Ule mkono wa gear unakuwa katika eneo la parking kwenye dashboard zile taa za herufi, kwenye parking haiwaki inakuws kiza

Ila akitoa kwenye parking na kuweka kwenye sehemu ya drive au neutral inawaka.... So inampa shida kujua kuwa ameshaiweka kwenye drive (D) ama la.

Kwakifupi akiweka gear kwenye parking, kwenye dashboard ile taa haionyeshi inakuwa imezima as if gari imezimwa but hapo hapo akiihamishia gear kwenda kwenye Neutral inawaka......
 
Msaada: Maana na Matumizi sahihi ya OD (Overdrive)
Afu pia humu JF zipo Threads nyingi zinazozungumzia kuhusu O/D. Ila kwa msaada kidogo pitia haya maelezo:
OD-Button.jpg

OVERDRIVE O/D
Overdrive (OD) ni gia katika mfumo wa gari ambayo huifanya gari kuwa katika spidi kubwa huku mzunguko wa injini ukiwa mdogo. Kwa lugha rahisi, OD ni gia ya mwisho inayokupa mwendokasi. OD hukupa mwendo wa kasi, uliotulia lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (revolutions per minute rpm). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi.

Overdrive ni kama gia ya ziada inayokupa mizunguko mingi ya driving shaft kwa mizunguko michache ya injini yako. Unapaswa kuitumia ukiwa unatembea mwendo mkubwa. Faida zake utatumia mafuta kidogo, maana gari inakwenda kasi kwa mizunguko michache ya injini.

Mfano katika gari ya kawaida yaani 180km/h ili ufikishe spidi 120 basi RPM inaweza ikawa 4000rpm katika barabara ya tambarare. Lakini ukiweka overdrive unaweza kutembea spidi hiyo hiyo kwa rpm 2000 katika barabara ya tambarare.

Utatambuaje kama Overdreive (OD) ipo on au off?

Pindi uonapo kitaa cha overdrive kwenye dashboard ya gari yako, inamaanisha kuwa overdrive ipo off na pindi kitaa hicho kisipoonekana basi tambua kuwa overdrive ipo on. Overdrive imewekwa kama chaguo (option) la kutumia wakati ukiwa unatembelea spidi chini ya 60km/h.

Unaweza kutumia ukiwa unataka kuipita gari nyingine, mathalani kwenye milima ambapo gari yako inakuwa imepunguza nguvu, hivyo unaweza kuiweka off (hapa unakuwa kama umerudisha namba 4) na injini itabadili kasi ya mzunguko, utaiweka ukishamaliza tena matumizi yake.

Eneo lingine, ni mara gurudumu la gari lako linapopasuka. Ikitokea hivyo, unaweza kuondoa OD, huku ukiwa umeacha kukanyaga pedeli ya mafuta, kwa maana ndiyo utakuwa unaomba mwendo upungue pasi na kukanyaga breki. Katika hali kama hii, utakuwa umesaidia kupunguza mwendo wa gari wakati ukithibiti muelekeo wa gari pia.

Katika hali kama hii huwa wanakanyaga breki. Kufanya hivi ni hatari, maana unasimamisha kabisa mwendo wa gurudumu lililopasuka, na matokeo yake mwendo wa gari, badala ya kwenda mbele, itajaribu kutii amri ya gurudumu linalogomea gari kwenda mbele na kuamua kwenda upande wa gurudumu lililopasuka, nikiwa na maana kwamba hapo gari itakuwa inaacha njia na au kupinduka.

Kwa giaboksi zenye kujibadili zenyewe, ni vema basi tukaziacha OD zijiendeshe zenyewe, maana kuziondoa hatari yake ni kuwa unaweza kusahau kuiweka tena unapokwenda zaidi ya km 70 kwa saa, mfano barabara ya Nyerere, na kusababisha matumizi makubwa ya nishati ya kuendeshea mtambo.
Kitaa cha Overdrive kikiwa hakionekani kwenye dashboard yako maana yake Overdrive ipo Automatic au on na hivyo ndivyo inavopendekezwa na wataalam gari iwe automatic pindi upo mjini na unatembelea speed tofauti (sometimes less or more than 60)..kwa vile overdrive inatumia gia kubwa na mwendokasi chini ya 60km kwahiyo unaweza kutumia wakati unashuka milima mikubwa.
 
Nadhani haujamuelewa, anamaanisha kuwa anapokuwa amewasha gari yake.... Ule mkono wa gear unakuwa katika eneo la parking kwenye dashboard zile taa za herufi, kwenye parking haiwaki inakuws kiza

Ila akitoa kwenye parking na kuweka kwenye sehemu ya drive au neutral inawaka.... So inampa shida kujua kuwa ameshaiweka kwenye drive (D) ama la.

Kwakifupi akiweka gear kwenye parking, kwenye dashboard ile taa haionyeshi inakuwa imezima as if gari imezimwa but hapo hapo akiihamishia gear kwenda kwenye Neutral inawaka......
Naamini pia Umeelewa nilicho kieleza apo...
 
Namimi pia Umeelewa nilicho kieleza apo...
Nimekuelewa vema. Wewe unazungumzia matatizo yangari kutokuwaka kwa maana baada ya jupiga starter. Mwenzako Nazungumzia kile anachokiona katika dashboard yaani vile vitaa vinavyokupa taarifa kuwa sasa hivi ule mkono wa gear umekaa sehemu gani pale pembeni yako dereva.

Sasa wewe umeongelea mswala ya plug sijui nozel..... Hizi zinahusiana nini na bulb kwenye dashboard.... Au nikueleweje kwa ulichoniuliza hapa kwenye hii comment yako ya leo?!
 
Soma vizuri usiishie sentensi ya kwanza we soma mpaka mwisho nimeweka na probably cause.
 
Wadau nina ist ya 2006, juzi niliipiga sehemu radiator ikapinda ikagusa fan na kuzuia fan kuzunguka... Kulikopelekea motor kuungua.

Baada ya motor kuungua fan ikashndwa kuzunguka na mashine ikaanza kuheat.

Shida yangu ni kuwa nishaweka motor zingine kama 2 hivi na bado injini inaheat kwa kilometer chache tu hata 30 hazifiki na maji yanaisha kabisa.

Nb.
Rejeta haivuji, sasa hapa solution ipo vipi.
Je kuna aina ya moto special kwa hizi gari, au fan special,. Na ni wapi naweza nikaipata na kwa gharama gani maaana nateseka saana na nina safari. Ya kwenda bukoba week ijayo.
 
Back
Top Bottom