Matengenezo ya Daraja la Kigongo Feri mpaka Busisi kulikoni?

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Jana tarehe 19/9/2023 nilipitia kivuko cha Kigongo Ferry mpaka Busisi, na kwa kawaida unapopitia pale utaona kazi zinavyofanyika kwa ajili ya matengenezo la daraja linalounga Kigongo Feri na Busisi.

Kwa masikitiko yangu sikuona chochote kinachofanyika pale kama vile watu wamehama au wako likizo. Tumeaminishwa na Serikali kuwa muda siyo mrefu daraja litakamilika. Kulikoni?

Taarifa ya Ujenzi - Ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo-Busisi) wafikia 85%
 
Walikuwa wameenda lunch🤣
 
Ccm wapo kusini skuizi
 
Hili limama linafikiria kuuza nchi kwa kupambwa na machawa wake! sio maendeleo!
 
Wanasubiria zege likauke
 
Alafu sio matengenezo..shughuli inayofanyika pale ni ya UJENZI WA DARAJA ...matengenezo ni sawa na kusema una fanya ufundi kwa kitu ambacho kilipata hitilafu
 
Haters kwa michuki hii mnaweza kujikuta mtajifungua njiti haki ya nani mamamameeee!
 
Ulipita Saa ngapi? Mchana 12:00pm to 1:30pm kwenye kampuni ya CCECC inayotenga daraja la JPM ni muda wa mapumziko.
 
Wanasubiri expansion joint zikauke kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…