Material hizi zimepitwa na wakati

Material hizi zimepitwa na wakati

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
704
Reaction score
2,435
Ni hulka ya binadamu kujaribu kufanya vitu vizuri, watanzia tulio wengi tunajipima na tunapimwa mafanikio kimaisha kupitia ujenzi, ukionekana pesa inapita mikoni mwako lakini huna nyumba inayoonekana ni nzuri utakosolewa sana na kupuuzwa kwa kiwango fulani, katika kuzunguka kwangu tanzania, nimejifunza baadhi ya material za ujenzi zinazopatikana kwa wingi mikoani zimepitwa na wakati.

Ukizitumia unaonekana wewe bado sana na hili limefanya ujenzi uwe very very complicated na unapoteza fedha nyingi kiasi kwamba hizo fedha ungezitumia kwingine huenda ungekuwa umetoboa, endelea kuorodhesha vifaa vilivyo pitwa n wakati ili hata sisi wa mikoani tusiendelee kuvitumia mimi nilivyoona vimepitwa ni hivyo,

1. Bati jeupe (huku niliko linaitwa bati la mama mjane)
2. Cement laini inayopigwa sakafuni
3. Chokaa inayopigwa ukutani
4. Maramaru zenye maua
5. Ceiling board
6. Mlango wa chuma
7. Wire za fensi ( wanaita senyenge na waya nyingine
8. Dirisha la mbao
 
Chokaa imepitwa na wakati kutokana na washindane wake waliokuja ambao ni white cement na baadaye wall puty.

White cement na wall puty wamemzidi chokaa uwezo wa kutengeneza smoothness ukifanya skimming kwa ajili ya maandalizi ya upakaji rangi.Nawasilisha hoja
 
Dirisha la mbao limepitwa na wakati kwa sababu kuu mbili moja ni aesthetic property na function failure.Dirisha La mbao litaruhusu hewa pekee kuingia ndani lakini dirisha la kioo litaruhusu hewa na mwanga na pia linaongeza urembo kwenye nyumba
 
Ceiling board ni Kama dirisha la mbao tu sababu zilezile. Kwenye function gypsum board anamzid ceiling board uwezo wa kudiffuse sauti pia urembo
 
Hivi nawezaje kuzuia fungus wa kwenye ukuta? Nmepiga rangi ya mafuta inabanduka tu, km ukuta unaoza
 
Dirisha la mbao limepitwa na wakati kwa sababu kuu mbili moja ni aesthetic property na function failure.Dirisha La mbao litaruhusu hewa pekee kuingia ndani lakini dirisha la kioo litaruhusu hewa na mwanga na pia linaongeza urembo kwenye nyumba
Naona dirisha la mbao ni zuri liki dizainiwa vizur

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom