GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Inasemekana, magereza ya Tanzania ni tofauti sana na ya Ulaya na nchi zingine "zilizostaarabika". Mfungwa wa Ulaya hukoseshwa uhuru tu wakati wa Tanzania hunyimwa karibia kila kitu: uhuru na mahitaji mengine muhimu ya kumwezesha kuishi kama binadamu wa kawaida.
Inasekana, magereza ya Tanzania ni kama mahali pa kuwakomolea watu. Kuna wafungwa wengi wanaodaiwa kufungwa kwa uonevu.
Inasemekana, magereza ya Tanzania hayazingatii haki za binadamu. Hata mfungwa anapowasili gerezani kwa mara ya kwanza, hukaguliwa kwa namna isiyozingatia utu. Huvuliwa nguo zote na kuamriwa kuruka kichura. Inamaanisha Serikali imeshindwa kununua vifaa vya kisasa vya kukagulia wafungwa kistaarabu?
Inasekana, magerezani kumejaa uonevu baina ya wafungwa na wafungwa, n.k.
Inasemekana, viongozi mbalimbali wameshatembelea magerezani na kusikiliza malalamiko ya wafungwa lakini malalamiko yao huwa kama yanayoishia hewani. Hayafamyiwi kazi.
Inasekana, mahalli wanakolala wafungwa ni pabaya sana. Magodoro ni machache kuliko idadi ya wafungwa.
Kwa ufupi, mbali na magereza kumpokonya mfungwa uhuru wake, jambo ambalo ni sahihi kama mahakama itajiridhisha kuwa anastahili hiyo adhabu, pia ni kama maeneo ya mateso.
Hayo mateso yanawasaidia wafungwa kujirekebisha au yanawafanya kuwa sugu?