Mateso ya Masheikh wetu

Mateso ya Masheikh wetu

Status
Not open for further replies.

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MATESO YA MASHEIKH WETU

Ananiambia, ‘’Nakwenda sijda natamani nilie kwenye sijda lakini nyoyo hizi ngumu zimekufa ganzi na pengine hata kuta zake zimesinyaa machozi ya wapi ndugu yangu?

Nanyanyuka natazama picha ya Sheikh Ponda katika pingu yuko mahakamani askari magereza anamfungua pingu zake.

Naiambia nafsi yangu pingu hizi kafungwa Sheikh Ponda si kwa kuwa ni jambazi, la hasha, kafungwa pingu hizi kwa kupigania haki za Waislam na wao waheshimike na wapewe kile ambacho wamekuwa wakikipata wengine toka uhuru upatikane mwaka wa 1961,

Naiambia nafsi yangu Sheikh Ponda yamemkuta yale kwa kupigania kile ambacho Waislam walikifikiria watakipata walipokuwa wanapigania uhuru wa Tanganyika.

Taratibu machozi yanatoka nafungua ukurasa mwingine nawaangalia masheikh wetu waliokuwa kifungoni kwa miaka takriban saba hawana kosa lolote na kesi inaahirishwa kwa miaka saba.

Sasa machozi utadhani bomba limefunguka.

Mume wangu anasikia kwikwi yangu ananifuata na kunipa glasi ya maji napokea.

Hasemi lolote kwani kazoea sasa na anajua kinachoniliza.

Nasoma dua na yeye ndiye muitikiaji wangu.

Mwanangu mkubwa siku moja kaniuliza, ‘’Mama unagombana na baba?

Nakusikia usiku unalia.’’

Wakati mwingine nawaona masheikh wengine katika runinga wamevaa kanzu nzuri za kupendeza kwa rangi zake na kofia za kumeremeta na makoti ya thamani juu wametupia kashda wako katika meza kuu na wakubwa wa chama serikali.

Nyuso zao zinang’ara kwa vyakula na vinywaji vizuri.

Inanijia picha ya masheikh wetu wako Segerea wanalalia virago na kupata shida zote za gerezani.

Nawafikira watoto na wake zao huko waliko na shida hizi za maisha.

Najiuliza hawa masheikh wengine vipi wanaweza kuoga na kujipara na kula na kunywa na wale ilhali ndugu zao wako jela wanateseka?

Tuko mezani na mume wangu na watoto wakati wa chakula cha jioni.

Runinga inawaleta masheikh wengine wamekaa na wale wamependeza wanacheka na kufurahi.

Nikiwafikiria masheikh wetu chakula kinanitumbukia nyongo nanyanyuka kimya kimya sitaki wanangu waone nalia nakwenda chumbani kujificha.

Mume wangu ananiambia, ‘’Honey usimsikilize Sheikh Mselem bin Ali akitafsiri Qur’an anakuliza na usidhani kuwa mimi siumii naumia sana lakini mimi mwanamme naweza kujikaza.

Usimsikilize Sheikh Mselem anakuliza Allah anakuelewa.’’
 
Angalia picha:
Screenshot_20200831-164253.jpg
Screenshot_20200831-163947.jpg
 
Sheikh Mohammed Allah akulipe kila lakheri!

Ni wachache sana wenye imani na huruma kama wewe, siku hizi waislamu JINA wako wengi tu, utamuona mtu kakuvalia kanzu na kofia kumbe mnafiq mkubwa, ndio ujue wengi wao wako kimaslahi na si kwa ajili ya Allah na kuwasaidia waislam.

Kikwete na Mohamed shein wote hawa ni waislamu, je walishindwa nini kuwatoa hawa masheikh kama ni waumini wakweli na wanamuogopa Allah SW! Viongozi wa bakwata pia kazi kumsifia mkulu tu mpaka anatolewa mfano kwa manabii, huku wamekaa kimya kuhusu masheikh.

Ivyo Waumini ni wachache sana, wengi wao wapo kidunia tu.
 
Mzee wangu habari yako.

Naomba kusema kuwa mimi siungi mkono kabisa unyanyasaji huo kama kweli unafanywa dhidi yao.

Pili naomba kukuuliza mzee wangu kuwa hawa mashekhe wakati wanahubiri unadhani walikuwa wanatumia haki ya kikatiba vizuri ?
Safuher,
Kesi itakaposikilizwa na hukumu kutolewa ndipo ukweli utajulikana.

Lakini inavyoelekea ni kuwa masheikh wetu hawana kesi ya kujibu wako rumande kwa miaka saba.
 
Sheikh Mohammed Allah akulipe kila lakheri!

Ni wachache sana wenye imani na huruma kama wewe, siku hizi waislamu JINA wako wengi tu, utamuona mtu kakuvalia kanzu na kofia kumbe mnafiq mkubwa, ndio ujue wengi wao wako kimaslahi na si kwa ajili ya Allah na kuwasaidia waislam.

Kikwete na Mohamed shein wote hawa ni waislamu, je walishindwa nini kuwatoa hawa masheikh kama ni waumini wakweli na wanamuogopa Allah SW! Viongozi wa bakwata pia kazi kumsifia mkulu tu mpaka anatolewa mfano kwa manabii, huku wamekaa kimya kuhusu masheikh.

Ivyo Waumini ni wachache sana, wengi wao wapo kidunia tu.

Muhimu washatakiwe na sheria iachwe ifanywe kazi sio kuwashikilia Kwa sababu hakuna ushahidi wa kuwashtaki
 
Kwa kusema haya ndugu yangu haiwezi kuwa na wewe unajiweka katika hatari ya kukamatwa na kufungwa bila hukumu?
Capitano,
Nani wa kuogopwa?

Allah au binadamu?
Nikamatwe kwa kosa gani?

Nikamatwe kwa kuikumbusha serikali kuwa inafanya makosa yanayohitaji kurekebishwa?

Hili si kosa.

Ikiwa serikali itanikamata kwa kuitahadharisha basi itakuwa serikali ya kidhalimu.
 
Amani ya nchi hii ni bora mara mia kuliko uhai wa magaidi wachache. Bado nasisitiza hawa wanyongwe haraka. Wewe mleta mada funga domo kabisa yaani hata usiote tena hoja kama hizi. Msitumie uislamu kama kichaka. Huyo Ponda mwenyewe wanamlea sana angeshatua ahera long time. AMANI YA TANZANIA NI BORA KUKIKO DINI. Povu ruksa.
 
FISI ni fisi tu mla mizoga kamwe hawezi kuwa binadamu.

Wenzako wanahoji kwanini hao masheikh wasipelekwe mahakamani, ili haki itendeke yaani kujua kama wanayo makosa kinyume chake wewe unaongea utumbo!!!.

Mtu anawekwa rumande kwa miaka 7 bila kufikishwa mahakamani au kuhukumiwa hiyo ni sawa katika nchi inayofuata misingi ya kisheria na haki za binadanu??!!!.
 
Amani ya nchi hii ni bora mara mia kuliko uhai wa magaidi wachache. Bado nasisitiza hawa wanyongwe haraka. Wewe mleta mada funga domo kabisa yaani hata usiote tena hoja kama hizi. Msitumie uislamu kama kichaka. Huyo Ponda mwenyewe wanamlea sana angeshatua ahera long time. AMANI YA TANZANIA NI BORA KUKIKO DINI. Povu ruksa.

Hayo yalifanyika Somalia wakati wa Siad Barre na Adhabu iliyokuja ndio mpaka leo tunaiyona kaanza kuondoka Raisi na wakafuatia wengine na mpira unaendelea

Ishara za TZ kuja adhabu tunaziona , labda hatujachelewa hizi dhuluma zifutwe na haki itendeke na kuomba msamaha , vyenginevyo tusubiri mateso ya karne nzima
 
Amani ya nchi hii ni bora mara mia kuliko uhai wa magaidi wachache. Bado nasisitiza hawa wanyongwe haraka. Wewe mleta mada funga domo kabisa yaani hata usiote tena hoja kama hizi. Msitumie uislamu kama kichaka. Huyo Ponda mwenyewe wanamlea sana angeshatua ahera long time. AMANI YA TANZANIA NI BORA KUKIKO DINI. Povu ruksa.

THIBITISHA KUWA NI MAGAIDI
KWA MIAKA SABA UMESHINDWA JAPO KUPATA TONE YA UGAIDI WAO
KAMA WEWE UNAO USHAHIDI PELEKA
 
Sheikh Mohammed Allah akulipe kila lakheri!

Ni wachache sana wenye imani na huruma kama wewe, siku hizi waislamu JINA wako wengi tu, utamuona mtu kakuvalia kanzu na kofia kumbe mnafiq mkubwa, ndio ujue wengi wao wako kimaslahi na si kwa ajili ya Allah na kuwasaidia waislam.

Kikwete na Mohamed shein wote hawa ni waislamu, je walishindwa nini kuwatoa hawa masheikh kama ni waumini wakweli na wanamuogopa Allah SW! Viongozi wa bakwata pia kazi kumsifia mkulu tu mpaka anatolewa mfano kwa manabii, huku wamekaa kimya kuhusu masheikh.

Ivyo Waumini ni wachache sana, wengi wao wapo kidunia tu.

Masheikh wetu hawana kesi ya kujibu wako rumande kwa miaka saba.
 
Kwani nyie Mungu wenu kawaagiza kutafuta nini duniani hapa hicho 'ambacho wengine wanakipata' na mtakwenda nacho huko peponi?
HAKI ipi mnaitaka duniani hapa na nani haonewi?
 
Wa kulaumiwa sana katika hii kadhia ya Masheikh ni Rais wa Zanzibar Dr Shein, kwani yeye anao uwezo wa kusema Masheikh hao warudishwe Zanzibar kuhukumiwa au wapewe dhamana huko Zanzibar au waachiliwe.

Bara tumekuwa kama "dog" tuliyeamrishwa na "master" wetu Zanzibar kuwafunga watuhumiwa kinyume na haki kwa miaka 7.

Shame on Us.
 
Mshukuruni JK lasivyo wangeshakua marehemu na kuwasahau.
nasema hivii watatunzwa Hadi pale tutapoona sio kitisho tena

Sheikh Abud rugo wa Mombasa marehem uamsho ndani cost imetulia
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom