BAVICHA Taifa
Senior Member
- Jul 25, 2013
- 117
- 661
Na John Pambalu
Mara milango ya gereza ikafunguliwa. Askari akasisitiza acheni simu zenu na Muingie watu 4 tu. Tukaambatana na viongozi wawili wa chama wilaya ya Mbeya mjini, mimi pamoja na Kamanda Mwaipaya tukaingia ndani ya lango la Gereza.
Mwenyekiti umekuja?. Ilikuwa sauti ya Mdude aliyekuwa akichechemea na urefu wake huku akiinamia mkono wake wa kushoto. Mwenyekiti umekuja?, aliuliza kwa mara ya pili, sikumjibu kitu nikiwa mwenye moyo wenye huzuni nikimuona kamanda akichechemea kuzikabili nyavu zinazotenganisha mahabusu/wafungwa na watu wanaokwenda kuwaona.
Wamesema ninafanya biashara ya madawa ya kulevya, ninayasafirisha kutoka Pakistan. Sijui nilikuwa nasafirishaje Tanzania na Pakistan ilihali hata passport ya kusafiria sina kamanda, alisema Mdude.
Oh! Mwaipaya ni wewe kamanda, umehitimu mafunzo ya gereza. Hongera sana kamanda, naamini kuna kitu umejifunza. Moja kati ya faida kuu ya jela ni kukufanya uwe na ujasiri wa kukipigania kile unachokiamini. Najua sasa wewe ni jasiri. Alimueleza Mdude.
Makamanda wamenipiga, wananiuliza kwa nini ninaisumbua serikali? Walikuwa wamevalia mizura wamenipiga kamanda. Walinipiga nikiwa naumwa, walinitoa kwenye Zahanati ya jela nikiwa mgonjwa wakaja kunisulubu nje huku wafungwa wenzangu wakishuhudia. Wamenipiga alirudia tena akizungumza huku akiwa mwenye ujasiri na akizungumza kwa sauti ya ushupavu.
Ninachokiamini mimi, sikumkosoa Magufuli kwa kuwa nilikuwa namchukia, hapana. Wala sikumkosoa kwa sababu ya sura yake, bali kwa sababu ya uovu wa mfumo wa Serikali yake. Najua Mungu ni mkubwa ipo siku nitatoka.
Nikasogelea zaidi nyavu zinazotutenganisha. Nikamwambia Mhe. Freeman anakusalimia, akaniambia msalimie Mwamba mwambie naisubiria kwa hamu hotuba yake. Nikamwambia Mhe. Mnyika anakusalimia, akaniambia najua amewaandikia barua wenye mamlaka kuhusu madai yangu ya kuteswa gerezani, nimeambiwa. Wamekuja kuniomba radhi nikawaambia tutayamaliza nilikoyasemea.
Wakazungumza na Mwaipaya na kupeana vifungu vya biblia, nikamrudia nikamwambia kuna vitu kadhaa tumekuletea, wana wamekuchangia fedha kidogo. Akasema wapeni wanaonipikia chakula wanajua nini cha kufanya. Wamefanya kazi nzuri sana sijawahi teseka. Waambie watanzania ninawapenda
Aluta continue akatueleza akirejea ndani ya gereza akivuta mguu wake.
Tukaachana naye kulikabili Gereza la Songwe lililopo zaidi ya kilometa 100 kutoka mjini mbeya wanakoshikiliwa wapiganaji wenzetu wapatao 60, kati yao wanaume 53 na wanawake 7 Gereza la Songwe. Wengi wao wakituhumiwa wa kesi za mauaji na uhujumu uchumi.
Leo tutahitimisha ziara yetu katika mahakama huku mkoani Njombe kusikiliza kesi ya mauaji inayowakabili viongozi wetu, akiwemo Mhe. George Sanga Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Njombe.
Unaweza kuchangia chochote kwa ajili ya mahitaji kwa wafungwa wenzetu kwa 0746 777 845 Voda Jina Twaha Mwaipaya
Wasalaam
John Pambalu
jpambalu@gmail.com
0676250710