Mateso ya wana daresalama yalivyoandikwa na msimulizi mnoko.

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Posts
7,491
Reaction score
8,304
Wakati ule amri ilitolewa na mfalme wa jiji kuwaita wote waliotelekezwa pamoja na watoto wao.
Hata walipofika ndani ya praitorio akainuka Bashite akawaambia, amani iwe kwenu enyi wakina mama kwa kuwa nimeyaona mateso yenu!!hamtahangaika peke yenu tena. Basi wakapaza sauti wakisema "walete,walete!wasulubishe".Naye akawauliza,"niwasulubishe waume zenu?"wakamjibu sisi hatuna mume ila Bashite,kila ajifanyaye kuwa mume wetu humfitini makamu" .
 
Nao wakazi wa mji wakamshangilia mkuu wao wakisema Ubarikiwe ee mkuu sana abarikiwe na baba yako Kipara maana enzi ya enzini ni yake milele.Ndipo wakuu wa wale watumishi majoho meupe wakatahayari wakainamisha nyuso zao wakaondoka vichwa chini kwa huzuni huku wakipiga piga vifua vyao
 
Kabla ya machweo ya alfajiri kuwia walionekana pia wavaa majoho ya kijani wakiranda randa maeneo ya hekalu la Yule nabii aliyetabiri kuondolewa Kabisa mabusha katika ufalme wake...soma waraka wa kwanza kwa wafuasi wa Yule mtawala Mkuu 2015 Aya ya kumi na mbili
 
Naye mkuu wa wavaa majoho akapaza sauti akisema hakika kiti changu kimetetemeka! Nao wanamji wakalia kwa sauti kuu wakisema "tumekuchoka"!je haitupasi kulihama jiji hili?
 
Reactions: Cyb
Je Wewe huna uwezo wa kuwa na mwanao mwenyewe??? Hadi ulee wawafilisti hawa???
Ndipo malaika akamtokea katika ndoto nakusema rudi ukanyenyekee chini ya mkono wa huyu kiranja mkuu,je hujui kama yeye anayo mamlaka ya kukuhamisha katika hilo jiji?maana tazama bwana amempa yeye kulimiliki
 
Ndipo Yule mtoza ushuru maarufu aishie nchi ya ng'ambo akawaandikia barua wanamji wote akipaaza sauti yake akasema....
 
Ndipo Yule mtoza ushuru maarufu aishie nchi ya ng'ambo akawaandikia barua wanamji wote akipaaza sauti yake akasema....
Ninyi hamjui kuwa yapasa mtu mmoja afe kwa ajili ya wengine,ili taifa zima lisiangamie? Basi wakuu wa mafarisayo wakatafuta kumkamata lakini herode mkuu akasema "wewe chapa kazi,mimi nimekuona unafaa hata kama hujui kusoma" .na makutano yote yakainama chini.
 
Ndipo akatokea Yule kaisari Mkuu wa watoza ushuru akasimama mbele ya baraza na kupaaza sauti kwa nguvu akasema "kuna dinari 1.5 zimeliwa na wevi na wanyanganyi" Ndipo akatokea mmojawapo wa wafuasi wa Yule msamaria jina lake tozibweka na kusema arudisheeee!!!!!
 
Ndipo Kaisari akasema niliyotumia nimetumia.
 
Ndipo Kaisari akasema niliyotumia nimetumia.
Mara Kabla ya ile siku kuu kubwa ya kuchanganya ardhi na maji kuwadia walionekana wanapunda jamii ya bombadeer wakiranda randa angani Karibia na hekalu la Yule kaisari Mkuu kushinda wote katika hema lile
 
Nalo jeshi la pilato likatoa tamko kuhusu kukusanyika bila kibali mjini mwa Daudi karibu na bahari ya galilaya....wakasema hii ni nchi niliyompa mwanangu mpendwa wangu iwe urithi wake,mbona mnapanga ghasia na kutafakari ubatili juu yake?
 
Hata ilipotimu siku ya pili, askari katika mji jirani na bahari ya Galilaya wali ruka na kutwanywa "Amini amin nawaambia msipowa tengua magoti wana hawa na kuwararua mitumba wavaayo pamoha na kuwarushia maji yaliotiwa chachu hakika hapana thumni itakayo piga kelele mifukoni mwenu" Nao baada ya amri ile kutoka chini ya mlima oduzungwa waliitika "Sisi ni nani ata tusitii sheria yako"? Wakazagaa mitaani huku wakipaza sauti na virungu mkononi "wapigwee wapigwee" pasipo kujua kua mvua i juu yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…