Baija Bolobi
JF-Expert Member
- Feb 25, 2009
- 1,093
- 1,733
Nimekosa usingizi nikaamua nianzishe thread hii.
Tujiulize, hivi Spika Ndugai anaposema Tundu Lissu hawezi kuhudumiwa na bunge katika matibabu yake kwa sababu alikiuka taratibu za kwenda kutibiwa nje, ana msingi gani katika hoja yake, ikiwa:
- Baada ya Tundu Lissu kupigwa risasi na kufikishwa hospitali hadi kwenda Nairobi, alikuwa hajitambui wala kufanya maamuzi yoyote kuhusu maisha yake!!
- Je, anaadhibiwa kwa kupoteza fahamu?
- Ikiwa ni CHADEMA au familia yake walifanya maamuzi haya, kwani yanamhusu nini Lissu na haki zake ikiwa Chadema na Familia siyo wabunge? Kwa nini serikali isiwachukulie hatua Chadema na familia kwa kumtorosha mbunge wake bila ridhaa ya bunge/serikali?
- Nakumbuka kusoma salaam za pole kutoka kwa Mheshimiwa Rais kwenda kwa Lissu na familia baada ya tukio; je kwa salaam hizo si Rais alitaka Lissu apone? Angeponaje bila kwenda hospitali?
- Nakumbuka mmoja wa madaktari waliomtibu Lissu Dodoma ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya. Kama Lissu angepelekwa DSM kama Ndugai anavyodai, si Katibu Mkuu huyu huyu ndiye angetoa kibali cha Lissu kwenda nje?
- Hivi hospitali ya Muhimbili ni majengo au ni wataalam ambao sasa ndo hawa waliomtibu Lissu huko Dodoma na bahati nzuri sasa Dodoma ndiyo DSM ya taifa?
- Kwanini serikali inaonekana kujibambikizia kesi hii mbaya mbele ya umma? Kumnyima matibabu, kukataa uchunguzi wa ndani na wa nje, kung'oa CCTV camera, kuzuia watu wasimuombee, kuzuia watu wasivae t-shirt za Lissu, kumtukana hata kama ni mgonjwa, n.k. Mbona hizi ni dalili za serikali yetu kujibambikizia kesi? Nilidhani mwenye jinai mjanja huwa anakuwa wa kwazna kufika kilioni.
- Kwanini serikali inalikuza mno suala hili? Kwa nini haijifunzi kutokana na historia, kwamba, mambo yaliyofumbiwa macho na serikali iliyopita, serikali hii imeyafukua na kuyachukulia hatua? Nani ataizuia serikali ijayo kuyafukua haya?