Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Mkuu Baija, nchi inaongozwa kama familia, hata wewe ukiwa nyumbani, kama mtoto wa kiume unaejitambua, siku mama yenu amesafiri kwenda kijijini kwao kusalimia, huku nyuma baba akaingiza mgeni, na ukamuona. Kumbe yule mgeni aliacha chumbani kwa baba nguo yeke fulani, bila baba kujua, ama kwa kusahau kwa bahati mbaya ama kwa makusudi ili mwenye nyumba ajue hayuko peke yake.Paskali, mwanzoni nilidhani na wewe huwajui "Wasiojulikana" na Wasiojulikana. Lakini nimeacha imani hiyo. Unawajua wote wa aina mbili na ndo maana unakimbilia kukosoa thread yangu badala ya kujikita na maswali niliyouliza.
Mama aliporudi, kukaibuka ugomvi mkubwa kati ya baba na mama kuhusu hiyo nguo imetoka wapi na imeachwa na nani?.
Baba kamwambia mama hamjui mwenye nguo hiyo wala hajui imeingiaje,labda watoto au msichana wa kazi alijichanganya.
Kwa vile wewe uliona picha nzima, jee utamweleza mama ukweli wa ulichoona?.
Hiyo ndio essence ya wasiojulikana hawa
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums
Kama baba amesema hajui nguo imefikaje, who are you kusema imefikaje?.
Kama yule aliyemshikia Nape bastola naye hajulikani mpaka leo anatafutwa na polisi, what are the chances kuwabaini julikana wa Lissu?.
Wana familia bora, wanamwamini baba mwenye nyumba, hata kama wewe ulimuona mgeni wa baba, lakini hukumshuhudia wakati akiivua hiyo nguo na kuiacha uvunguni mwa kitanda chumbani kwa baba, hivyo kama baba kasema hajui, then it migh be true, baba hajui, na hiyo nguo iliachwa siku nyingi nyuma na mgeni mwingine ambaye hata wewe hukumuona.
P
Hivyo nilitoa angalizo hili
Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums
Kwenye hili la kuwabaini wasiojulikana wa Tundu Lissu, serikali yetu imeshindwa, nilisema humu, kwa vile tupo watu wenye uwezo kuisaidia serikali yetu iweze kuwabaini, nikauliza jee tujitolee tuu kuwabaini na kuwataja, kuisaidia serikali yetu au tuisubiri, serikali iseme imeshindwa ndipo isaidiwe?.
WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums
P .