CCM nayo yadai imeshinda, wawakilishi wa vyama wako ndani ya ofisi za Halmashauri yanapofanyiwa majumuisho. Ni ukweli usiopingika kutangaza matokeo based on data za chama ni hatari, japo kurelease mapema, kunaziba mianya yoyote ya kuyafanyia madudu matokeo halisi.
Hali ni tete mjini Biharamulo, watu kwa makundi wametanda jirani na ofisi ya msimamizi na wanaonyesha hawako tayari kusikia lolote kinyume cha matumaini waliyokuwa nayo. Matokeo rasmi yakitangazwa CCM imeshinda, nadhani kuanzia hapo kwa msimamizi, patakuwa hapatoshi.FFU nao wamekaa mkao wa kula!.
Inapoelekea Saa 4:30 bila matokeo, Muda wangu BiMulo ndio umeniishia. Natamani kukaa mpaka mwisho, ila kesho ni 77 niking'ang'ana na Bi'Mulo, nitakula polisi. Ziko mtu 7 za JF Bi'Mulo, natumaini update zitaendelea, Mimi naitafuta Busisi.