Ingawa matokeo rasmi hayajatangazwa, CHADEMA wameweza kuwashinda kwa karibu kabisa CCM kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Biharamulo hii leo.
Mpaka zinapatikana hesabu za mwishomwisho kukiwa bado kituo kimoja cha Nyabugombe B chenye wapiga kura 394 CHADEMA ilikuwa ikiongoza kwa 50.6% huku CCM ikiifuatia kwa karibu ikiwa na asilimia 48.8% ya kura zote na TLP ikiwa imejinyakulia 0.55% ya kura zote.
Matokeo yanatarajiwa kutangazwa rasmi punde
Lakini matokeo ambayo yamejumlishwa mpaka dakika hii ni haya:
CHADEMA: 17,313
CCM: 16,682
TLP: 187
Turnout ilikuwa 39.24% (incredible!)
========================================
UPDATE 1...
Matokeo ya kituo kwa kituo tuliyoyapata toka kwa mwakilishi wa JF jimboni humo yameambatanishwa hapa chini kama attachment:
========================================
UPDATE 2.
Tume ya uchaguzi imesema hivi:
CCM: 17,561 = 51%
CHADEMA: 16,670 = 48.4%
CHADEMA wameyakataa matokeo kwani wanadai matokeo ya kata 3 yamegeuzwa tofauti na walivyosaini wasimamizi wa matokeo na yalivyohesabika vituoni!