Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Kwa sababu CCM wameshindwa na CHADEMA.

Kwa mtindo huu wa CCM wajue wanakaribisha mapigano na vita kwenye nchi yetu. Kwa nini wasikubali kushindwa tu? Huu udikiteta una mwisho, na mwisho hauko mbali kutoka sasa!!!

Tiba
 
Ingawa matokeo rasmi hayajatangazwa, CHADEMA wameweza kuwashinda kwa karibu kabisa CCM kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Biharamulo hii leo.

Mpaka zinapatikana hesabu za mwishomwisho kukiwa bado kituo kimoja cha Nyabugombe B chenye wapiga kura 394 CHADEMA ilikuwa ikiongoza kwa 50.6% huku CCM ikiifuatia kwa karibu ikiwa na asilimia 48.8% ya kura zote na TLP ikiwa imejinyakulia 0.55% ya kura zote.

Matokeo yanatarajiwa kutangazwa rasmi punde

Lakini matokeo ambayo yamejumlishwa mpaka dakika hii ni haya:

CHADEMA: 17,313

CCM: 16,682

TLP: 187

Turnout ilikuwa 39.24%
(incredible!)

========================================
UPDATE 1...

Matokeo ya kituo kwa kituo tuliyoyapata toka kwa mwakilishi wa JF jimboni humo yameambatanishwa hapa chini kama attachment:

i511_matokeobiharamulomagharibi.jpg

========================================

UPDATE 2.

Tume ya uchaguzi imesema hivi:

CCM: 17,561 = 51%

CHADEMA: 16,670 = 48.4%

CHADEMA wameyakataa matokeo kwani wanadai matokeo ya kata 3 yamegeuzwa tofauti na walivyosaini wasimamizi wa matokeo na yalivyohesabika vituoni!

nilihisi kitu kama hichi kutokea ndio maana sikutoa comment yoyote.
 
Jamani hii demokrasia ya vyama vingi kwenye nchi hii ni kama kiini macho.Tuache wananchi wachague wanayemtaka,tuheshimu utashi wao na chaguo lao.

Sasa hili suala la kutaka kila mahali/jimbo mshinde bila kujali matakwa ya wananchi husika ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaopaswa kulaaniwa kwa nguvu zote.

Tuacheni wananchi wetu wachague wanaowataka ili tujipime kama chama (CCM) tunao ufuasi kiasi gani na tuone namna ya kujirekebisha na kujipanga upya kwaajili ya chaguzi zijazo.
 
wana JF mnaongopewa na akina Pasco na genge lake, ukweli CCM imeshinda tena kwa margin kubwa tu.

Hakuna ubaya kupeana false hope na hongera za kujifurahisha lakini ukweli utabaki Biharamulo CCM ndio mshindi period!

Niliwaambia katika postings za awali watakachofanya Chadema ni kugomea kusaini fomu za matokeo, hicho ndicho kinachofanyika sasa hivi.
 
Last edited by a moderator:
Wana jf kwa taaifa za uhakika nilizopata ni kuwa tume ya uchaguzi imeitangaza ccm kuwa imeshinda bharamulo magharibi kwa kupata kura 17,561 sawa na 51% na chadema kura 16,670 sawa na 48.4%.

But taarifa zaidi zinasema kuwa chadema wamekataa matokeo kwa hoja kuwa matokeo ya kata tatu yamebadilishwa na kuipa ccm ushindi.

Naomba kuwasilisha
 
wana JF mnaongopewa na akina Pasco na genge lake, ukweli CCM imeshinda tena kwa margin kubwa tu.

Hakuna ubaya kupeana false hope na hongera za kujifurahisha lakini ukweli utabaki Biharamulo CCM ndio mshindi period!

Niliwaambia katika postings za awali watakachofanya Chadema ni kugomea kusaini fomu za matokeo, hicho ndicho kinachofanyika sasa hivi.
I dont buy your words.
 
leo ni mwisho wangu kujiusisha na siasa,nisije kufa bure kwa presha.
 
Tehe teh teh!

Haya sasa wenye wivu chukueni kamba zenu mjimalize!
 
Hii ya Biharamulo ni Kiboko, kwa vile nilikuwepo, nimeona kwa macho yangu na kusikia kwa masikio yangu na sasa japo sipo tena Biharamulo, bali kuamini kuna aina yoyote ya usanii unaoweza kufanyika.

Maadam mwenye mamlaka ya kutangaza matokeo ni Tume, lazima sote tukubali kuwa matokeo ya Tume ndio matokeo rasmi

Na mengine yote yalikuwa upotevu.

Kama Chadema wana hoja za Msingi, wajenge hoja, wala wasiende mahakamani kupinga, bali waijumuimuishe kwenye ilani yao ya uchaguzi 2010 na kuwaeleza wananchi mchezo mchafu unaofanywa na Tume ya Uchaguzi na CCM, wananchi wapenda haki, watawaelewa na kura za kumwaga watawapa.
 
Mara baada ya kupata habari hizi kwamba Chadema wameshinda jambo la kwanza ilikuwa ni kuuliza kama katika kampeni hizi Mzee Tingatinga alitinga huko .Kwa nilikuwa nimepata ajali siweza kurudi tena Bukoba wenzangu wajulishaji wakasema ni kweli alikuwepo.Nikajiuliza hii maana yake nini kwamba wana Biharamulo wamekataa kata kata na kuamua kulinda kura zao ? Nimeona nisiumie kichwa bali nije hapa na kuuliza wajuvu nyie .Je huu ndiyo mwisho wa Malecela ama aliteleza tu huko bado ana nguvu za kuweka namna ya kuiba kura ?
Mkuu Mh. Malecela alilazimika kwenda huko kupatch difference za wanachama wa CCM zilizosababishwa na Makamba kwa kumzodoa Mwenyekiti wa Biharamulo Anatory Choya mbele ya kikao cha Halmashauri ya NEC wilaya.Aliropoka kwa kumwabia kuwa aridhike na matokeo ya uchaguzi wa awali kwa vile yeye angepitishwa angesababishia chama mzigo usiobebeka kwa vile ana tuhuma za rushwa PCCB.Baada ya kauli hiyo wafuasi wa Choya, waliona Mtu wao amedhalilishwa.Hisia zao ziliwatuma kuwa Deodarus Kamala anawapandikizia mtu wake kwa sababu anazojua yeye,hivyo wakaapa kumuangusha.Na hiyo namba iliyojitokeza kuwa ndogo imesababishwa na daftari la Tume kuwa na hitilafu za wapiga kura kukosa majina yao wakati wana shahada.
Kutokana na hilo ndiyo maana Makamba anamsumbua msimamizi ahesabu upya anajua kuna akina Dr Mwakyembe watamwashia moto wa kutaka ajiuzulu.Turejee uchaguzi wa Tarime, ni Makamba huyuhuyu alitamka maneno mbele ya hadhara kwa kumwita Chambiri kuwa alikuwa si chaguo zuri kwa wanatarime.Ni tamko hili lililosababisha kambi ya Chambiri kumpigia Charles Mwela wa CHADEMA.Na hiyo ilitokana na Gachuma ambaye ni hasimu wa kisiasa wa Chambiri kushikamana na Makamba.
 
leo ni mwisho wangu kujiusisha na siasa,nisije kufa bure kwa presha.
 
Tunashukuru sana kwa kazi nzuri sana lakini Tume ya uchaguzi ni Kichaka cha ujambazi Tanzania na Wizi mtupu katika taifa letu
 
Una khiari na kakulazimisha? wewe baki na Chadema yashinda Biharamulo sawa?
Kusema kwamba kina pasco na genge walikuwa wanatoa habari za uongo si kweli walifanya vile wanaweza na vile waliona sote tunajua CCM ni baba ya magic fisadi, tunajua ushindi wa CCM ni mapenzi ya tume hakuna asiyejua hilo kura hazimfanyi mgombea wa CCM kushinda bali karatasi za tume ya CCM ndizo zinazopanga mshindi, nitatetea demokrasia kwa kadri ya uwezo wangu.
 
Binafsi sikufikiri ingekuwa rahisi kuishinda CCM hasa wakati huu ambapo matokeo ya chaguzi ndogo yanaushawishi sana katika kuamua hatma ya uchaguzi wa mwakani. Nilijua kuwa CCM kingeshinda hata kwa kumfukuza mwenyekiti wa NEC. Nadhani wanaoshabikia mageuzi ya kisiasa katika nchi hii wana wakati mgumu sana wa kuzishawishi hisia zao kuwa mabadiliko yanahitaji uvumilivu wa juu hasa katika hali kama ya Tanzania ambapo kuna kundi dogo la watu wanaofaidi raslimali za nchi. Si rahisi kama ambavyo haijawa rahisi kuleta mabadiliko. Historia inasema mabadiliko wakati mwingine yamegharimu maisha ya watu. Faraja kwa wataka mabadiliko wote ni kuwa mwisho wa siku haki HUSHINDA kama ambavyo tunashuhudia vyama kama CHADEMA kikikipa shida chama tawala. Si muda mwafaka kukata tamaa maana mabadiliko yaja
 
It is so really nust man, and it is so crazy with all this happened there. Siwezi kusema but kuna haja ya kutaka TUME HURU YA UCHAGUZI TANZANIA!! Hawa jamaa ni wezi na tena wanafaa watake sasa hivi. hivi ilivyo huko kila mtu ni shaidi mzuri kama wao ndio wananyima haki ya watu wa Taifa hili ni DHAMBI KUBWA SANA
 
Back
Top Bottom