Kwa sababu CCM wameshindwa na CHADEMA.
Ingawa matokeo rasmi hayajatangazwa, CHADEMA wameweza kuwashinda kwa karibu kabisa CCM kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Biharamulo hii leo.
Mpaka zinapatikana hesabu za mwishomwisho kukiwa bado kituo kimoja cha Nyabugombe B chenye wapiga kura 394 CHADEMA ilikuwa ikiongoza kwa 50.6% huku CCM ikiifuatia kwa karibu ikiwa na asilimia 48.8% ya kura zote na TLP ikiwa imejinyakulia 0.55% ya kura zote.
Matokeo yanatarajiwa kutangazwa rasmi punde
Lakini matokeo ambayo yamejumlishwa mpaka dakika hii ni haya:
CHADEMA: 17,313
CCM: 16,682
TLP: 187
Turnout ilikuwa 39.24% (incredible!)
========================================
UPDATE 1...
Matokeo ya kituo kwa kituo tuliyoyapata toka kwa mwakilishi wa JF jimboni humo yameambatanishwa hapa chini kama attachment:
========================================
UPDATE 2.
Tume ya uchaguzi imesema hivi:
CCM: 17,561 = 51%
CHADEMA: 16,670 = 48.4%
CHADEMA wameyakataa matokeo kwani wanadai matokeo ya kata 3 yamegeuzwa tofauti na walivyosaini wasimamizi wa matokeo na yalivyohesabika vituoni!
Choka mbayanilihisi kitu kama hichi kutokea ndio maana sikutoa comment yoyote.
Yep... Kamati ya ufundi imefanya kazi yake! Kwishnei....Choka mbaya
I dont buy your words.wana JF mnaongopewa na akina Pasco na genge lake, ukweli CCM imeshinda tena kwa margin kubwa tu.
Hakuna ubaya kupeana false hope na hongera za kujifurahisha lakini ukweli utabaki Biharamulo CCM ndio mshindi period!
Niliwaambia katika postings za awali watakachofanya Chadema ni kugomea kusaini fomu za matokeo, hicho ndicho kinachofanyika sasa hivi.
I dont buy your words.
Mkuu Mh. Malecela alilazimika kwenda huko kupatch difference za wanachama wa CCM zilizosababishwa na Makamba kwa kumzodoa Mwenyekiti wa Biharamulo Anatory Choya mbele ya kikao cha Halmashauri ya NEC wilaya.Aliropoka kwa kumwabia kuwa aridhike na matokeo ya uchaguzi wa awali kwa vile yeye angepitishwa angesababishia chama mzigo usiobebeka kwa vile ana tuhuma za rushwa PCCB.Baada ya kauli hiyo wafuasi wa Choya, waliona Mtu wao amedhalilishwa.Hisia zao ziliwatuma kuwa Deodarus Kamala anawapandikizia mtu wake kwa sababu anazojua yeye,hivyo wakaapa kumuangusha.Na hiyo namba iliyojitokeza kuwa ndogo imesababishwa na daftari la Tume kuwa na hitilafu za wapiga kura kukosa majina yao wakati wana shahada.Mara baada ya kupata habari hizi kwamba Chadema wameshinda jambo la kwanza ilikuwa ni kuuliza kama katika kampeni hizi Mzee Tingatinga alitinga huko .Kwa nilikuwa nimepata ajali siweza kurudi tena Bukoba wenzangu wajulishaji wakasema ni kweli alikuwepo.Nikajiuliza hii maana yake nini kwamba wana Biharamulo wamekataa kata kata na kuamua kulinda kura zao ? Nimeona nisiumie kichwa bali nije hapa na kuuliza wajuvu nyie .Je huu ndiyo mwisho wa Malecela ama aliteleza tu huko bado ana nguvu za kuweka namna ya kuiba kura ?
Kusema kwamba kina pasco na genge walikuwa wanatoa habari za uongo si kweli walifanya vile wanaweza na vile waliona sote tunajua CCM ni baba ya magic fisadi, tunajua ushindi wa CCM ni mapenzi ya tume hakuna asiyejua hilo kura hazimfanyi mgombea wa CCM kushinda bali karatasi za tume ya CCM ndizo zinazopanga mshindi, nitatetea demokrasia kwa kadri ya uwezo wangu.Una khiari na kakulazimisha? wewe baki na Chadema yashinda Biharamulo sawa?
leo ni mwisho wangu kujiusisha na siasa,nisije kufa bure kwa presha.
It is so really nust man, and it is so crazy with all this happened there. Siwezi kusema but kuna haja ya kutaka TUME HURU YA UCHAGUZI TANZANIA!! Hawa jamaa ni wezi na tena wanafaa watake sasa hivi. hivi ilivyo huko kila mtu ni shaidi mzuri kama wao ndio wananyima haki ya watu wa Taifa hili ni DHAMBI KUBWA SANABinafsi sikufikiri ingekuwa rahisi kuishinda CCM hasa wakati huu ambapo matokeo ya chaguzi ndogo yanaushawishi sana katika kuamua hatma ya uchaguzi wa mwakani. Nilijua kuwa CCM kingeshinda hata kwa kumfukuza mwenyekiti wa NEC. Nadhani wanaoshabikia mageuzi ya kisiasa katika nchi hii wana wakati mgumu sana wa kuzishawishi hisia zao kuwa mabadiliko yanahitaji uvumilivu wa juu hasa katika hali kama ya Tanzania ambapo kuna kundi dogo la watu wanaofaidi raslimali za nchi. Si rahisi kama ambavyo haijawa rahisi kuleta mabadiliko. Historia inasema mabadiliko wakati mwingine yamegharimu maisha ya watu. Faraja kwa wataka mabadiliko wote ni kuwa mwisho wa siku haki HUSHINDA kama ambavyo tunashuhudia vyama kama CHADEMA kikikipa shida chama tawala. Si muda mwafaka kukata tamaa maana mabadiliko yaja
Kila la kheri