Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Matokeo yamerudiwa kuhesabiwa mara nne, hii yote ni ili kuhakikisa CCM inashinda.
Kwanini iwe ni kuhakikisha kwamba CCM inashinda, na sio kuhakikisha kwamba hakuna udanganyifu wowote uliotokea?
 
ccm kwakweli wizi wenu sasa umekuwa wa waziwazi na tumechoshwa..maana huko ni kutuchagulia watu..wezi sana ccm nyie
 
Kwanini iwe ni kuhakikisha kwamba CCM inashinda, na sio kuhakikisha kwamba hakuna udanganyifu wowote uliotokea?

Sasa ni udanganyifu uliofanywa na nani. Kama kura zilihesabiwa tangu jana na matokeo ya awali yalipatikana, swala la kuhesabu hesabu lilikuwa ni la nini. Narudia tena kusema "Itachukua muda mrefu sana kupatikana demokrasia ya kweli Tanzania".
 
Nilishasema mambo ya Tume ya Uchaguzi!! TUME YA CCM. WAKURUGENZI WA CCM, WOTE NI MALI ZAO. HAKUNA HAJA YA UCHAGUZI HATA KIDOGO. Wawe wanasema mapema kama kuna haja ya uchaguzi


bila tume ya uchaguzi huru upinzani utashinda wakiamua CCm. tunahitaji dikteta mzalendo kama Gadaf, Castro hata Idd Amin kabla nyerere hajamwita dada
 
UPDATE 2.

Tume ya uchaguzi imesema hivi:

CCM: 17,561 = 51%

CHADEMA: 16,670 = 48.4%

CHADEMA wameyakataa matokeo kwani wanadai matokeo ya kata 3 yamegeuzwa tofauti na walivyosaini wasimamizi wa matokeo na yalivyohesabika vituoni!

========================================

Update 3.

Tume ya Uchaguzi imemtangaza mgombea wa CCM kama mshindi kwa kura zinazoonyeshwa kwenye Update ya awali ingawa CHADEMA wameyakataa matokeo ya vituo 9 kati ya vituo 237 vya uchaguzi!
Mkuu tupe update ya kituo kwa kituo ili tujue mabadiliko yako vituo vipi?
 
TUmechoka na matokeo na tume ya uchaguzi!! Hatutaki mambo ya ajabu kama haya ya mazigaombwe kama hivi


Usijali sana, PM Pinda anajaribu utawala wa kijeshi mkoani Mara hasa Tarime na Rorya ukifanikiwa tutaufanya wa nchi nzima so no more chaguzi kubwa na ndogo.
 
Hakuna jipya hapo mzee wangu!! wezi watupu na tume ni kichaka chao cha wizi wa kura
 
Siku CCM inashindwa kwenye uchaguzi wa rais itabidi tufanye iwe public holiday. Iwe siku ya kumbukumbu, maana Tanzania itakuwa imemshinda adui wake mkuu na mnyonyaji wake numba moja!
 
Usijali sana, PM Pinda anajaribu utawala wa kijeshi mkoani Mara hasa Tarime na Rorya ukifanikiwa tutaufanya wa nchi nzima so no more chaguzi kubwa na ndogo.
Tunahitaji jeshi tu sasa hivi maana hali jinsi ilivyo kuna ufisadi kila sehemu maana kuna mambo ya ajabu sana katika chaguzi zetu. Hakuna haja ya kuwa na chaguzi ndogo kama hizi za huko Kagera
 
ccm kwakweli wizi wenu sasa umekuwa wa waziwazi na tumechoshwa..maana huko ni kutuchagulia watu..wezi sana ccm nyie

CCM wala si wizi ila kuna watu watanzania wachache wasioitakia mema tanzania kama tanzania na wananchi wake!hao watu tusiwalalumu ila tujilaumu sisi wenyewe kwa kuwawekea mazingira ya kutudanganya!
sasa inabidi tuamke maana Tanzania ni ya kwetu wote na si ya kikwete peke yake!hebu tujiulize ni wapi tulipoangukia ili tuweze kuinuka na kung'uta mavumbi kisha kusonga mbele!
kama kuna tick tack imepigwa kwenye haya matokeo kwa kweli watanzania tunaibiwa haki yetu
 
Hebu nitoeni ushamba.... Ina maana hayo makaratasi yaliotoka vituoni hayakuwa na sahihi za watu wa CHADEMA? Je CHADEMA hawana specimen za signature zao?
 
Siku CCM inashindwa kwenye uchaguzi wa rais itabidi tufanye iwe public holiday. Iwe siku ya kumbukumbu, maana Tanzania itakuwa imemshinda adui wake mkuu na mnyonyaji wake numba moja!

bila tume huru ya uchaguzi ni ndoto za mchana labda jeshi lipindue serikali
 
Mmmmhhh! siasa za Tanzania kichwa cha Mwendawazimu. Kama CHADEMA wameshinda si waachieni jimbo tu? Muda wenyewe uliobaki ni mwaka mmoja tu.

Kama hawakushinda basi hizi tabia za kuletewa habari hapa JF ambazo sio sahihi zinaweza kusababisha madhara makubwa.

Sasa ile hongera yangu kwa CHADEMA nitaiondoa vipi?

Hongera CCM kama mtu mmeshinda kihalali.

Invisible na Pasco, nasifu mchango wenu kwenye hizi chaguzi. Ila tu in future kuweni makini kwa ku report news na sio kutengeneza news.
 
Chadema wamefanya kitu walichofanywa wapinzani wa IRAN hii si habari nzuri kwa democrasia
 
Invicible, funga hii thread, anzisha ya ushindi wa CCM inayojitegemea ili JF iplay impartiality, kuendelea kuwepo kunajustify kama tunasymphasize na Chadema.
Wana JF, kutangaza mwelekeo wa kituo kwa kituo ni kitu cha kawaida. Hakuna haja ya kuibeza JF kwa hilo, na sasa tuipongeze CCM huku tukitafakari ni nini haswa kilichotokea.
 
Chadema wajifunze kwa CUF zanzibar nafikiri CCM 2010 itaua watu wengi sana
 
Mhhhhhhhhhh! CCM hatari. Jamani haki iko wapi? Huu ugonjwa wa kukosa haki ya kweli utaendelea kututafuna na kuliweka taifa letu kwenye laana. Unaweza kuona jinsi matokeo yalivyocheleweshwa kutangazwa yote hii ilikuwa ni janja ya kuitafutia CCM ushindi.
Tusipoacha hii dhambi tusitarajie baraka kutoka kwa MUNGU.

Haki huinua taifa bali dhambi ni aibu ya watu wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…