Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

achana na huyo kaona misalaba kwenye avatar yako kimemkera.....
anyway
hivi mmegundua hata wana CCM wenyewe hawaipendi CCM?am sure masatu kafurahia ushindi wa CHADEMA
Kijana unaonekana unapenda kushabikia pumba... sasa msalaba wake mimi unanihusu nini?
 
Tunafurahia matokeo kwa kuwa amepatikana mbunge mzuri, au kwa sababu tu CCM imeshindwa? Sina hakika na track record ya wagombea. I hope aliechaguliwa alichaguliwa kutokana na record yake na si tu kwa kuwa ni mtu wa Chadema
 
Msishangae kesho na kesho kutwa mka mkuta barabarani kagongwa na gari tu.
 
Bongolander,
Mkuu, lini ulitazama mbunge wa CCM kama anafaa kushinda unaposhangilia?.. ushauri huu ungekuwa mzuri sana siku CCM wanashinda maanake wachovu wote tunawajua, na akitoke mbora kati yao tutashukuru hata kushindwa kwa Upinzani.
 
Tunafurahia matokeo kwa kuwa amepatikana mbunge mzuri, au kwa sababu tu CCM imeshindwa? Sina hakika na track record ya wagombea. I hope aliechaguliwa alichaguliwa kutokana na record yake na si tu kwa kuwa ni mtu wa Chadema

Hamna shida nae akifanya vibaya anaondolewa. Tunacho shangilia ni kuweza kupokezana madaraka na siyo chama kimoja kung'ang'ania ushindi by any means possible. Hatushangilii Chadema wala CCM tuna shangilia DEMOKRASIA.
 
Aisi kwa safu hiyo ni vigumu kunihamasisha ,maana nikama unanihamasisha ili ni isaliti akili.

Hii ni sawa na mimi , mfano wewe ni mjahidina nikuhamasishe ule kama nyama ka nguruwe maana kanguruwe kenyewe kalikuwa kadogoooo tuuuu ,hivyo unajisi wake ni tofaute na lile libabayao la nguruwe.teh teh teh
Malafyale na MkamaP,
angalia red! Hivi ndivyo alivyonijibu muungwana MkamaP nami nikamjibu hivyo mkuki kwa nguruwe ...kama inakuwa boa pole sana
 
InakuwajeTumaini anatumia lugha za dharau kwa mwana JF mwenzake?Please moderator nipe mwongozo kwa kauli kama hizi zikiingizwa hapa JF, huwa unachukuliwa uamuzi gani?Anatakiwa ama afute kauli yake au akae chini?

Kumbukeni JF haina dini,anayekula paka ni juu yake na kizazi chake,anayekula bundi ni uamuzi wake,na anayesali hata kwenye mapango ni haki yake.Hamna mpumbavu kwenye jamii iliyostaharabika kama hii,na KAULI hii imenishtua!

Nawasilisha hoja na JF mnilinde!
Akianzisha hatutamwacha muungwana hujibiwa kiungwana and vice versa kila moja ajifunze kumhesimu mwenzake...
 
Hamna shida nae akifanya vibaya anaondolewa. Tunacho shangilia ni kuweza kupokezana madaraka na siyo chama kimoja kung'ang'ania ushindi by any means possible. Hatushangilii Chadema wala CCM tuna shangilia DEMOKRASIA.
Nakuunga mkono 100% itasaidia hasa wananchi kufahamu vyama vingine kwakuwa chaguzi ndogo zinatangazwa sana hivyo kushinda kwa chadema kutaifanya vyama vingine kujulikana siyo ccm tuu miaka nenda rudi..na wananchi wataona kumbe waweza kuchagua chama kingine it is a good result for Tanzanian democracy
 
Mkuu
haina haja yoyote yakumushutumu kwa lugha mbaya ,sisi tumefundishwa kuwapenda adui kama tunavyojipenda,hivyo kusema achukuliwe hatua kwa kauli mbaya ni kutomtendea haki mhusika maana wenda mafunzo yake tangu utoto ni kama ya kwetu ama yapo kinyume chake kitu kinachompa haki na uhalali wa kutamka maneno ya mfano huo.
Ungekuwa muungwana usingeandika uliyoandika hapo juu..mjahidina inaingiaje kwenye thread hii? Wewe huna lugha nzuri usitegemee lugha nzuri kutoka kwangu....uungwana -uungwana.. ujinga hujibwa kwa ujinga...ndiyo lugha anayoelewa ukibadili lugha yako nami nabadili lakini hutanikuta nikianza kukusema wewe vibaya wala kukejeli imani(dini )yako kama ulivyfanya wewe? Imani yangu ni zaidi ya siasa/na JF be informed! just want to make it clear.
 
Hamna shida nae akifanya vibaya anaondolewa. Tunacho shangilia ni kuweza kupokezana madaraka na siyo chama kimoja kung'ang'ania ushindi by any means possible. Hatushangilii Chadema wala CCM tuna shangilia DEMOKRASIA.

Yes Indeed. Tunatakiwa kujua kuwa demokrasia ni yetu watanzania. sio ya Mbowe, Lipumba wala Kikwete. Tukiwa na mwelekeo kama huu hakika tutafika tunakotaka kwenda.
 
CHADEMA isishiriki Biharamulo!Kwanza haina sababu ya kufanya hivyo. Pili, inachosha kusikia wimbo wao wa malalamishi kuhusu CCM, dola n.k lakini kubwa ni kupoteza mtaji wao wa kisiasa. Wamuunge mkono mgombea wa chama kingine wao fedha na raslimali ambayo wangeitumia huko kwanza warudi Busanda, Kiteto, Mbeya Vijijini, Tunduru n.k na majimbo mengine kama 70 tu na huko wajijenge kwa ajili ya 2010.

a. Kuandikisha wanachama wapya (kupata kura 22,000 si mchezo kwani kuna wanachama wangapi?)
b. Kufungua matawi mapya
c. Kutengeneza mtandao wa mafunzo kwa makada wake
d. Kutengeneza ajenda za mahali (hili nitalichambua baadaye)
e. Kubadilisha Katiba yake ili kilenge kushinda uchaguzi na kuunda serikali.
f. kulenga majimbo ya mjini ambako imekuwa ikikubalika kwa kufanya hayo ya a, b na c
g. Kubadili mkakati wa mahubiri yake, kuhubiri ufisadi hakuleti ushindi bali kuhubiri ujumbe wa matumaini dhidi ya ufisadi kutaleta. Wao watafanya nini. Hapa hawana budi kuradicalize their message. "tutawatafuta wale wote waliohusika na wizi wa fedha umma, tutawawajibisha, na walioficha fedha nje tutahakikisha zinarudishwa ndani ya muda x).
h. Wahamishe makazi yao toka Dar na kuamia vijijini; Dar iwe pa kuja kuchaji tu.
i. x,y

Sidhani hata moja kati ya hayo hapo juu yamefanyika lakini.........
 
Niko Biharamulo na ninayo nakala ya Official Results za Chadema, data ni kama Invisible alivyoweka. Labda niongezee kidogo. Matokeo hayo ni ya jimbo zima isipokuwa kituo kimoja cha Nyabugombe "A" katika kata ya Nyakahura ambacho kina idadi ya wapiga kura 394. Hivyo Chadema wanasema hata CCM wakishindwa kwa 100% hicho kituo bado hawatafikia kura zao kwani tofauti ya kura ni 631.

Hivi sasa ni saa tisa usiku wafuasi wa Chadema bado wako nje ya ofisi ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wakiimba na kusheherekea, wakisubiri matokeo. CCM nao walikuja wakaanza na kuimba na kushangilia lakini wakazidiwa nguvu na wakaondoka. Walioko ndani ya nyumba ni Basil Lema wa Chadema na Watumishi wa Tume. Timu za CCM na TLP hazijaonekana. Habari kutoka ndani ya ofisi ni kwamba gari lililokuwa limebeba masanduku ya kura kutoka kata ya Kalenge (mpakani na Kibondo) limeharibika na limekwama Nyakanazi hivyo hamna majumlisho yoyote yatakayoendelea usiku huu. Lakini kuna habari kutoka Nyakanazi zinazosema dereva wa gari hilo anasema amepewa order apaki gari hapo Nyakanazi mpaka atakapopewe maelezo zaidi.

Uongozi wote wa CCM uliondoka Biharamulo jana na kuelekea Chato. Waliobaki ni watendaji waliokuwa na majukumu siku ya uchaguzi. Habari kutoka Chato ni kwamba kambi ya CCM imepata matokeo ya kata sita na bado hawana uhakika wa matokeo ya kata mbili: Kalenge na Nyabusozi. Licha ya hayo wanadai wameshinda kwa kura 1,971.

Sijui kama hapo kwa mkurugenzi patatosha kesho. Tusubiri tuone.
Asante Nyumbu for being there, nimegundua kuangalia uchaguzi Biharamulo na kulala Chato was a mistake!.
Returning officer alisema kuwa majumuisho yanaanza saa moja kamili asubuhi hii, naomba uwe pale utuupdate.
Kuna wanaJF 6 Biharamulo, naombeni mtuupdate ili uthibitisha rasmi upatikane. Hii ya kutegemea Matokeo ya Chadema pekee na sio Tume, bado haijatulia, haswa kama na CCM wamejitangazia ushindi.
Kama matokeo ya Tume yatakuwa tofauti na ya Chadema,
Mnawaweka wana Bi'Mulo kwenye position gani?.
 
The title has been changed to reflect the unofficial results that have been received so far. Until the official pronouncement by the Returning Officer so far the winner of the election has not been announced. We are waiting for the official results this morning.

For Admins.
 
Thank you for your smart English sentences. However, we are sorry for you as you seem to be either CCM clerk or one of the UFISADI beneficiaries. The truth has serveiled and remain to a landslide victory for the true ANT-FISADISM party....CHADEMA.
 
Mzee Mwanakijiji kasema "Chadema kijijenge kiwe chama mbadala". Hilo sio lengo sahihi. Chadema kijijenge kiwe chama tawala.

Keil kasema "This is the end of Mrema". It could be the beginning of the end of TLP, but Mrema will probably live on for a few more years. He will join CCM if necessary.

Kasheshe kasema tuache kusema CCM inaiba kura. Kwa kisa gani? Wewe hukusikia ushahidi uliotolewa mahakamani kuonyesha wazi kwamba CCM iliwataka wasimamizi wa uchaguzi kubadilisha matokeo ya kura ili Dr. Slaa asishinde? CCM inaiba kura. Labda hawakuiba wakati huu, lakini uko ushahidi wa kutosha kwamba wale ni wezi wa kura za wananchi. Ni kawaida yao. Na Jaji Lewis Makame anafumbia macho huo wizi. Shame on him!

Hongereni Chadema. Bila shaka nyie ndio tegemeo la Watanzania wengi. Wasomi karibu wote wanawaungeni mkono. Na sasa raia wengine nao wametambua ubora wenu
 
Thank you for your smart English sentences. However, we are sorry for you as you seem to be either CCM clerk or one of the UFISADI beneficiaries. The truth has serveiled and remain to a landslide victory for the true ANT-FISADISM party....CHADEMA.

teh teh teh..aarrhhg..JF bana, can't have short of fun..lolz
 
Thank you for your smart English sentences. However, we are sorry for you as you seem to be either CCM clerk or one of the UFISADI beneficiaries. The truth has serveiled and remain to a landslide victory for the true ANT-FISADISM party....CHADEMA.

you just made my day mate!.. goodday!
 
Thank you for your smart English sentences. However, we are sorry for you as you seem to be either CCM clerk or one of the UFISADI beneficiaries. The truth has serveiled and remain to a landslide victory for the true ANT-FISADISM party....CHADEMA.

Duh! We had fascism, nazism, communism na sasa tuna fisadism. Kweli this ideology best fits our leaders.
 
Ingawa matokeo rasmi hayajatangazwa, CHADEMA wameweza kuwashinda kwa karibu kabisa CCM kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Biharamulo hii leo.

Mpaka zinapatikana hesabu za mwishomwisho kukiwa bado kituo kimoja cha Nyabugombe B chenye wapiga kura 394 CHADEMA ilikuwa ikiongoza kwa 50.6% huku CCM ikiifuatia kwa karibu ikiwa na asilimia 48.8% ya kura zote na TLP ikiwa imejinyakulia 0.55% ya kura zote.

Matokeo yanatarajiwa kutangazwa rasmi punde

Lakini matokeo ambayo yamejumlishwa mpaka dakika hii ni haya:

CHADEMA: 17,313

CCM: 16,682

TLP: 187

Turnout ilikuwa 39.24%
(incredible!)

Invisible, wewe una amini kuwa CCM watakosa hizo kura 631 ili kulingana na CHADEMA wakati turnout ni 39.24%. usishangae kusikia kuwa final turnout ni 45% na hiyo percentage yote iliyo ongezeka wakawa wameipigia kura CCM.
 
Back
Top Bottom