Ni kweli CCM ilishinda chaguzi ndogo za Kiteto, Busanda, na Mbeya Vijijini. Pamoja na huo ushindi kitu kilichokuwa wazi ni kwamba CHADEMA walionyesha ushindani wa kuitoa jasho CCM.
Tukumbuke kwamba CCM ilikuwa inasaidiwa na NEC, Polisi na kutumia resources za umma kwenye kampeni. Kuna mawaziri waliacha ofisi wakaenda kusaidia kupiga kampeni wakitumia magari ya serikali. Kuna cases nyingi za jinai zilikuwa reported na hakuna kilichofanyika mpaka leo. Mfano, Kiteto akina Mtalemwa na wenzake walipigwa sana lakini polisi hawakufanya kitu. Kule Busanda kuna viongozi wa serikali za mitaa walikamatwa wakinunua shahada, mpaka leo hakuna kitu. Kuna magari yalionekana yakipakua magodoro kule Busanda NEC na Polisi hawakufanya chochote.
Kwa tathimini yangu hilo gap dogo la kura ni dalili nzuri kwa CHADEMA kwamba wakiweka wagombea wazuri na wakatumia vyema poor resources walizonazo, wanaweza kushinda viti vingi uchaguzi ujao wa 2010. Uchaguzi wa mwakani kutakuwa hakuna kusaidiana, kila mmoja anapambana kivyake jimboni kwake. Hao mawaziri kila mmoja atakuwa jimboni kwake akipiga kelele kivyake na Polisi hawatamwagwa wengi kwenye jimbo kama ilivyo sasa kwamba uchaguzi mdogo ukija Polisi wanamwagwa sehemu moja na hivyo kuongeza woga na sometimes hutumika kwa manufaa ya CCM.