Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Mafisadi kwisha kabisa.....!!!
Moto huu usizimwe mpaka 2010...CCM watakiona....HONGERENI BIHARAMULO KWA MAAMUZI SAHIHI....2PO PAMOJA....!!!!
 
Don't read too much into this. Local politics are not necessarily national politics. Kwa vile jimbo hilo tayari lilikuwa upinzani hivyo aliyeanguka zaidi si CCM bali TLP. Ndio maana ushindi wa Tarime pamoja na ukubwa wake wote ulitafsiri jambo moja tu nalo ni kurudisha jimbo mikononi mwa Chadema.

Hadi hivi sasa katika chaguzi hizi ndogo, Chadema haijaweza kushinda jimbo la CCM. Imeshindwa Tunduru, Kiteto, na Mbeya Vijijini. Na hii utaona tofauti kubwa ya jinsi gani CCM inapeleka nguvu zake. Huwezi kulinganisha jinsi CCM ilivyopania kuichukua Busanda na jinsi ilivyopandia kuichukua Biharamulo.

Jambo kubwa ambalo ni zoezi kwa chadema ni jinsi gani kuweza kushinda sasa kwenye majimbo ya CCM maana sasa hivi hakuna tena uchaguzi mdogo hadi uchaguzi mkuu mwakani.

Ninachokiona sasa ni CCM kuanza kujipanga kuyakomboa majimbo ya upinzani na kuyarudisha CCM.

Na suala la kuungana mimi nilishassema mapema, hakuna ulazima wa Chadema kuungana na chama kingine bali kujijenga ili kiweze kuwa chama mbadala na hili ni kweli kwa CUF vile vile. Endapo kutakuwa na ulazima wa kuungana basi ni muungano wenye kuunganisha fikra, sera, katiba, mitazamo n.k na siyo muungano wa kuiondoa CCM.

Lakini pamoja na CHADEMA kushindwa bado wameweza kuonyesha upinzani wenye heshima.... Ukianzia na Kiteto, Mbeya vijijini (goli la mkono) na Busanda kote huko CCM (chama kikongwe) ilibidi watumie nguvu za ziada.
 
rmashauri..
Kwenye dini ya kiislam unapoona muislam mwenzako anapambana na mgalatia ni mwiko kabisa kumtupa hata kama unajua ametenda makosa mabaya... hivyo usitegee Game theory amseme vibaya Ustaadhi Idrisa wa tanesco au Prof. Lipumba amseme vibaya sheikh Rostam Aziz...

Kwa hiyo hata wakifanya kosa hawasemwi. Wakifanya Wakristo hivyo si itaonekana udini? Kama ni hivyo ni hatari basi. Kwa mfano mimi hata Mkapa akikosea lazima nimseme japo wote ni Wakristo. Ina maana mkuu hata Muislamu akosee vipi waislamu wengine hawata usema ubaya wake wala makosa yake? Mh basi kazi. But I don't believe all muslims are like that.
 
Lakini pamoja na CHADEMA kushindwa bado wameweza kuonyesha upinzani wenye heshima.... Ukianzia na Kiteto, Mbeya vijijini (goli la mkono) na Busanda kote huko CCM (chama kikongwe) ilibidi watumie nguvu za ziada.

Je watagomea matokeo pamoja na uvunjaji wa sheria za uchaguzi au ni pale wanaposhindwa ndio matokeo yanagomewa?
 
Hongera CHADEMA.

Hivi wasio piga kura hawajui kuwa ni kutokupiga kura ni UJINGA? Kwa 2010 ili Vyam mbadala viwe na nafasi ni lazima hawa wahamasishwe kwa kweli.
Hapana... Si ujinga tu! Ni DHAMBI KUBWA...! Inabidi elimu itolewe kwa nguvu sana kabla ya 2010
 
Nimesubiri maoni ya Mwl. Kitila Mkumbo kwa muda mrefu bila mafanikio ingawa naona anachungulia hapa!!!

Naenda zangu kulala!!!

Hii staili ya Mwalimu kufurahia ni kali sana..
 
Kama kweli CUF ina nia njema na ukombozi wa watanzania waungane na chadema kiwe chama kimoja kwani CUF bado wanakampumzi Zanzabar na Chadema wanapuma kwa kasi Tanganyika itaweweka pazuri sana kupambana na CCM la sivyo Cuf itakufa taratibu kama NCCR na TLP.

Kinepi_nepi,
Mimi naona CHADEMA wajipange tu vizuri wenyewe. CUF wataenda kuwavuruga tu. Unajua wanaume wawili wenye miji yao na wana historia ya kutokuwa marafiki wa dhati hawawezi kuunganisha familia zao pakakaa salama. Tumeona jinsi walivyokuwa wanapondana hasa tangu uchaguzi wa kule Tarime, Mbeya Vijijini na hata Busanda.
 
Kitu kimoja tu nimejifunza.. Wanaposimama wapinzani wachache kuna uwezekano wa chama pinzani kuishinda CCM lakini wakiingia wengi, wapinzani hugawana kura na CCM huibuka mshindi..
 
Nakumbuka ndugu Mtanzania alisema Chadema wasimuweke mgombea wao kule Biharamulo, bali wamuunge mkono yule wa TLP.

Mh! Logic zingine bwana! Za wasomi wa fasttrack hizo.
 
Kitu kimoja tu nimejifunza.. Wanaposimama wapinzani wachache kuna uwezekano wa chama pinzani kuishinda CCM lakini wakiingia wengi, wapinzani hugawana kura na CCM huibuka mshindi..

Mkandara,
Lakini hii ya Biharamulo naona ilikuwa tofauti kidogo maana hata hao wapinzani wengine hawajapata kura kabisa kwahiyo issue ya kugawana kura hapa haikuwepo. Na kumbuka vyama vyote vyenye majina i.e TLP na CUF walisimamisha wagombea.

Sorry: CUF hawakusimamisha mgombea bali waliunga mkono TLP
 
Last edited:
Hongereni CHADEMA kwa ushindi.Kazeni buti, mwendo mdundo mpaka 2010.
 
Je watagomea matokeo pamoja na uvunjaji wa sheria za uchaguzi au ni pale wanaposhindwa ndio matokeo yanagomewa?

Kwa ujumla sheria za uchaguzi zinai-favour CCM... hivyo pamoja na CHADEMA kubahatika kushinda kwenye mazingira magumu inabidi wasibweteke ila waendelee kupigia kelele uwanja wa uchaguzi uwe tambarare...
 
Don't read too much into this. Local politics are not necessarily national politics. Kwa vile jimbo hilo tayari lilikuwa upinzani hivyo aliyeanguka zaidi si CCM bali TLP. Ndio maana ushindi wa Tarime pamoja na ukubwa wake wote ulitafsiri jambo moja tu nalo ni kurudisha jimbo mikononi mwa Chadema.

Hadi hivi sasa katika chaguzi hizi ndogo, Chadema haijaweza kushinda jimbo la CCM. Imeshindwa Tunduru, Kiteto, na Mbeya Vijijini. Na hii utaona tofauti kubwa ya jinsi gani CCM inapeleka nguvu zake. Huwezi kulinganisha jinsi CCM ilivyopania kuichukua Busanda na jinsi ilivyopandia kuichukua Biharamulo.

Jambo kubwa ambalo ni zoezi kwa chadema ni jinsi gani kuweza kushinda sasa kwenye majimbo ya CCM maana sasa hivi hakuna tena uchaguzi mdogo hadi uchaguzi mkuu mwakani.

Ninachokiona sasa ni CCM kuanza kujipanga kuyakomboa majimbo ya upinzani na kuyarudisha CCM.

Na suala la kuungana mimi nilishassema mapema, hakuna ulazima wa Chadema kuungana na chama kingine bali kujijenga ili kiweze kuwa chama mbadala na hili ni kweli kwa CUF vile vile. Endapo kutakuwa na ulazima wa kuungana basi ni muungano wenye kuunganisha fikra, sera, katiba, mitazamo n.k na siyo muungano wa kuiondoa CCM.

majimbo yote ambayo Chadema imeshinda yalikuwa ni ya CCM, CCM ilijijenga zaidi ya miaka 30. Kazi iliyopo mbele yetu ni sisi sote kama wana wa demokrasia ya kizazi kipya kukipa nguvu Chadema kwa kuelimisha wajomba , shangazi, binamu, mama na baba ili kuwasaidia wagombea wa chadema kuwa na mazingira mazuri kushinda kuanzia ngazi ya vijiji, kata nk. Chadema ni watu na watu ni mimi na wewe na yule.

Sote tumedhurika na utawala dhalimu wa serikali ya CCM hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuelimisha na kutoa mawazo chanya jinsi ya kutokomeza utawala wa kiimla wa serikali ya CCM. Wasomi, vijana, wazee na wanaharakati mnakaribishwa sana Chadema kujenga Chama ili kushiriki katika mfumo huru na wa demokrasia ya kweli katika fikra huru.

Haba na haba ...........................
 
Pasco kapotea jumla.....keshakamata shori wa kisubi basi wanagonganisha glasi Robert hotel....
 
Nakumbuka ndugu Mtanzania alisema Chadema wasimuweke mgombea wao kule Biharamulo, bali wamuunge mkono yule wa TLP.

Mh! Logic zingine bwana! Za wasomi wa fasttrack hizo.

Watabiri wa hivo walikuwa wengi, hata mleta news wetu kipenzi Pasco alikuwa ameandika hivo kwamba wapinzani watagawana kura na CCM kuibuka kidedea, Ila kweli Mungu si Athumani, nimefurahia sana waongo hawa kushindwa,

Na sasa naomba Chadema msiache yafuatayo
-Endelezeni kesi ya uraia tata wa Oscar liwe funzo kwa waongo hao
- RPC msimuachie ili ajifunze kufanya kazi yake badala ya kuwa kibaraka
- Wale walio pigwa kanisani, fungueni kesi mahakamani, liwe ni fundisho kwa uhuni huo unaofanya eti green guard!!
 
-bwa ha ha ha ha sasa hivi FMES anakuja......mzee malecela kama ni mtindo wa nywele basi ni afro.....kapitwa na wakati.....
 
Where did the 67% disappear to.
Something is very wrong when 2/3 of the voters do not vote. All parties, the EC and GoT must sit down and untangle/clear this mystery.
 
Chuki zinakusumbua kijana kiasi ya kwamba likitajwa neno Uislam matumbo yako yanaunguruma. lol!

Udini kijana unakutafuna, hapa hujatoa maoni ya maana kazi yako unatafuta tu pale uislamu ulipoguswa, lol! After all mimi nilikuwa na-quote statement ya mtu mwingine, sasa shehe mbona waniandama mie ati!
 
achana na huyo kaona misalaba kwenye avatar yako kimemkera.....
anyway
hivi mmegundua hata wana CCM wenyewe hawaipendi CCM?am sure masatu kafurahia ushindi wa CHADEMA
 
Back
Top Bottom