Don't read too much into this. Local politics are not necessarily national politics. Kwa vile jimbo hilo tayari lilikuwa upinzani hivyo aliyeanguka zaidi si CCM bali TLP. Ndio maana ushindi wa Tarime pamoja na ukubwa wake wote ulitafsiri jambo moja tu nalo ni kurudisha jimbo mikononi mwa Chadema.
Hadi hivi sasa katika chaguzi hizi ndogo, Chadema haijaweza kushinda jimbo la CCM. Imeshindwa Tunduru, Kiteto, na Mbeya Vijijini. Na hii utaona tofauti kubwa ya jinsi gani CCM inapeleka nguvu zake. Huwezi kulinganisha jinsi CCM ilivyopania kuichukua Busanda na jinsi ilivyopandia kuichukua Biharamulo.
Jambo kubwa ambalo ni zoezi kwa chadema ni jinsi gani kuweza kushinda sasa
kwenye majimbo ya CCM maana sasa hivi hakuna tena uchaguzi mdogo hadi uchaguzi mkuu mwakani.
Ninachokiona sasa ni CCM kuanza kujipanga kuyakomboa majimbo ya upinzani na kuyarudisha CCM.
Na suala la kuungana mimi nilishassema mapema, hakuna ulazima wa Chadema kuungana na chama kingine bali kujijenga ili kiweze kuwa chama mbadala na hili ni kweli kwa CUF vile vile. Endapo kutakuwa na ulazima wa kuungana basi ni muungano wenye kuunganisha fikra, sera, katiba, mitazamo n.k na siyo muungano wa kuiondoa CCM.