Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Ndugu, watawekaje uislamu pembeni?? waache kuwa-waislamu khaa...huko chadema hakuna uislamu ebo mbona balaa sasa...onyesheni uso zenu...uislamu ni zaidi ya chama/siasa... be infomed.

I get you sir!!
 
Ila washikaji msione CUF kukataa matokeo siku zote kule kwenye visiwa vya Unguja na Pemba, ushindi wa tofauti ya kura chache unauma sana... ni sawa na kwenye soka goli la dakika ya 93 au 123.
 
Kama kweli CUF ina nia njema na ukombozi wa watanzania waungane na chadema kiwe chama kimoja kwani CUF bado wanakampumzi Zanzabar na Chadema wanapuma kwa kasi Tanganyika itaweweka pazuri sana kupambana na CCM la sivyo Cuf itakufa taratibu kama NCCR na TLP.

CUF fisadi papa RA kaisha waweka ndani, hapo sijui kama wataweza jitanzua!

CHADEMA sangala mshikilieni, mshindo wake ni mkubwa.

Hata Busanda tulijua kilicho tokea, kwahiyo 2010 hiyoooo, walau tupate Bunge la kueleweka.
 
rmashauri..
Kwenye dini ya kiislam unapoona muislam mwenzako anapambana na mgalatia ni mwiko kabisa kumtupa hata kama unajua ametenda makosa mabaya... hivyo usitegee Game theory amseme vibaya Ustaadhi Idrisa wa tanesco au Prof. Lipumba amseme vibaya sheikh Rostam Aziz...

Tehetehetehetehetehetehetehetehe,
Mzee kwa mtindo huu basi hatuwezi kuwa na wapiganaji halisi wa kiislamu maana kwao ni dini kwanza na maslahi ya nchi baadae, kitu ambacho ni hatari sana kwa maendeleo ya nchi zetu zenye machanganyiko wa dini.
 
Don't read too much into this. Local politics are not necessarily national politics. Kwa vile jimbo hilo tayari lilikuwa upinzani hivyo aliyeanguka zaidi si CCM bali TLP. Ndio maana ushindi wa Tarime pamoja na ukubwa wake wote ulitafsiri jambo moja tu nalo ni kurudisha jimbo mikononi mwa Chadema.

Hadi hivi sasa katika chaguzi hizi ndogo, Chadema haijaweza kushinda jimbo la CCM. Imeshindwa Tunduru, Kiteto, na Mbeya Vijijini. Na hii utaona tofauti kubwa ya jinsi gani CCM inapeleka nguvu zake. Huwezi kulinganisha jinsi CCM ilivyopania kuichukua Busanda na jinsi ilivyopandia kuichukua Biharamulo.

Jambo kubwa ambalo ni zoezi kwa chadema ni jinsi gani kuweza kushinda sasa kwenye majimbo ya CCM maana sasa hivi hakuna tena uchaguzi mdogo hadi uchaguzi mkuu mwakani.

Ninachokiona sasa ni CCM kuanza kujipanga kuyakomboa majimbo ya upinzani na kuyarudisha CCM.

Na suala la kuungana mimi nilishassema mapema, hakuna ulazima wa Chadema kuungana na chama kingine bali kujijenga ili kiweze kuwa chama mbadala na hili ni kweli kwa CUF vile vile. Endapo kutakuwa na ulazima wa kuungana basi ni muungano wenye kuunganisha fikra, sera, katiba, mitazamo n.k na siyo muungano wa kuiondoa CCM.
 
Ila huku bara tuachane na upuuzi wa kusema kura zinaibwa... yaani huwaga nikisikia hiyo sentensi huwa naona upuuzi mkubwa sana.
 
Ingawa matokeo rasmi hayajatangazwa, CHADEMA wameweza kuwashinda kwa karibu kabisa CCM kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Biharamulo hii leo.

Mpaka zinapatikana hesabu za mwisho CHADEMA ilikuwa ikiongoza kwa 50.4% huku CCM ikiifuatia kwa karibu ikiwa na asilimia 49.3% ya kura zote.

Matokeo yanatarajiwa kutangazwa rasmi punde

Lakini matokeo ambayo yamejumlishwa mpaka mwisho ni haya:

CHADEMA: 17,367

CCM: 16,483

TLP: 184

Turnout ilikuwa 33%
(incredible!)

Hongera CHADEMA.

Hivi wasio piga kura hawajui kuwa ni kutokupiga kura ni UJINGA? Kwa 2010 ili Vyam mbadala viwe na nafasi ni lazima hawa wahamasishwe kwa kweli.
 
Hongera CHADEMA!!!!!

The beginning of the end of Mafisadi in Tanzania is near. Uzi ni huo huo!! Endeleeni na "Operesheni Sangara" Mkoani Kagera, mkihakikisha ktk kila kijiji mnasimika viongozi kuanzia ngazi ya shina. Baada ya Kagera, mikoa yote ambayo bado OS haijafika hakikisheni mnakwenda. Hakuna kulala; Mpaka Kieleweke!!
 
rmashauri..
Kwenye dini ya kiislam unapoona muislam mwenzako anapambana na mgalatia ni mwiko kabisa kumtupa hata kama unajua ametenda makosa mabaya... hivyo usitegee Game theory amseme vibaya Ustaadhi Idrisa wa tanesco au Prof. Lipumba amseme vibaya sheikh Rostam Aziz...
Macho mdiliko maana yake mtu hasiye ona ukweli na kukumbatia uongo. Na hapa umedhihirisha wazi kabisa... Hoja zako haziwezi kusimama zenyewe mpaka uongope!?
 
Mara baada ya kupata habari hizi kwamba Chadema wameshinda jambo la kwanza ilikuwa ni kuuliza kama katika kampeni hizi Mzee Tingatinga alitinga huko .Kwa nilikuwa nimepata ajali siweza kurudi tena Bukoba wenzangu wajulishaji wakasema ni kweli alikuwepo.Nikajiuliza hii maana yake nini kwamba wana Biharamulo wamekataa kata kata na kuamua kulinda kura zao ? Nimeona nisiumie kichwa bali nije hapa na kuuliza wajuvu nyie .Je huu ndiyo mwisho wa Malecela ama aliteleza tu huko bado ana nguvu za kuweka namna ya kuiba kura ?
 
Don't read too much into this. Local politics are not necessarily national politics. Kwa vile jimbo hilo tayari lilikuwa upinzani hivyo aliyeanguka zaidi si CCM bali TLP. Ndio maana ushindi wa Tarime pamoja na ukubwa wake wote ulitafsiri jambo moja tu nalo ni kurudisha jimbo mikononi mwa Chadema.

Hadi hivi sasa katika chaguzi hizi ndogo, Chadema haijaweza kushinda jimbo la CCM. Imeshindwa Tunduru, Kiteto, na Mbeya Vijijini. Na hii utaona tofauti kubwa ya jinsi gani CCM inapeleka nguvu zake. Huwezi kulinganisha jinsi CCM ilivyopania kuichukua Busanda na jinsi ilivyopandia kuichukua Biharamulo.

Jambo kubwa ambalo ni zoezi kwa chadema ni jinsi gani kuweza kushinda sasa
kwenye majimbo ya CCM maana sasa hivi hakuna tena uchaguzi mdogo hadi uchaguzi mkuu mwakani.

Ninachokiona sasa ni CCM kuanza kujipanga kuyakomboa majimbo ya upinzani na kuyarudisha CCM.

Na suala la kuungana mimi nilishassema mapema, hakuna ulazima wa Chadema kuungana na chama kingine bali kujijenga ili kiweze kuwa chama mbadala na hili ni kweli kwa CUF vile vile. Endapo kutakuwa na ulazima wa kuungana basi ni muungano wenye kuunganisha fikra, sera, katiba, mitazamo n.k na siyo muungano wa kuiondoa CCM.

MM,

Pamoja na yote, si haba...!!! Kigaila Benson, mwanamageuzi halisi unanisoma... Hongera sana.
 
kumbe siwapendi CCM......najihisi kama vile nina furaha
Si kama huwapendi CCM, ni kuwa nafsi yako inahitaji 'mabadiliko' na yanapotokea nafsi yako inafarijika kwa namna flani hivi...
 
...taratibu mzee, unamaanisha Prof. Lipumba akikaa na laptop yake pale Buguruni anaandika na kuita waandishi wa habari na kusemea lolote analotaka akisema ni msimamo wa chama chake?

Kasheshe,
Huyu msomi wetu kuna wakati huwa anatoa maoni yake na kuna wakati anatoa misimamo ya kichama. Sasa pale anapotoa maoni yake binafsi na yakaonekana yamepinda sisi wananchi tunachulia kama ndo chama kilivyo maana yeye ndo kioo cha chama ati!
 
I salute Chadema good ....Raha ndani ya Moyo..kwanza kwa Kumdhalilisha CCM, Hope come 2010 tutakuwa na wabunge wengi wa upinzani.
 
Tehetehetehetehetehetehetehetehe,
Mzee kwa mtindo huu basi hatuwezi kuwa na wapiganaji halisi wa kiislamu maana kwao ni dini kwanza na maslahi ya nchi baadae, kitu ambacho ni hatari sana kwa maendeleo ya nchi zetu zenye machanganyiko wa dini.
Chuki zinakusumbua kijana kiasi ya kwamba likitajwa neno Uislam matumbo yako yanaunguruma. lol!
 
Yaani Mrema pamoja na kupiga kelele zote hizo na kuwasagia CHADEMA kwamba nao ni mafisadi, ndiyo ameambulia kura 184 tu? Hii ni dalili mbaya sana kwa TLP.

TLP sasa haina tofauti na vyama vya akina Mziray ambavyo huwa vinasikika wakati wa uchaguzi tu na baada ya hapo hupotea kabisa. This is the end of TLP na Mrema mwenyewe.
 
Back
Top Bottom