Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Malecela should know the old Adage that CRIME DOESN'T PAY. Organizing the stealing of votes is criminal and planning or backing or turning a blind eye to the beating up of staggling young democrats in Tanzania is unpardonable.

At the age of 75, JSM, you should gracefully retire. Amen
 
Alaaa! basi makosa yangu inabidi nianze kuamini uwezo wa Chadema kusimama pekee, kumbe CUF na NCCR-Mageuzi pia walisimamisha wagombea?..
Heee, Imekuwaje hawana hata asilimia moja!

Mkandara,
Sorry mkuu inaonekana hapa kulikuwa na mshikeli kidogo katika kuweka kumbukumbu zangu sawa. CUF na NCCR mageuzi kumbe baadae waliamua kuunganisha nguvu zao kui-support TLP. Kwa maana nyingine hawakusimamisha wagombea japo inasemekana kuwa muunganiko wa NCCR Mageuzi na CUF nao ulikuwa katika makundi mawili moja liki-support CHADEMA moja liki-Support TLP.
 
Last edited:
Ni kweli CCM ilishinda chaguzi ndogo za Kiteto, Busanda, na Mbeya Vijijini. Pamoja na huo ushindi kitu kilichokuwa wazi ni kwamba CHADEMA walionyesha ushindani wa kuitoa jasho CCM.

Tukumbuke kwamba CCM ilikuwa inasaidiwa na NEC, Polisi na kutumia resources za umma kwenye kampeni. Kuna mawaziri waliacha ofisi wakaenda kusaidia kupiga kampeni wakitumia magari ya serikali. Kuna cases nyingi za jinai zilikuwa reported na hakuna kilichofanyika mpaka leo. Mfano, Kiteto akina Mtalemwa na wenzake walipigwa sana lakini polisi hawakufanya kitu. Kule Busanda kuna viongozi wa serikali za mitaa walikamatwa wakinunua shahada, mpaka leo hakuna kitu. Kuna magari yalionekana yakipakua magodoro kule Busanda NEC na Polisi hawakufanya chochote.

Kwa tathimini yangu hilo gap dogo la kura ni dalili nzuri kwa CHADEMA kwamba wakiweka wagombea wazuri na wakatumia vyema poor resources walizonazo, wanaweza kushinda viti vingi uchaguzi ujao wa 2010. Uchaguzi wa mwakani kutakuwa hakuna kusaidiana, kila mmoja anapambana kivyake jimboni kwake. Hao mawaziri kila mmoja atakuwa jimboni kwake akipiga kelele kivyake na Polisi hawatamwagwa wengi kwenye jimbo kama ilivyo sasa kwamba uchaguzi mdogo ukija Polisi wanamwagwa sehemu moja na hivyo kuongeza woga na sometimes hutumika kwa manufaa ya CCM.

Mkuu hili ndo tumaini letu, lakini hata hivo inabidi kupiga kelele kurekebisha NEC iliyopo sasa hivi iko biased mno! Lazima italeta ya Kivuiti tu
 
Hahaaaa imetulia hiii,

Ila nina uhakika wengi ndani ya CCM watakuwa wamefurahia CCM kudondokea pua, hasa wale ambao hawakufurahishwa na uongo wa kunganganiza mtu asiye raia kugombea! well kule wasubi huwa wana msemo wao hivi

''Bhasubi twimanye''

Duu hiyo niliyoitilia mkazo ndiyo siri ,CHADEMA wasifurahie sana huo ushindi ,Japo nawapa 5.

Wasubi huwa mara nyingi kama sio mara zote mtu mgeni kama siye musubi ni ngumu kushinda kule ,wale jamaa wanangalia mtu wao hawaangalii sana chama.

Nakumbuka vizuri MAGUFULI alibwagwa sana na marehemu Kabuye kwa msemo huo tu ulitosha sana kumutoa Magufuli nje ya ulingo,mpaka mwisho japo sina uhakika mpango ulifanyika kuligawa hilo jimbo ndiyo Pombe akapata kule.

Cha msingi hapa CHADEMA wanahaki ya kufurahia ushindi lakini pia waangalie kama wapinzania wao walikuwa wazawa ,bila hivyo mambo yanaweza badirika mwaka 2010 mpaka mkashindwa kuwaamini wasubi.
 
True, lakini 2010, Dr. mbassa si atatetea kiti chake? Kumbuka sasa hivi ataingia kwa nguvu na atakuwa anaanza kuonyesha ufanisi. kwahiyo mwakani kwake nadhani itakuwa rahisi zaidi!
 
Enzi za utawala wa kibabe,kiimla,kishetani,kisayuni na kibabeli wa CCM unakaribia kwisha!Kama tu ilivyotabiriwa kwenye bible kwa jinsi ambavyo utawala wa Roma utakavyo anguka ni vivyo hivyo DALILI zi wazi jinsi ambavyo utawala wa CCM ya zamani ya Mkapa umeanza kudidimia!

Hongera CHADEMA
 
True, lakini 2010, Dr. mbassa si atatetea kiti chake? Kumbuka sasa hivi ataingia kwa nguvu na atakuwa anaanza kuonyesha ufanisi. kwahiyo mwakani kwake nadhani itakuwa rahisi zaidi!

Mkuu nakubaliana na wewe sana,kitu cha kwanza nilichotaka kuwaambia CHADEMA ni kuwa wasijipe matumaini ama kuamini ushindi huo ni matokeo yao kukubarika kwa wasubi kama wanavyokubarika Tarime.

Pili ushindi ni mwembamba sana kiasi kwamba akija Msubi mwingine anayekubalika kubwagwa ni rahisi sana pale.

Angalia Kabuye alivyobwagwa na mwenzie wa ccm nayeye akiwa mbunge,na mbunge tena huyo akaja akabwaga na Kabuye wa TLP.Hivyo pale kwa wasubi ni pagumu upepo unabadirika sana
 
jamani haya mambo ya wasubi isiwe kisingizio hebu tuangalie mgawanyo wa makabila yalivyo huku. Sukuma 20%, waha 25, wasubi 35%, wahaya 10% and others 10% kwa hiyo wasubi ni 35% tu na nimekutana nao wengi tu ambao ni wanacham wa ccm kwa hiyo hili tuliache kabisa
 
Tatizo viongozi wetu sijui ni tamaa. I'm sure mzee anapesa za kutosha tu lakini sijui bado anatafuta nini. What's the point of doing something where you can no longer progress forward? Yeye the only thing he had left to look forwad to ni huo uraisi & there is no chance in hell that will ever happen.

Haa ha haaa ....inanikumbusha ile slogan ya mkewe wakati wakiutafuta urais...first lady anatoka Anna anaingia Anna.....
 
Haa ha haaa ....inanikumbusha ile slogan ya mkewe wakati wakiutafuta urais...first lady anatoka Anna anaingia Anna.....

Hahaha nilikua nimesahau hicho kitu. Ilikuwa inaelekea alikuwa anautaka kweli ufirst lady. Ndiyo maana sasa hivi ana malizia hasira zake zote kwa JK na serikali yake haha.
 
Hongera Chadema. Hongera wanabiharamulo west kwa kugoma kumchagua Mrundi/Mganda... Magufuli upo?
 
Nafikiri kutokana na ushindi huu wa CHADEMA na anguko kwa TLP, huu ni muda muafaka kwa Bw. Lyatonga Mrema kupumzika na kuwaachia vijana waendeleze TLP. Kama bado anahitaji kuendelea na siasa ni bora arudi SISIEMU alikotokea.
Mrema hata sasa hivi akiamua kugombea ukatibu kata kwa chama chake hawezi kupata kura za kumuwezesha kushinda huo uchaguzi.

Mrema, Kiraracha yakungojea, pumzika sasa.
 
Alaaa! basi makosa yangu inabidi nianze kuamini uwezo wa Chadema kusimama pekee, kumbe CUF na NCCR-Mageuzi pia walisimamisha wagombea?..
Heee, Imekuwaje hawana hata asilimia moja!

Mkandara

Mambo ya wapinzani kwa kweli inabidi tuwe tunaongea kwa tahadhari kubwa sana. Mimi ndiyo maana nimeamua nifunge safari nije nione mwenyewe. kweli wapinzani wakiungana kuna nguvu kidogo itaongezeka lakini ukiwasikia maneno yao hutataka waungane tena hata kama ni kushinda uchaguzi kwani utajua kuwa wana malengo tofauti kabisa. nina baadhi ya crip za mrema itabidi niziweke hewani nikifika sehemu yenye speed kubwa ili mjionee wenyewe mliokuwa mnataka eti chadema wajiunge na na chama kama TLP
 
SISIEMU watasema wameshindwa Biharamulo kwa sababu watu wa huko wana fedha za kununua magazeti, wana umeme wa kuwawezesha kuangalia TV kujua ni nini kinaendelea nchini, hawahitaji vitisho vya kunyimwa vibali vya kuchimbia madini kama Busanda........ wewe subiri utasikia tu hizo spins.
 
wewe unapafahamu Biharamulo?? pengine afadhali ya Busanda kule choka mbaya ndugu yangu.

Sema watu wavijijini watu wanaolazimisha wakawaelimishe ndio wenye mwamko na siasa tofauti na mjini kabisa.
 
Don't read too much into this. Local politics are not necessarily national politics. Kwa vile jimbo hilo tayari lilikuwa upinzani hivyo aliyeanguka zaidi si CCM bali TLP. Ndio maana ushindi wa Tarime pamoja na ukubwa wake wote ulitafsiri jambo moja tu nalo ni kurudisha jimbo mikononi mwa Chadema.

Hadi hivi sasa katika chaguzi hizi ndogo, Chadema haijaweza kushinda jimbo la CCM. Imeshindwa Tunduru, Kiteto, na Mbeya Vijijini. Na hii utaona tofauti kubwa ya jinsi gani CCM inapeleka nguvu zake. Huwezi kulinganisha jinsi CCM ilivyopania kuichukua Busanda na jinsi ilivyopandia kuichukua Biharamulo.

Jambo kubwa ambalo ni zoezi kwa chadema ni jinsi gani kuweza kushinda sasa kwenye majimbo ya CCM maana sasa hivi hakuna tena uchaguzi mdogo hadi uchaguzi mkuu mwakani.

Ninachokiona sasa ni CCM kuanza kujipanga kuyakomboa majimbo ya upinzani na kuyarudisha CCM.

Na suala la kuungana mimi nilishassema mapema, hakuna ulazima wa Chadema kuungana na chama kingine bali kujijenga ili kiweze kuwa chama mbadala na hili ni kweli kwa CUF vile vile. Endapo kutakuwa na ulazima wa kuungana basi ni muungano wenye kuunganisha fikra, sera, katiba, mitazamo n.k na siyo muungano wa kuiondoa CCM.

Asavali hapa umeongea kidogo!
 
Wakuu,

Nime-edit 1st post... Kuna mabadiliko kidogo ambayo ni muhimu kuzingatiwa!

Ukiangalia vema, utaona kuwa kituo kimoja kilichosalia hata CCM ikipata kura ZOTE haitaweza kuifikia CHADEMA...
 
Back
Top Bottom