Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

The title has been changed to reflect the unofficial results that have been received so far. Until the official pronouncement by the Returning Officer so far the winner of the election has not been announced. We are waiting for the official results this morning.For Admins.
Thanks Silencer, the heading is now perfect. Ile ya mwanza ilikaa kama JF ni Tume ya Uchaguzi ya JF. Najiandaa kurejea Biharamulo kusikiliza majumuisho ya kura, kama hakutakuwa na utata wowote, matokeo rasmi yatatangazwa saa 4 asubuhi hii mbele yamwenyekiti wa NEC, Jaji Agostino Ramadhani.
 
Invisible, wewe una amini kuwa CCM watakosa hizo kura 631 ili kulingana na CHADEMA wakati turnout ni 39.24%. usishangae kusikia kuwa final turnout ni 45% na hiyo percentage yote iliyo ongezeka wakawa wameipigia kura CCM.

Mkuu hiyo turnout rate inahusiana vipi na hizo kura 631?
 
Hongereni Chadema. Bila shaka nyie ndio tegemeo la Watanzania wengi. Wasomi karibu wote wanawaungeni mkono. Na sasa raia wengine nao wametambua ubora wenu

Nakuunga mkono Augustine Moshi, CCM huwa wanatumia nguvu nyingi na pesa nyingi sana (ambazo ni za walalalahoi) kwenye kampeni zao. Wakati umefika wa kufanya mabadiliko.

TANZANIA BILA YA CCM INAWEZEKANA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Mfano 2010 kwanini nijisumbue kupiga kura kwa mgombea urais kama safu itakuwa hivi,JK,Mbowe,Mrema,Lipumba
Hapo mimi itabidi niangalie. Zikiletwa mahakama za kadhi nitamchagua JK. Lakini zikiletwa na kugharamiwa na serikali nitamchagua Mbowe. Zisipoletwa kabisa nitamchagua Lipumba. Sioni condition yoyote itakayonishawishi kumchagua Mrema! 😀 😀 😀 😀
 
Pasco,

Mwenyekiti wa NEC ni Jaji Lewis Makame. Huyo uliyemtaja ni Jaji Mkuu
 
Mkuu hiyo turnout rate inahusiana vipi na hizo kura 631?

Kura 631 ni difference kati ya kura walizopata CHADEMA vs CCM. Kwa kuwa haya ni matokeo ya awali (yani yasiyo rasmi) usishangae kusikia kuwa kuna sanduku la kura lilikuwa bado halijafika kutoka kwenye kijiji kilicho ndani ndani kabisa. Hii ina maanisha kuwa turnout itaongezeka na kutokana na kuingezeka kwa hiyo turnout difference kati ya CCM na CHADEMA itabadilika. CCM wanaweza wakapata kura zaidi.

TANZANIA BILA YA CCM INAWEZEKANA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Wana JF nisaidieni kwa hili. Hivi ni kwa nini wanachelewa kutangaza matokeo kama wameshamaliza kuhesabu kura???
 
Wana JF nisaidieni kwa hili. Hivi ni kwa nini wanachelewa kutangaza matokeo kama wameshamaliza kuhesabu kura???

ni lazima ccm washinde. kura zinafanyiwa kazi ili ccm washinde kwa kura hata moja

macinkus
 
Kura 631 ni difference kati ya kura walizopata CHADEMA vs CCM. Kwa kuwa haya ni matokeo ya awali (yani yasiyo rasmi) usishangae kusikia kuwa kuna sanduku la kura lilikuwa bado halijafika kutoka kwenye kijiji kilicho ndani ndani kabisa. Hii ina maanisha kuwa turnout itaongezeka na kutokana na kuingezeka kwa hiyo turnout difference kati ya CCM na CHADEMA itabadilika. CCM wanaweza wakapata kura zaidi.

TANZANIA BILA YA CCM INAWEZEKANA, MUNGU IBARIKI TANZANIA

Mkuu Farmer, turnout haitambuliwi kwa kuhesabu kura, inatambuliwa kwa kujumlisha idadi ya waliojitokeza kupiga kura. Kumbuka maafisa wa tume pamoja na mawakala wa vyama vya siasa wanarecord kila mtu anayejitokeza kupiga kura. Hivyo turnout inajulikana mapema hata kabla ya kuanza kuhesabu kura.

Endapo kura zilizohesabiwa zitakuwa nyingi kuliko waliojitokeza kupiga kura basi matokeo ya vituo husika lazima yafanyiwe utafiti na kurekebisha kasoro. Pia itakuwa ni ishara ya wazi ya wizi wa kura kama alivyoaibika rais wa Iran.
 
Kura 631 ni difference kati ya kura walizopata CHADEMA vs CCM. Kwa kuwa haya ni matokeo ya awali (yani yasiyo rasmi) usishangae kusikia kuwa kuna sanduku la kura lilikuwa bado halijafika kutoka kwenye kijiji kilicho ndani ndani kabisa. Hii ina maanisha kuwa turnout itaongezeka na kutokana na kuingezeka kwa hiyo turnout difference kati ya CCM na CHADEMA itabadilika. CCM wanaweza wakapata kura zaidi.

TANZANIA BILA YA CCM INAWEZEKANA, MUNGU IBARIKI TANZANIA

o.k. nimekuelewa sasa mkuu.
 
weweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!1

good chadema!!!

Bravo!
 
Ishara inaonyesha sasa chadema taratibu inakubalika katika jamii. Ukiangalia idadi ya kura ilzopata Busanda ni ushara wazi ya wananchi kukikubali chama hicho. Hivyo ushindi wowote ule ni pigo kwa watawala kuwa mwisho wao u karibu
 
Nimeongea na Mtu wa CHADEMA aliyeko Biharamula, na bado amenihakikishia kuwa CHADEMA inaongoza au aniseme imeshinda ila kuna taarifa kuwa Makamba amesogelea mahali ambapo yanfanyika majumuisho ili kuvuruga matokea.
Wananchi wanajiandaa kusogelea eneo ilo ili kushinikiza matokeo kutangazwa bila kuvurugwa.
Nawasilisha
 
Mimi naamini CCM watafanya tu hujuma zao -- watamlazimisha Returning Officer (hawa huwa ni makada wa CCM maana Tume ya Uchaguzi huwa haina kauli kuhusu uteuzi wao) kumtangaza mgombea wao kuwa mshindi kwa kura chache kama 1,000 hivi. Nyie mtaona tu! Demokrasia ya kweli bado ngumu sana hapa nchini.
 
Nimeongea na Mtu wa CHADEMA aliyeko Biharamula, na bado amenihakikishia kuwa CHADEMA inaongoza au aniseme imeshinda ila kuna taarifa kuwa Makamba amesogelea mahali ambapo yanfanyika majumuisho ili kuvuruga matokea.
Wananchi wanajiandaa kusogelea eneo ilo ili kushinikiza matokeo kutangazwa bila kuvurugwa.
Nawasilisha

Sasa majumuisho ni ya nini tena kama kura zimesha hesabiwa???
Mimi naona kuna namna inayotakiwa kufanywa hii sio bure.
 
Nadhani nakubaliana nawe Kafiri. Mradi Makamba anasogelea, basi hujuma tayari iko njiani. Kwa nini nilizaliwa Tanzania?
 
Back
Top Bottom