Nadhani wajumbe mshafahamu matokeo kamili, CCM washafanya mambo yao kama kawaida, mbili imekuwa moja na moja imekuwa mbili. Ingawa wamefanya wizi kama kawaida yao lakini wajue kwamba haya mambo yana mwisho, hivyo ndivyo historia inavyotufundisha. Cha kujivunia ni kwamba sasa hivi wananchi wengi wameamka usingizini na CHADEMA wasikate tamaa, hizo asilimia walizopata zinaonyesha kwamba sasa CHADEMA ndo chama mbadala.
Akina zitto, Slaa, Mbowe kazeni buti wananchi wameanza kuwakubali. Uchaguzi mkuu unakaribia inatakiwa zifanyike juhudi za makusudi ili kulinda ushindi siku zijazo. Kabla ya uchaguzi ujao inabidi yafanyike mambo yafuatayo:
1 Iundwe tume huru ya uchaguzi, hii tume ya sasa haiaminiki ndo maana hata wananchi wanakosa hata moyo wa kupiga kura maana wanajua ni tume ni part and parcel ya CCM. wanafahamu kwamba ni yaleyale ya kuibiwa.
2. Kiundwe chombo kingine cha kusimamia chaguzi majimboni, Haiingii akilini kwamba maafisa wa serikali za mitaa wasimamie uchaguzi uwe fair wakati wao ni waajiliwa wa serikali ambayo inaongozwa na chama dola CCM. Hawa watendaji wakati mwingine wanatishwa kabisa wanapewa amri kwamba wakiruhusu upinzani kushinda kibarua chao kitaota mbawa! Waziri wa TAMISEMI akitoa amri wataikataa? bila shaka hawawezi.
3. Jeshi la polisi lisitumike kama ilivyo sasa, hiki chombo sasa hivi kinatumika kudidimiza demokrasia. Wakati kuna mapigano tarime polisi walioko Biharamuro ni wengi kuliko walio tarime, CCM wakishaiba uchaguzi polisi wanatumika kufanya ukandamizaji ili watu wasitoe malalamiko yao. Jana FFU walisambazwa Biharamuro ili kulinda wizi wa CCM. Kwa hiyo hili jeshi lijitoe kwenye siasa, kukiwa na transparency hakuna haja ya kumwaga askari, askari wanaletwa wengi kwa kuwa haki haitendeki, kwa hiyo amani inabidi ilindwe kwa nguvu, lakini wajue kwamba paka ukimfungia chumbani bila kuacha upenyo mwishowe atakurarua.
4. Wana mageuzi inabidi kuelewa historia kwamba hakuna haki inayokuja kama lulu, Haki upiganiwa, siku ya kupiga kura utasikia wanakwambia kwamba ukishapiga kura nenda nyumbani, hii ina maana gani? Hii inakusudia kile kituo kibaki na wawakilishi wa vyama ndani ya vyumba ili iwe rahisi kuwahonga matokeo yabadilishwe, uchaguzi ujao hakuna kwenda nyumbani mpaka kieleweke. matokeo yahesabiwe vituoni wapiga kura wote tushuudie kama tumeshinda au tumeshindwa. Hivyo virungu vya askari tuvivumilie lakini haki yetu tupate!
Yasipofanyika hayo hapo niliyotaja hapo juu itakuwa ni kilio tu, CCM wangefurahi kama wangerudisha nchi katika utawala wa chama kimoja, huu ni ujinga na nimesema wajinga sijasema wapumbavu maana kuna uwezekano wa kuwaelimisha wakaelewa. Ndugu zangu watanzania tusikubali hili.