Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Nadhani wajumbe mshafahamu matokeo kamili, CCM washafanya mambo yao kama kawaida, mbili imekuwa moja na moja imekuwa mbili. Ingawa wamefanya wizi kama kawaida yao lakini wajue kwamba haya mambo yana mwisho, hivyo ndivyo historia inavyotufundisha. Cha kujivunia ni kwamba sasa hivi wananchi wengi wameamka usingizini na CHADEMA wasikate tamaa, hizo asilimia walizopata zinaonyesha kwamba sasa CHADEMA ndo chama mbadala.
Akina zitto, Slaa, Mbowe kazeni buti wananchi wameanza kuwakubali. Uchaguzi mkuu unakaribia inatakiwa zifanyike juhudi za makusudi ili kulinda ushindi siku zijazo. Kabla ya uchaguzi ujao inabidi yafanyike mambo yafuatayo:

1 Iundwe tume huru ya uchaguzi, hii tume ya sasa haiaminiki ndo maana hata wananchi wanakosa hata moyo wa kupiga kura maana wanajua ni tume ni part and parcel ya CCM. wanafahamu kwamba ni yaleyale ya kuibiwa.

2. Kiundwe chombo kingine cha kusimamia chaguzi majimboni, Haiingii akilini kwamba maafisa wa serikali za mitaa wasimamie uchaguzi uwe fair wakati wao ni waajiliwa wa serikali ambayo inaongozwa na chama dola CCM. Hawa watendaji wakati mwingine wanatishwa kabisa wanapewa amri kwamba wakiruhusu upinzani kushinda kibarua chao kitaota mbawa! Waziri wa TAMISEMI akitoa amri wataikataa? bila shaka hawawezi.

3. Jeshi la polisi lisitumike kama ilivyo sasa, hiki chombo sasa hivi kinatumika kudidimiza demokrasia. Wakati kuna mapigano tarime polisi walioko Biharamuro ni wengi kuliko walio tarime, CCM wakishaiba uchaguzi polisi wanatumika kufanya ukandamizaji ili watu wasitoe malalamiko yao. Jana FFU walisambazwa Biharamuro ili kulinda wizi wa CCM. Kwa hiyo hili jeshi lijitoe kwenye siasa, kukiwa na transparency hakuna haja ya kumwaga askari, askari wanaletwa wengi kwa kuwa haki haitendeki, kwa hiyo amani inabidi ilindwe kwa nguvu, lakini wajue kwamba paka ukimfungia chumbani bila kuacha upenyo mwishowe atakurarua.

4. Wana mageuzi inabidi kuelewa historia kwamba hakuna haki inayokuja kama lulu, Haki upiganiwa, siku ya kupiga kura utasikia wanakwambia kwamba ukishapiga kura nenda nyumbani, hii ina maana gani? Hii inakusudia kile kituo kibaki na wawakilishi wa vyama ndani ya vyumba ili iwe rahisi kuwahonga matokeo yabadilishwe, uchaguzi ujao hakuna kwenda nyumbani mpaka kieleweke. matokeo yahesabiwe vituoni wapiga kura wote tushuudie kama tumeshinda au tumeshindwa. Hivyo virungu vya askari tuvivumilie lakini haki yetu tupate!

Yasipofanyika hayo hapo niliyotaja hapo juu itakuwa ni kilio tu, CCM wangefurahi kama wangerudisha nchi katika utawala wa chama kimoja, huu ni ujinga na nimesema wajinga sijasema wapumbavu maana kuna uwezekano wa kuwaelimisha wakaelewa. Ndugu zangu watanzania tusikubali hili.
 
Poti,
Pamoja na kukubali "ushauri" wako wa ku-quote yote lakini siwezi kuzungumzia neno kwa neno kama ulivyojadili. Mimi nimejaribu kuzungumzia hoja mojawapo uliyoitoa na ambayo umeirudia tena hapa. Yaani ni kusema kwamba tuendelee tu kutokuwa na tume huru ya uchaguzi?kama kweli umesoma na unapenda maendeleo ya demokrasia huwezi kamwe kutetea kuendelea/kushikilia tume ya uchaguzi iliyo biased, tume isiyo huru kabisa, tume inayokitumikia ccm na kuhakikisha kuwa hakishindwi.
ushauri wa kususia kazi nao ni low(samahani kwa hilo) kwa kuwa unategemea hao wafanyakazi watajimudu vipi?unadhani wapenda mageuzi wote ni wafanyakazi wa serikali ya ccm kama unavyodhani?je ni wapi hiyo style ya kususia kazi iliwahi kufanyika na ikafanikiwa?
halafu poti wangu usipende ku-generalise mambo, mimi kuwa na mawazo tofauti na yako haimaanishi kuwa mimi ni mchadema kama wewe ulivyo m-ccm.Na kama huu mfumo dhalimu wa kuwa na tume ya uchaguzi isiyo huru unanufaika nao, basi waache wale wasionufaika nao waseme.Mimi nitakuunga mkono na mguu ikiwa kutakuwa na jukwaa lililo sawa kwa vyama vyote kuendesha siasa na mwisho wa yote kuwe na mwamuzi(tume ya uchaguzi iliyo huru) asiye na mahaba na chama chochote.

Mkuu vipi tena
Mimi nimewashauri hivyo baada ya wao wakereketwa wa chama chenu kupropose kumwaga damu,ndio nikaonelea ni bora kususia kazi maana wataendelea kuishi hata kwa mbinde kuliko kumwaga damu zao ,logic hiyo ni ngumu kueleweka mkuu.? Kuiona hiyo ni low na ukaisapoti ile nyingine itakuwa sio low tuu bali..........

Harafu mbona walia nani kaanza kugenalize kuwa mimi ni ccm ? hii ni tabia ya wafuasi wa chadema ,ukiona mtu anakuita ccm ama fisadi wewe hitimisha tu kuwa huyu ni chadema.

Poti mimi sina chama chochote ila sina hakika na wewe kuwa si mfuasi wa chadema, mawazo yangu ndiyo chama changu sifungamani na upande wowote ,tatizo kubwa lililoko hapa ni lile la mtazamo wa Ki-Bush Bush eti ya kwamba ili uwe great thinker ama mtu asiyeshusha plofile lake ama anayetowa point za uhakika lazima uisapoti chadema kinyume chake wewe fisadi ama unatowa low .

Hili ni tatizo kubwa kwa chama chenu ,tena linaenda mbali sana hata ktk hadi uongonzi wenu huko juu lakuona yanayofanywa na ninyi ni sahihi tu hivyo kwa vyovyote vile mtaungwa mkono tu na wengine hakuna kitu na kinyume chake kwa vyovyote vile mtakuwa mumeibiwa kura ama mmeonewa.
 
Wewe ndugu una akili sana ..... yaani umegundua kuwa umwagaji damu ni kitu kibaya sana kabla ya wana chadema wote hawajagundua hili? Inabidi upewe nafasi ya ushauri mkuu hapa JF.

Harafu mbona walia nani kaanza kugenalize kuwa mimi ni ccm ? hii ni tabia ya wafuasi wa chadema ,ukiona mtu anakuita ccm ama fisadi wewe hitimisha tu kuwa huyu ni chadema.

Kwani ni makosa kuwa mwana ccm? unaniangusha sasa!

Nilitegemea kuwa elimu kubwa uliyoipata ingekusaidia kufanya uamuzi wa kuwa na msimamo kwenye maisha.

Diagnosis tayari imeshatolewa ...... mhh ..... nimenyanyua mikono
 
Kama inavyoeleweka mpaka sasa CCM washafanya mambo yao, moja imekuwa mbili na mbili imekuwa moja. Chaguzi za serikali za mitaa zinakaribia na uchaguzi mkuu mwakani. Wapenda demokrasia na vyama kwa ujumla kabla ya uchaguzi inabidi kushinikiza yafanyike yafuatayo:
1. Tume ya sasa ya uchaguzi ivunjwe iundwe upya na muundo wake usiwe uteuzi wa Rais kama ilivyo sasa. Wananchi wamekata tama sana na hii tume ya sasa, ndo maana hawaendi kupiga kura wanajua ni yale yale ya kuibiwa. CCM wanaiba shaada tume imenyamaza , watu wanauawa tume imenyamaza kwa kuwa yenyewe ni part and parcel ya huo uozo. Huyo bwana Makame hajawahi kutwambia alirudisha lini kadi ya uanacma wa CCM!
2. Kiundwe chombo kipya cha kusimamia chaguzi za majimboni. Haiingii akilini kwamba watumishi wa almashauri wasimamie uchaguzi kwa haki, Hawa ni waajiliwa wa serikali ambayo inaongozwa na chama dola CCM. Hawa watumishi wakati mwingine wanapenda kutenda haki lakini wanatishwa mno, wanaambiwa kabisa kwamba wakiruhusu ushindi kwa upinzani vibarua vyao vitaota mbawa! Bila shaka hakuna mtu atalikubali hilo. Hivi waziri wa TAMISEMI akitoa amri kuna mtumishi atakayebisha? Bila shaka hakuna.
3. Jeshi la polisi lifundishwe majukumu yake upya, linatakiwa lifundishwe namna ya kutumikia wananchi wote bila ubaguzi. Sasa hivi hili jeshi linatumika kukandamiza demokrasia katika nchi yetu. Wakati wa uchaguzi Biharamuro polisi waliokuwa huko walikuwa wengi kuliko walioko Tarime ambako kuna mapigano ya kikabila. Kwa nini ? wanapelekwa huko kulinda maovu. CCM wakishafanya wizi polisi wanatumika kufanya ukandamizaji ili watu wasitoe malalamiko yao. Baada ya matokeo batili kutangazwa Biharamuro FFU walisambazwa kuhakikisha kwamba wananchi hawatoi malalamiko yao. Wafahamu kwamba haya yana mwisho, paka ukimfungia sana chumbani bila kumuachia upenyo mwishowe atakurarua.
4. Wapenda demokrasia na vyama kwa ujumla inabidi tujifunze kutokana na Historia, hakuna haki inayokuja hivi hivi tu kama lulu, waliopata haki zao walizipigania na wengine kupoteza maisha. Tusiwe waoga. Wakati wa uchaguzi utasikia matangazo ya CCM na vyombo vyake kwamba ukishamaliza kupiga kura nenda nyumbani! Hii ina maana gani? Maana halisi ya hili ni kwamba mkiondoka mkaenda nyumbani wanabaki na wawakilishi wa vyama kwenya vyumba vya kuhesabia kura kwa hiyo kama unavyojua umaskini wa watanzania wanatumia mwanya huo kuwahonga ili wabadilishe matokeo. Hiyo ndo siri ya hiyo slogan. Ucahguzi ujao hili tusilikubali, tubaki vituoni mpaka matokeo yatoke kama ni kushinda au kushindwa ijulikane kila mmoja aridhike.Virungu vya polisi tuvivumilie lakini haki yetu tupate!
5. Wanamageuzi (siwaiti wapinzani) wakaze buti, CHADEMA hususan wanatakiwa waelewe kwamba hizo asilimia walizopata katika chaguzi za busanda na Biharamuro zinaashiria kwamba sasa ndo chama mbadala, kinatakiwa kijitangaze zaidi hususan vijijini kifungue matawi ya wanachama, kiwashawishi wasomi wa fikra mbalimbali ili kiwe na watu wa kushika nyadhifa za kuongoza nchi siku zijazo. Wanamageuzi waelewe kwamba CCM wangefurahi kama nchi hii ingerudi katika mfumo wa chama kimoja, ni wajinga! Sijawaita wapumbavu maana muda upo wa kuweza kuwaelimisha wakaelimika. Tusikubali waturudishe tulikotoka.
 
Mkuu vipi tena
Mimi nimewashauri hivyo baada ya wao wakereketwa wa chama chenu kupropose kumwaga damu,ndio nikaonelea ni bora kususia kazi maana wataendelea kuishi hata kwa mbinde kuliko kumwaga damu zao ,logic hiyo ni ngumu kueleweka mkuu.? Kuiona hiyo ni low na ukaisapoti ile nyingine itakuwa sio low tuu bali..........

Harafu mbona walia nani kaanza kugenalize kuwa mimi ni ccm ? hii ni tabia ya wafuasi wa chadema ,ukiona mtu anakuita ccm ama fisadi wewe hitimisha tu kuwa huyu ni chadema.

Poti mimi sina chama chochote ila sina hakika na wewe kuwa si mfuasi wa chadema, mawazo yangu ndiyo chama changu sifungamani na upande wowote ,tatizo kubwa lililoko hapa ni lile la mtazamo wa Ki-Bush Bush eti ya kwamba ili uwe great thinker ama mtu asiyeshusha plofile lake ama anayetowa point za uhakika lazima uisapoti chadema kinyume chake wewe fisadi ama unatowa low .

Hili ni tatizo kubwa kwa chama chenu ,tena linaenda mbali sana hata ktk hadi uongonzi wenu huko juu lakuona yanayofanywa na ninyi ni sahihi tu hivyo kwa vyovyote vile mtaungwa mkono tu na wengine hakuna kitu na kinyume chake kwa vyovyote vile mtakuwa mumeibiwa kura ama mmeonewa.

hata mtu mwenye elimu ndogo tu ya kujua kusoma na kuandika hahitaji ufafunuzi kama huu unaoutoa hapa.Kwasababu kwa akili yako mtu asiyekubaliana na madudu yanayofanywa na tume ya uchaguzi unajua kuwa ni chadema hapo sina la kukusaidia kwasababu we si msomi?
sisi wengine hapa hatuko kuisupport chadema wala ccm wala cuf wala tlp, bali tunasupport demokrasia ya kweli ili iweze kushamiri nchini mwetu.
hata kama ukisema wewe sio ccm mabandiko yako yanadhihirisha hivyo, ingawa si wana ccm wote wanaokubaliana na faulo zinazaochezwa na chama chao pamoja na tume ya uchaguzi, na katika hao wewe si mmoja wao.Ngoja tu nikuache uendelee kusherekea kwa ushindi wa tsunami mlioupata biharamulo.
 
Sio lazima kuwe na tume huru wala nini wafanykazi wote wakiacha kazi na mtanzania yoyote akakataa kazi mpaka ccm itakapong'oka mbona ni tiba tena ya week tu

Ndugu yangu hadi hapo, kwakweli umechangia very low.
Kama unadai kwamba wazee wako vijijini walikutuma ukasome upate elimu kisha uje kuwasaidia kuondokana na hali duni, na hapo juu umeonyesha kuwa umesoma kama ulivyotumwa na wazee wako.
Lakini ghafla unapogeuka na kutoa hoja dhaifu kama hii, nabaki kuwaonea huruma hao wazee wako huko kijijini. Watakuwa wamekula hasara kama hali yenyewe ndio hii.Tangu mwanzo nilikuwa nasoma post zako naona kama una kitu cha maana unataka tukifahamu toka kwako, pamoja na mapenzi yako ya dhati kwa ccm, lakini kwa ushauri huu, umejishusha mno. Pole sana yego mwamba.

Mkuu angalia hapo palipokandamizwa ,hii ni post yako ya kwanza kabisa kati yako na yangu.

Tatizo mnapenda sana huruma ili kupata sapoti ,mtajitahidi kwa kila hali kujenga point zenu kwa kumuhusisha mhusika ama na ccm ama na ufisadi HAKIKA hili ni tatizo kwenu na limekuwa sugu.
 
hata mtu mwenye elimu ndogo tu ya kujua kusoma na kuandika hahitaji ufafunuzi kama huu unaoutoa hapa.Kwasababu kwa akili yako mtu asiyekubaliana na madudu yanayofanywa na tume ya uchaguzi unajua kuwa ni chadema hapo sina la kukusaidia kwasababu we si msomi?
sisi wengine hapa hatuko kuisupport chadema wala ccm wala cuf wala tlp, bali tunasupport demokrasia ya kweli ili iweze kushamiri nchini mwetu.
hata kama ukisema wewe sio ccm mabandiko yako yanadhihirisha hivyo, ingawa si wana ccm wote wanaokubaliana na faulo zinazaochezwa na chama chao pamoja na tume ya uchaguzi, na katika hao wewe si mmoja wao.Ngoja tu nikuache uendelee kusherekea kwa ushindi wa tsunami mlioupata biharamulo.

Kwa hiyo kwa kutokubaliana na tume jibu lake ni kumwaga damu? Kwa kweli mie siwaelewi
 
Wewe ndugu una akili sana ..... yaani umegundua kuwa umwagaji damu ni kitu kibaya sana kabla ya wana chadema wote hawajagundua hili? Inabidi upewe nafasi ya ushauri mkuu hapa JF.

Kwani ni makosa kuwa mwana ccm? unaniangusha sasa!

Nilitegemea kuwa elimu kubwa uliyoipata ingekusaidia kufanya uamuzi wa kuwa na msimamo kwenye maisha.

Diagnosis tayari imeshatolewa ...... mhh ..... nimenyanyua mikono

wewe poiti zako nawe zinahitaji kuombewa si bure teh teh teh, msimamo upi unaongelea?
 
Mkuu angalia hapo palipokandamizwa ,hii ni post yako ya kwanza kabisa kati yako na yangu.

Tatizo mnapenda sana huruma ili kupata sapoti ,mtajitahidi kwa kila hali kujenga point zenu kwa kumuhusisha mhusika ama na ccm ama na ufisadi HAKIKA hili ni tatizo kwenu na limekuwa sugu.

Baraka Obama angefuata ushauri wako (wa kuongelea sera tu bila kuhusisha ubovu wa chama cha republican) angepata kura nyingi zaidi kuliko huo ushindi wa kiduchu aliopata.

Mkuu, my hat is off!
 
Baraka Obama angefuata ushauri wako (wa kuongelea sera tu bila kuhusisha ubovu wa chama cha republican) angepata kura nyingi zaidi kuliko huo ushindi wa kiduchu aliopata.

Mkuu, my hat is off!

teh teh teh teh
Kweli kazi ipo, kwa hiyo kwa mtu yeyote aliyekuwa aki argue na Obama lazima alikuwa anataja Republican kujenga hoja yake teh teh teh teh teh teh .Huruma tupuu
 
teh teh teh teh
Kweli kazi ipo, kwa hiyo kwa mtu yeyote aliyekuwa aki argue na Obama lazima alikuwa anataja Republican kujenga hoja yake teh teh teh teh teh teh .Huruma tupuu

Yaani hata kicheko chenyewe cha kisomi kabisa. Yaani mkuu wewe ni jiniasi wa hali ya juu. Inabidi uendelee kutoa shule yako hapa maana inahitajika sana (hasa namna ya kuongelea ushindani wa kisiasa bila ya kuongelea mapungufu ya mpinzani wako).
 
Awali:

Ingawa matokeo rasmi hayajatangazwa, CHADEMA inaelekea wameweza kuwashinda kwa karibu kabisa CCM kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Biharamulo hii leo.

Mpaka zinapatikana hesabu za mwishomwisho kukiwa bado kituo kimoja cha Nyabugombe B chenye wapiga kura 394 CHADEMA ilikuwa ikiongoza kwa 50.6% huku CCM ikiifuatia kwa karibu ikiwa na asilimia 48.8% ya kura zote na TLP ikiwa imejinyakulia 0.55% ya kura zote.

Matokeo yanatarajiwa kutangazwa rasmi punde

Lakini matokeo ambayo yamejumlishwa mpaka dakika hii ni haya:

CHADEMA: 17,313

CCM: 16,682

TLP: 187

Turnout ilikuwa 39.24% (incredible!)

========================================

UPDATE 1...

Matokeo ya kituo kwa kituo tuliyoyapata toka kwa mwakilishi wa JF jimboni humo yameambatanishwa hapa chini kama attachment:

i511_matokeobiharamulomagharibi.jpg

========================================

UPDATE 2.

Tume ya uchaguzi imesema hivi:

CCM: 17,561 = 51%

CHADEMA: 16,670 = 48.4%

CHADEMA wameyakataa matokeo kwani wanadai matokeo ya kata 3 yamegeuzwa tofauti na walivyosaini wasimamizi wa matokeo na yalivyohesabika vituoni!

========================================

Update 3.

Tume ya Uchaguzi imemtangaza mgombea wa CCM kama mshindi kwa kura zinazoonyeshwa kwenye Update ya awali ingawa CHADEMA wameyakataa matokeo ya vituo 9 kati ya vituo 237 vya uchaguzi!

========================================

Invisible,
Kwa kutambua kuwa hii forum si ya kushabikia chama chochote cha kisiasa au kundi fulani, basi iko haja ya kutolea maelezo vyanzo vya habari vya takwimu ulizozichapisha hapo juu. Kitendo cha kuleta habari nyeti kama za matokeo ya uchaguzi huku zikuwa na upotoshaji wa hali ya juu nadhani ni kitendo cha kukiangalia kwa makini kiifanye forum hii kuwa ni ya kupigia debe makundi fulani ya kisiasa.
Ninasema hivyo kwani taarifa uliyoichapa hapo juu ina makosa makubwa ambayo unaweza kuona kuwa yametokana na kutokuwa makini kwa mpokea taarifa au mpokea taarifa alikuwa na agenda nyingine iliyojificha. Nia yangu si kukurushia lawama, bali nikuondoa na kupiga vita dhana zozote zile za upotoshaji wa jambo.
Kwa mfano kimahesabu haiwezekani hata siku moja katika mchakato wa kuhesabu kura namba ikahesabika kutoka kubwa kwenda ndogo, ni wazi kabisa huenda chanzo chako kili-doctor / manipulate figures hizo kwa nia ya kutaka kuleta mkanganyiko hapa jamvini. Kwa jinsi matokeo ya kura zilizopigwa pale Biharamulo, vyama vya CCM na CHADEMA vilikuwa na nafasi zinazokaribiana kabisa katika kutwaa ushindi wa kiti kile. Kushinda kwa CCM haiwezekani ionekane kuwa ni kitu cha ajabu au kutondwa kwa CHADEMA ionekana kuwa ni uonevu. CHADEMA imekwenda Biharamulo huku iktambua wazi kuwa CCM tayari inarekodi nzuri ya kupanga mikakati ya ushindi katika majimbo mawili ya Mbeya (V) na Busanda, kwa maana hiyo CCM ilikuwa inategemewa zaidi kushinda Biharamulo kuliko hata CHADEMA. Kitu ambacho CHADEMA watajivunia kwa sasa pale Biharamulo ni kuweza kupata kura nyingi kuliko walizozipata 2005 lakini si kulalamikia ushindi wa CCM.
Namalizia kwa kusema kuwa hizi habari za matumizi ya wananchi bila ya kujali itikadi ni vyema zikawa ni zile ambazo zimethibitishwa na mamlaka halali au la basi hii ingekuwa imetolewa na CHADEMA kama malalamiko halali kwa Tume ya Uchaguzi wakipinga matokeo.
 
Wewe ndio mpotoshaji au mgumu kuelewa au Hujaelewa hata maelezo ya Invisible au ndio ATTACK ambazo zinalenga kumdhibiti MOD wetu? Mbona unaweka vitisho vya kisheria visivyo na miguu wala kichwa; Kwa ufupi tume mpaka sasa ian taarifa hizi pale ila majibu ya mwisho yaani majumuisho yako tofauti na hizi unazoona hapa;
Chadema hawaendi mahakamani sababu ya muda ni mfupi wa mwaka mmoja na wanasubiria umma utoe hukumu na ni kwa kuangalia ukweli huu ambao kila mmoja wetu mkiacha wachache mnaotumiakia matyumbo yenu kwa manufaa yenu ; Mbunge wenu kwa taarifa ana kesi tatu huku Biharamulo mpaka sasa (independent cases);

1. Kesi ya Kugombea jimbo la Tanzania wakati in real sense ni Mganda ( si MTZ)
2. Kesi ya Wizi wa Kura
3. Kutumia rasilimali za Tanzania kwa manufaa ambayo kwa wazalendo tunaamini ni kwa ajili ya waganda
Ukiona inakuuma sana wewe kama kada mzuri Nenda mahakamani kaishitaki JF kama itakuwa hamjishitaki wenyewe ili aondolewe kwenye Ubunge wake wa kuchonga ( yaani wa mezani
 
Last edited:
Sijawaelewa kabisa unasemaje juu ya taarifa hizo. Huyu jamaa hapa juu ndio hajaelewa kabisa.
 
MOST OF PRO CCM HAWAPENDI HII MOD IENDELE; NA KUTOIPENDA HII HEADLINE NI SAWA NA KUANZA JF KUKATAA UKWELI; NA HIYO NI HATARI SANA KWA MSTAKABALI WA NCHI NA JF KWA UJUMLA; KUONDOA UKWELI KWANGU NI SAWA NA KUANZA UFISADI; NI SAWA NA KUNIFUKUZA JF MAANA IM NOT READY TO BE USED/USE BY ANY WAY; JF SHOULD AS WELL NOT BE USED/USE by ANY WAY; SO THOSE RESULTS FOR US STILL HOLDS; WANABIHARAMULO HAPA WANAANGALIA HAWANA LA KUSEMA ILA UKWELI WANAO HUO NDIO UZURI WA JF
 
Biharamulo waishtukia CCM -MAJIRA
Wednesday, 08 July 2009 06:32
Na Suleiman Abeid, Kagera

SIKU moja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuibuka na ushindi kiduchu katika uchaguzi
mdogo jimbo la Biharamulo Magharibi mkoani Kagera, baadhi ya wakazi wa jimbo hilo wamelalamika na kudai kuwa chama hicho kina ajenda ya siri ya kuua demokrasia ya vyama
vingi vya siasa nchini.

Wakazi hao wametoa kauli hiyo kutokana na kile walichodai uendeshaji wa kampeni za CCM uliofanywa maeneo mbalimbali na viongozi wake na hotuba za makada wake zilizoonesha wazi kuwa chama hicho hakikubaliani na mfumo wa vyama vingi hapa nchini.

"Kwa kweli inaelekea chama tawala hivi sasa hakitaki tena nchi hii kuendeshwa chini
ya mfumo wa vyama vingi kutokana na jinsi vigogo wa chama hicho walivyokuwa
wakituhutubia katika mikutano yao ya kampeni, walieleza wazi kuwa iwapo tutamchagua
mbunge kutoka upinzani hatutapata maendeleo,"

"Hizi kauli kwa kweli zilitushitua watu wengi, na hata baadhi yetu tuliona hakuna
haja ya kwenda kupiga kura kwa maana ni wazi kuwa tuliamini iwapo tutamchagua
mgombea tunayemtaka lakini anatoka katika chama cha upinzani, basi tutakuwa
tumejinyima maendeleo," alieleza Bi. Victoria Modest mkazi wa mjini Biharamulo.

Bi. Modest alisema Serikali ya CCM imeonesha udhaifu mkubwa katika kuvumilia mfumo
wa vyama vingi hapa nchini na kwamba haikuwa busara kutumia 'fimbo' ya kuwanyima
wananchi wake maendeleo kwa kigezo tu kuwa wamemchagua mbunge kutoka chama cha
upinzani.

Kwa upande wake mkazi wa kijiji cha Kabindi kata ya Runazi, Bw. Steven Barikwegonza
alisema umefika wakati wa viongozi wa CCM waamue bila ya woga kufuta mfumo wa vyama
vingi nchini kutokana na kuonekana wazi kuwa wameshindwa kuvivumilia vyama vingine
vya siasa hapa nchini.

"Hebu ndugu mwandishi fikiria kauli ambazo zilikuwa zikitolewa na mheshimiwa Makamba
(Yusufu Makamba) Katibu Mkuu wa CCM Taifa, alisema wazi eti wakazi wa Biharamulo
tulifanya makosa makubwa mwaka 2005 kuchagua mbunge kutoka chama cha upinzani, na
hii ndiyo sababu ya kukosa kwetu maendeleo,"

"Alitueleza wazi kuwa safari hii tusirudie kosa iwapo shida yetu ni maendeleo, sasa
hii haiingii akilini, iweje wananchi ambao ndiyo tunaolipa kodi inayoendesha nchi
hii bila kujali mlipaji anatoka chama gani cha siasa, sasa inapofika wakati wa
kuchagua viongozi tupangiwe watu wa kuwapigia kura tena ni wale wa kutoka CCM?,"
Alihoji Bw. Barikwegonza.

Bw. Barikwegonza alishauri kuwa iwapo hivi sasa wananchi hawatakiwi kuwapigia kura
wabunge ama madiwani kutoka vyama vya upinzani ni vizuri CCM ikapeleka mswada
bungeni ili kuufuta rasmi mfumo wa vyama vingi, vinginevyo hakuna haja ya kuendelea
kuendesha chaguzi ambazo hazina tija.

"Tazama kila kinapofika kipindi cha uchaguzi serikali inatenga fungu la fedha kwa
ajili ya kuendeshea shughuli hiyo, lengo ni kutoa nafasi ya demokrasia kwa wananchi
wa Tanzania kuchagua viongozi wanaowataka na wanaoamini kuwa watawafanyia kazi,
lakini CCM wanasema mkichagua upinzani hakuna maendeleo, uchaguzi wa nini sasa?"
Alihoji.

Kwa upande mwingine wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
wamelalamikia kile walichodaiwa kitendo cha ‘kupokwa' kwa ushindi walioupata katika uchaguzi huo na wanaamini kuwa mgombea wa chama chao, Bw. Mbasa Gervas ndiye
aliyeshinda .

Wanachama hao waliungana na viongozi wao wa kitaifa kudai kuwa CCM ilishinikiza
mgombea wake Bw. Oscar Mukasa kutangazwa kuwa mshindi japo walielewa alishindwa katika uchaguzi huo baada ya kupata kura 16,682.

Walidai kuwa mgombea wao wa CHADEMA katika uchaguzi huo alipata kura
17,313 na yule wa TLP kuambulia kura 187 matokeo ambayo hata hivyo yalikataliwa na
msimamizi wa uchaguzi na kuzua mtafaruku mkubwa kutoka kwa viongozi wa CHADEMA.

Viongozi hao walidai kuwa matokeo yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi Bw. Zubeir Mbiana yalikuwa 'yamepikwa' huku wakidai kuwepo njama katika vituo tisa vya kata ya Nyarubungo.

Katika uchaguzi huo mgombea wa CCM Bw. Mukasa alitangazwa mshindi kwa kupata
kura 17,561 sawa na asilimia 50.9, wakati Bw. Gervas wa CHADEMA alipata kura 16,700
sawa na asilimia 48.46 na mgombea wa TLP aliambulia kura 198 sawa na asilimia 0.6.
 
Back
Top Bottom