MATOKEO Darasa la Saba si yenyewe

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Serikali inabaka elimu. Jana nilipigiwa simu na Afisa mmoja wa Baraza la Taifa la Mitihani akiniomba msaada wa kisheria.Ni juu ya kutishiwa kwake kufukuzwa kazi kama hatakubali kupitisha matokeo ya darasa la saba 'yaliyotengenezwa'. Afisa huyo wa Idara ya Mitaala,pamoja na vigogo wenzake NECTA,walipokea amri kutoka Mamlaka za juu za nchi wahakikishe kuwa matokeo ya darasa la saba yanavutia. Yeye akaonesha kugomea amri hiyo. Kazi yake iko mashakani.

Sasa ananiandaa niwe Wakili wake pale atakapofukuzwa kazi kwa kugomea kupitisha matokeo yaliyochakachuliwa. Mimi niko tayari.Nimemwambia aendelee kukusanya nyaraka ili tuuwashe moto. Elimu yetu inadhalilishwa,inabakwa,inauliwa.Hatuwezi kukubali.

NB: Matokeo yatatangazwa wakati wowote kuanzia leo
 
Isije ikawa mmepika vinavyopikwa, ili mtuletee uzushi. Habari uliyoileta ni ya kuambiwa, sasa je kama umeingizwa chaka itakuwaje?
 
tukianza kuleta mchezo kwenye swala la elimu ujue tanzania tumeshaichimbia kaburi tena la futi 100.
 
That's very Possible kuna afisa Elimu Mmoja ameniambia matokeo ya Mwaka huu ni mabaya sana na serikali imegoma kuyatangaza yamerudishwa serikalini kwanza it's very Possible kwa ajili ya kuchakachuliwa
 
 
Hata siku moja NECTA haijawahi toa matokeo HALALI hata ya chekechea wakitoa ni ***** mtupu
 
Mi sifikirii kam yanachakachuliwa bali yatakua yanfanyiwa stanadadization ili yakae sawa.
Na kwa nini watu wailaumu tu serikali wasichukue tahadhari kabla ili kusaidia mambo yasiharibike
wakati waalimu wanagoma kudai stahiki zao watu walifikiri kwamba mambo ynaisha kwa mtindo huo
lakini madhara yake yataonekana kama tahadhari haitachukuliwa.
 

Tahadhari iliyochukuliwa mapema na Serikali ni kuzima mgomo wa waalimu mahakamani halafu wakawa wamewashinda walimu. HAyo ndo matokeo mazuri lakini wiki moja iliyopita kulikuwa na maswala ya ELimu Feki kama bidhaa za kichina!!
 
huyu bwana anakosea kabisa!na anakiuka miiko ya utumishi wa umma
kama amepewa maagizo kutoka juu anatakiwa atekeleze ,kama anaona kitamtia hatiani akwepe sio kukataa kutamletea matatizo makubwa,maamuzi mengine huwa ya nakuwa kwa maslahii ya nchi si vizuri kuanza kuyatilia shaka
pia huyo bwana anatoa siri za ofisi kwa watu wanjee sio jambo jema kwa mtumishi wa umma aliyekula kiapo cha utii kwa serikali iliyopo madarakani
 
lakini nilimbiwa na mmoja wa wakaguzi wakuu katik moja ya mikoa ya kanda ya ziwa kwanba wamekutana na vituko katika selection. anasema shule ambazo zinakawaida ya kupokea wanafunzi 200 zilikuwa zinaishia wanafunzi 120 kwani ushindi ulikuwa hovyo mno.
kwa upande wa walimu wakawa wanachekelea kwamba mgomo wao umejibu.
 
Hapo kwenye red ndiyo maana nchi inayumba, maana watumishi wamekuwa wakitekeleza hata maagizo ya kipumbavu.
 

Akusanye ushahidi wa hayo makaratasi ya matokeo halisi ikiwezekana na scripts chache za wanafunzi ambao anuhakika wamefeli lakini wamepewa marks za bure. He can collect as many as possible ushahidi uwe na nguvu vinginevyo watakufukuza na hutakuwa na ushahidi wa kuwabana,.
 
hapo kwenye red ndiyo maana nchi inayumba, maana watumishi wamekuwa wakitekeleza hata maagizo ya kipumbavu.

nami naungana na wewe,watumishi wa umma wamechangia kwa kiasi kikubwa kuiharibu hii nchi kwa kisingizio cha kiapo cha utii.pum............zenu,fyyyyyyyyyuuuuuuuuuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…