VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Serikali inabaka elimu. Jana nilipigiwa simu na Afisa mmoja wa Baraza la Taifa la Mitihani akiniomba msaada wa kisheria.Ni juu ya kutishiwa kwake kufukuzwa kazi kama hatakubali kupitisha matokeo ya darasa la saba 'yaliyotengenezwa'. Afisa huyo wa Idara ya Mitaala,pamoja na vigogo wenzake NECTA,walipokea amri kutoka Mamlaka za juu za nchi wahakikishe kuwa matokeo ya darasa la saba yanavutia. Yeye akaonesha kugomea amri hiyo. Kazi yake iko mashakani.
Sasa ananiandaa niwe Wakili wake pale atakapofukuzwa kazi kwa kugomea kupitisha matokeo yaliyochakachuliwa. Mimi niko tayari.Nimemwambia aendelee kukusanya nyaraka ili tuuwashe moto. Elimu yetu inadhalilishwa,inabakwa,inauliwa.Hatuwezi kukubali.
NB: Matokeo yatatangazwa wakati wowote kuanzia leo