jaxonjaxon
JF-Expert Member
- Nov 21, 2014
- 217
- 136
Mbunge mmoja kapost hii kitu, nawe itafakari ili upate, mwelekeo:
ila matokeo ya kidato cha nne ni uozo mtupu. People are too clever,Matokeo yametolewa kwa mfumo wa GPA ambazo watahiniwa/wahitimu wenyewe hawawezi kuzichanganua ili kujua GPA husika inamaanisha nn, na wameenda mbali zaidi kwa kutoa GPA zisizofanana hata kidogo na zile za vyuo ili hata kaka zao, dada zao au wazazi wa hao wahitimu wasiweze kuzichanganua.
Walisema madaraja yatakua hivi...
0.0-0.1 Fail
0.2-1.5 Pass
1.6-2.5 Credit
2.6-3.5 Merit
3.6-5 Distinction
Kutokana na zile pass ambazo mtu anakua amepata kwenye somo husika, kwa kufuata mtiririko huu ufuatao...
A>>> 75 - 100
B+>> 60 - 74
B>>> 50- 59
C>>> 40 - 49
D>>> 30 - 39
E>>> 20 - 29
F>>> 0 - 19
Kwa maana hiyo utapata ukipata marks kulingana na grade hizo utakua umeangukia kwenye mojawapo ya alama hizi...
A=5
B+=4
B=3
C=2
D=1
E=0.5
F=0 Lakini tatizo bado lipo, kwa wale wataalamu wa kukokotoa wakijaribu kutumia alama hizo kukokotoa matokeo ya mtu wanakuta alichoandikiwa kama ni Pass au distinction hakifanani na ukokotozi sahihi, kwa mfano...
Mtu aliyepata
CIVICS - C
HIST - C
GEO - C
KISWA - B
ENGL - B
PHY - B
CHEM - B
BIO - B
MATH - D
Ukikokotoa kulingana na mfumo wao na grade zao zilivyopangwa unapata 2.44 ambayo ni credit, ila wao wanamuandikia 2.7 ambayo ni Merit. Kuna tatizo hapa.
Nadhani waTz tumekua wajinga sana, hauwezi kumpa mtu matokea ambayo hata yy hayaelewi.
ELIMU NI BURE
Ni 2.7 hivyohivyo, bcoz wanajumlisha masomo 7 aliyofanya vizuri then wanagawa kwa 7
B+B+B+B+B+C+C=19÷7=2.7
