Matokeo kidato cha pili 2012 hatimae yatolewa, mkoa wa D'salaam washika mkia.

Matokeo kidato cha pili 2012 hatimae yatolewa, mkoa wa D'salaam washika mkia.

Ni longterm effect of mgomo

unajua ubabe hausaidi maana unayemfanyia ubabe ana akili timamu na anajua anweza fanya nini na sehemu ipi. Ninavyoona serikali isalimu amri kwa walimu na madaktari wawalipe madai yao haraka iwezekanavyo
 
Walimu walishagoma tokea zamani na haya ndo matokeo yake, Watu wakisema walimu wana mgomo baridi serikali inabisha! Haya sasa!
 
Mimi nafikiria mawaziri wahusika wajihizuru maana hili jahazi limeshawashinda kabisa. Nimemsikiliza akisema hata Dar wananfunzi wamefail sana

Au wazazi turudishiwe ada zetu kama watoto wanafeli kwa ukosefu wa vitendea kazi na walimu. Bora mtupe hizo hela tuwapeleke VETA.
 
Walimu walishagoma tokea zamani na haya ndo matokeo yale, Watu wakisema walimu wana mgomo baridi serikali inabisha! Haya sasa!
Haya ni matokeo ya walimu bado ya madaktari kudadadeki tutakuoma sisi tusiokuwa na hata nauli za kwenda Apolo....
 
Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi, waziri Mulugo, ameshangazwa na matokeo mabaya kwa wanafunzi wa kidato cha pili ambapo Dar es salaamu ndiyo mkoa ambao wanafunzi wamefanya madudu sana! Akizungumza na waandishi wa habari leo wakati akiyatangaza matokeo ya kidato cha pili, ametumia muda huo kupinga dhana iliyoyojengeka kwamba wanafunzi wanafeli kwa sababu hakuna walimu akitolea mfano jiji la Dar es salaam kuwa na walimu wengi na bado wanafunzi wamefeli. Ametoa wito kwa wazazi kufatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni, na pia akawataka waalimu wajiulize sababu ya hawa wanafunzi kufeli.

MY TAKE:
Sijui mulugho anataka kusema nini lakini wizara ndiyo ambayo inapaswa kutupa majibu, kama waziri anayehusika na elimu anaona matokeo mabovu anashangaa na kuuliza maswali sijui wananchi watakua katika hali gani, ni miaka mingi sasa wizara ya elimu inafanya madudu na kuchezea elimu za watoto wetu, tunaomba Rais aitizame elimu kama kitovu cha maendeleo!

Kweli asiyejua maana hambiwi maana hata akiambiwa maana haelewi maana, Mulugo anataka wazazi wafuatilie maendeleo ya watoto wao 100% correct, walimu wajiulize kwa nini watoto wamefeli 100% halafu basi, mimi ninchojua elimu inajumuisha wadau wakuu watatu

1. Serikali.
2 Mwalimu
3. Mzazi
Ametaja wadau wawili mwalimu na mzazi, maana yake ni kwamba wala hata serikali haioni tatizo kwao wao hakuna haja ya kukaa na kutathmini hili, kweli tunawaziba nafasi si viongozi!
 
Labda nichukue fursa hii kumkumbusha Naibu Waziri Mh (Amin) Philipo Mulugo kuwa NG'OMBE JIKE ASIPOLISHWA VIZURI HAWEZI KUTOA MAZIWA. Leo tunashangaa matokeo na kujadili kuhusu sababu ya kufeli na cha kushangaza zaidi anatoa wito kwa wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto shuleni, hii haisaidii kabisa. Mwaka jana kulikuwa na mgomo wa watukufu walimu nchi nzima na hata baada ya mgomo walimu hao waliahidi kundelea na mgomo kwa style ya kutofundisha kwa weledi. Kifupi cha mambo haya ni kwamba matokeo ya kidato cha pili, cha nne cha sita na mengine yatakayokuwa chanzo chake ni serikali yenyewe. Yaelekea Philipo ni msahaulifu sana juzi tu kasababisha leo anashangaa.
Mh Mulugo that is YOU.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Penye miti hapana wajenzi,watoto wa dar wanawaza movies,kucheza viduku,kuimba nyimbo,sasa unafikiri mtoto atachomokaje hapo? Baba,mama wanakaa na mtoto kwenye tv toka 1 jioni wanacheck philipians movies mpaka saa 5,kunakuchomoka hapo?
 
kutokana na kipato cha walimu na elimu yao hawakuwa na ubabe wa kufanya mgomo wa moja kwa moja kwa mwezi hata mmoja kwani tuna jua serikali inaweza kuwaita walio maliza chuo, six na four kwenda kuchukua nafasi zao sasa walicho kiamua ni hicho unachokiona kwenye matokeo mpaka kieleweke..
mgomo gani tena mkuu mbona nchini saizi shwari tu......
 
Tatizo la serikali yetu ya CCM badala ya kushughulika na kiini cha tatizo wao wanafanya mibadala rahisi ili mambo yaende. Mfano kiwango cha ufaulu kilianza kushuka siku nyingi, ila wao badala ya kushughulika na vyanzo, wanakimbilia kushusha viwango vya ufaulu. Kwanini wasishughulikie matatizo sugu ya walimu? Kwanini wasiboreshe mazingira ya elimu (madarasa, vifaa, motisha kwa walimu nk). Sijui baada ya miaka 10 tutakuwa na rasilimali watu wa aina gani nchini. Inashangaza kuona hata TCU walishusha viwango vya ufaulu wa kuingia/kudahiliwa vyuo vikuu vya serikali nchini, nahisi hapo baadaye ukiwa na E moja tu utaruhusiwa kujiunga na chuo kikuu. Mibadala rahisi kwa mambo sensitive, kisa tumalizie uongozi salama.
 
Kuna mtu anaweza kueleza hapa Dr Shukuru Kawambwa anafanya nini? Tunajua Naibu waziri wake hajui hata Tanzania ni muungano na nchi gani? Sasa Waziri wake yuko wapi, na anafanya nini?

Miaka yote hii watoto wanafeli lakini Wizara bado inatoa porojo? Hakuna actions kabisa!
 
Kweli asiyejua maana hambiwi maana hata akiambiwa maana haelewi maana, Mulugo anataka wazazi wafuatilie maendeleo ya watoto wao 100% correct, walimu wajiulize kwa nini watoto wamefeli 100% halafu basi, mimi ninchojua elimu inajumuisha wadau wakuu watatu

1. Serikali.
2 Mwalimu
3. Mzazi
Ametaja wadau wawili mwalimu na mzazi, maana yake ni kwamba wala hata serikali haioni tatizo kwao wao hakuna haja ya kukaa na kutathmini hili, kweli tunawaziba nafasi si viongozi![/QUOTE Bubu Msemaovyo amemaliza kila kitu...Serikali ndiyo chanzo cha haya yote na bado...
 
Last edited by a moderator:
Huyu Waziri utafikiri ni mgeni na matatizo ya elimu ya Tanzania.
1. Migomo ya walimu haitatuwi kwa muda muafaka, hivyo walimu hawana morali ya kufundisha
2. shule nyingi za Kata hazina walimu, hivi kweli waziri hajui shule za kata hazina walimu?
3. Wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza wana vigezo, maana wengine hawajui kuandika jina lake utegemee nini hapo.

wizara ya Elimu tanzania ijipange upya sio kuwahadaa watanzania kuwa kuna elimu hapa, mbona nyinyi viongozi watoto wenu wanasoma nje na sio hapahapa.
 
wameshusha na kiwango cha ufaulu std 7! siku hizi mtihani wa hesabu std 7 ni multiple choice, yaani ni ujingaaaaaaa ambao hata mayai yangu kwenye ovaries hayawezi kubali!! stupid me kuendelea kuwa na vitu vyenye rangi ya KIJANI!

macho yangu yana tabu kutoka machozi kwa kufurahi!
khaaaaaa
 
tafadhali naomba maali amabapo naweza kuyapata hayo matokeo kitaifa maana ninashida ya kuangalia mjibu ya mdogo wangu kama nae ni miongoni mwao
 
wameshusha na kiwango cha ufaulu std 7! siku hizi mtihani wa hesabu std 7 ni multiple choice, yaani ni ujingaaaaaaa ambao hata mayai yangu kwenye ovaries hayawezi kubali!! stupid me kuendelea kuwa na vitu vyenye rangi ya KIJANI!

Mayai yako kwenye ovaries!!!!??? Asprin ana mke aisee dah
 
Last edited by a moderator:
Hiki kinachofanyika ni makusudu kabisa kwa hii Serikali ya CCM
- Kwani wao Ujinga wa Watanzania ndiyo manufaa yao kuendelea kututawala, kwani haiingii akilini mtu apewe Kofia, Fulana na scaf halafu hakipigie kura hicho chama kama shukhrani kwa zawadi hiyo

- Huku kudumaza kwa elimu kwa walala hoi ni manufaa yao pia kwani watoto wao shule wanazosoma ni tofauti na hizi shule kwahiyo watoto wao mwisho wa siku tukiingia kwenye soko la ajira wao watapewa kipaumbele kutokana na CV zao

- Kama Hii serikali ingekuwa na nia ya dhati kutatua tatizo la elimu katika nchi hii kwa nini wameshindwa kutatua tatizo la walimu kimaslahi? kwani tukilinganisha shule za Private na hizi za Mchangani(Serikali) zinatofautiana sana kiufauru kwani wenzetu wa Private walimu wanafanya kazi pasipo manung'uniko na wanakubaliana na malipo wanayopata kutokana na makubaliano ya mikataba yao.
 
Back
Top Bottom