Matokeo kidato cha pili 2012 hatimae yatolewa, mkoa wa D'salaam washika mkia.

Matokeo kidato cha pili 2012 hatimae yatolewa, mkoa wa D'salaam washika mkia.

maskini tanzania .me wakati nasoma elimu haikuwa kwa kiwango cha kizembe namna hii sijui tunaelekea wapi jamani
 
matokeo hayo waweza kuyaona wapi, mwenye adress yake tafadhali maanahata kwenye website ya wizara ya elimu sijaona
 
Ndugu wana JF,

Naibu waziri wa Elimu Philip Mulugo ametangaza matokeo ya kidato cha pili kupitia vyombo vya habari, Channel Ten ikiwa mmoja wapo wa vyombo hivyo na yalikuwa kama ifuatavyo hapo chini:

1. Waliofanya mtihani 386,248
2. Waliofaulu 249,325 (65%)
3. Waliofeli 136,923 (35%)

Karibuni kwa tathmini wadau wote
 
Wana JF naomben hata Link kupata hayo matokeo.
 
Wana Jf naomben hata Link kama inawezekana, au matokeo ya Zanaki
 
Mbona tena mwisho ch10 wamesema matokeo yaliyosomwa yanadosari? Jamani Mulugo mbona mwaka kauanza mapema hivi? Ngoja tusibiri atarudije na marekekebisho yake lawama zote zitakuwa kwa wasaidizi wake
 
Hiyo ndiyo Tanzania yetu jamani!!!!!!!

Na bado unakuta uongozi husika bado inang'ang'ania madaraka! Shenzi sana!
 
Hivi tuko serious kweli jamani?? Yaani 35percent ya waliofanya mtihani wa form two wameshindwa 'kufaulu' mtihani ambao passmark yake ni average ya 30percent??
Kwa kweli mimi naona hata hiyo passmark ya 30percent ni ndogo sana, lakini bado hata hiyo bado inasumbua kiasi hicho?? There is something wrong in our education system.............
 
Waalim wa Dar wako busy na miradi maana serikali ilishatupa waalim!!! Wako mgomo seriously!!!

Ikiwa kama DSM inashika mkia, je Shinyanga, Singida, Mtwara, Lindi zitashika nafasi ya ngapi?
Napata kizungumkuti ninaposikia DSM imeshika mkia.
 
shule zilizofanya vibaya ni kutoka mikoa ya kusini mwa Tanzania, Lindi na Pwani. naona mkoa wa Pwani nao kauhamishia kanda ya kusini. . mh kweli wizara imepata naibu
 
Ikiwa kama DSM inashika mkia, je Shinyanga, Singida, Mtwara, Lindi zitashika nafasi ya ngapi?
Napata kizungumkuti ninaposikia DSM imeshika mkia.

Ina maana kama DSM imeshika au iko karibia na mkia, mikoa tajwa inaweza kuwa imeishinda DMS ambayo resources angalao ni better off (madarasa, japo kukaa chini kule kwa St. Kayumba kupo, waalim, tution, etc)!! Ni aibu sana kwa taifa hili!! Ngoja utaona hata wa kidato cha tano miaka ijayo ili wapate wa kutosha watashusha pass mark ya kidato cha nne!! kama walivyofanya kwa darasa la saba.
 
Ndugu wana JF,

Naibu waziri wa Elimu Philip Mulugo ametangaza matokeo ya kidato cha pili kupitia vyombo vya habari, Channel Ten ikiwa mmoja wapo wa vyombo hivyo na yalikuwa kama ifuatavyo hapo chini:

1. Waliofanya mtihani 386,248
2. Waliofaulu 249,325 (65%)
3. Waliofeli 136,923 (35%)

Karibuni kwa tathmini wadau wote
Mkuu hawajafafanua kati ya hizo 35% fail shule za kata zipo ngapi?
 
Back
Top Bottom