DJkus
JF-Expert Member
- Nov 9, 2018
- 354
- 469
Vilaza LST ila vipanga vyuo watokavyo? Hebu fikiri kwa sauti....angalia hoja za wahanga hao na sio jibu la pamoja lisilo na msingi kwa malalamiko tajwaWatu wamekuwa vilaza. Tuache kulalamika.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vilaza LST ila vipanga vyuo watokavyo? Hebu fikiri kwa sauti....angalia hoja za wahanga hao na sio jibu la pamoja lisilo na msingi kwa malalamiko tajwaWatu wamekuwa vilaza. Tuache kulalamika.
Acha nicheke.Mimi ni mwalimu wa shule ya sheria niseme tu ukweli kutoka moyoni naumia sana kuona vijana wanafauru kwa wingi, eti kijana mdogo tu wa miaka 28 eti na yeye ni wakili
Safari ya kudai haki haijawahi kuwa rahisi.
Tulipo kumeundwa tume ambayo composition yake ni suala jingine.
Cha kushangaza kutokea kwenye website ya matokeo ya LST cohort 33 kuna ukarabati mpya!
Awali kulikuwa na cases za marks dash (-) kwenye somo moja mtu kafaulu na dash (-) kwenye somo jingine mtu kafeli.
View attachment 2385998
Maajabu ya Mussa. Ghafla na punde tu, wamebadilisha!
Sasa hivi kwenye dash (-) mtu kafeli wamebadili kwa kuindoa dash na kuwa "F". Hii ni mpya!
View attachment 2386000
Bila shaka wangali wana shauriana cha kufanya kwenye dash (-) mtu kafaulu iweje.
Tunaendelea ku monitor kila hatua wanayofanya.
Hili, hadi mbivu na mbichi zijulikane.
Unadhani wasomi wote nguli tuna mtazamo mmoja?
Watanzania hasa wanafunzi wanapenda dezo sana na mteremko sana! Watu wamefeli badala wajipange kurudia mitihani wanakwenda kushitaki kwa wanasiasa !
Hivi hata form four wakiwa wanafeli hatutashangaa wakilalamika na ikaundwa tume!
Wanasiasa wanataka watu wajinga wajinga wasio na vigezo mtaani ili wawatawale vizuri......
Hao walimu wamekuwa wakifanya mambo ya hovyo makusudi kuwakomoa wanafunzi, wakijua hakuna mwanafunzi atakayelalamika kwani matokeo mabaya yamekuwa ndio tabia yao miaka yote.
Sasa haya malalamiko ya wakati huu ndio yamewaamsha usingizini, hawakutegemea; matokeo yake wanakurupuka kufanya jambo bila kujua jambo hilo hilo walishalifanya mwanzo tofauti, hawa wanazidi kujitega.
Huu ni uthibitisho mwingine usioacha shaka, matokeo ya wanafunzi hapo LST huchezewa kwa makusudi na walimu wajuaji wasiojali, huku kisingizio chao siku zote kikiwa wanafunzi walipotoka hawakuandaliwa vizuri.
Ikiwa wanafunzi ambao ni wafanyakazi wa taasisi za umma wakiongoza kwa ufaulu, sijui wao waliandaliwa vizuri vyuo gani walipotoka tofauti na wanafunzi wengine wa hapo LST.
Mkuu nawashauri endeleeni kupambania suala hili, naamini litasaidia sana hata katika vyuo vingine ambapo lecturers huwa na imani ya kushikilia hatma ya maisha ya wanafunzi wao.