Matokeo Law School yafanyiwa ukarabati

Watu wamekuwa vilaza. Tuache kulalamika.
Vilaza LST ila vipanga vyuo watokavyo? Hebu fikiri kwa sauti....angalia hoja za wahanga hao na sio jibu la pamoja lisilo na msingi kwa malalamiko tajwa
 

Watanzania hasa wanafunzi wanapenda dezo sana na mteremko sana! Watu wamefeli badala wajipange kurudia mitihani wanakwenda kushitaki kwa wanasiasa !

Hivi hata form four wakiwa wanafeli hatutashangaa wakilalamika na ikaundwa tume!

Wanasiasa wanataka watu wajinga wajinga wasio na vigezo mtaani ili wawatawale vizuri......
 

Kwani wewe ni mmoja wa wanafunzi hao?

Miaka nenda rudi malalamiko haya yapo.

Wewe hujawahi kusikia wanafunzi kufelishwa?
 

NI kawaida kwa waonevu kudhani maisha yataendelea hivyo hivyo Hadi kurudi Messiah mara ya pili. Wasijue hayapo marefu yasiyokuwa na mwisho.
 
Mkuu nawashauri endeleeni kupambania suala hili, naamini litasaidia sana hata katika vyuo vingine ambapo lecturers huwa na imani ya kushikilia hatma ya maisha ya wanafunzi wao.

Aluta continua na kelele za chura ni nadra kumteteresha mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…