Matokeo Necta2012Kutenguliwa

BUMIJA

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
5,950
Reaction score
11,295
Magazeti leo yanasomeka kua JK atengue matokeo hayo,je ni njia nzuri ya kuboresha elimu na unazani matokeo yakitenguliwa Form 4 watakua tayari kusoma wakafanye mitihani au ni kulazimishia ufaulu
 
badala aje na strategic za kuboresha elimu ya TZ anakuja na wazo la kutengua so hata next yea atatengua?
 
Magazeti leo yanasomeka kua JK atengue matokeo hayo,je ni njia nzuri ya kuboresha elimu na unazani matokeo yakitenguliwa Form 4 watakua tayari kusoma wakafanye mitihani au ni kulazimishia ufaulu
Magazeti gani hayo mkuu, si uyataje angalau moja
 
asitengue,matokeo yameonyesha hali halisi,lilipo ni kujiuliza shida ipo wapi ili tujenge elimu bora.kutengua itakuwa ujinga zaidi.HEKO KWA SERIKALI MAANA INAONYESHA IMEDHIBITI UIBAJI WA MITIHANI.
 
Magazeti leo yanasomeka kua JK atengue matokeo hayo,je ni njia nzuri ya kuboresha elimu na unazani matokeo yakitenguliwa Form 4 watakua tayari kusoma wakafanye mitihani au ni kulazimishia ufaulu

Serikali ikifanya hivyo Elimu itakuwa imezikwa rasmi. Wanafunzi wafeli halafu uwafaulishe!
Nijuavyo, kufeli mtihani sio kutojua tu bali hata kutofuata na kuzingatia maelekezo uliyopewa.
 
Mwache atengue na mtazamo hasi aliokuwa nao,ni ajabu xana kutenda kosa na kuzidi kulijadili kosa!kwanini asijadili ni namna gani atalitatua hili tatizo,mawaziri na viongozi wa secta zote nchini kwa kushirikiana na wadau wa elimu jaribun kumshauri huyo raisi.
 
Kwan matokeo kua mabaya au mabovu nani atatakiwa kuwajibika
 
Mtoa mada muongo hakuna gazeti lilioandika hiyo habari, sana sana alichokisema kawambwa ni kuwa kufeli kwa wanafunzi chanzo ni kuwa serikali imedhibiti mitihani
 
asitengue,matokeo yameonyesha hali halisi,lilipo ni kujiuliza shida ipo wapi ili tujenge elimu bora.kutengua itakuwa ujinga zaidi.HEKO KWA SERIKALI MAANA INAONYESHA IMEDHIBITI UIBAJI WA MITIHANI.

pia wawatengenezee walimu mazingira mazuri ya kuwahamishia walichonacho akilini kwenda kwa wanafunzi
 
Jamaa anashaurika kwani? Nadhani anaamini ni upepo tu na utapita
 
Alaf jaman mwanafunzi anafutiwa matokeo yake na sababu za kufanana kwa mitihani ikiwa undani wake sababu zinajulikana,, paper ya computer practical wakat wa ku print kaz zinatoka nying na kukuta wanawekewa na wengine majib ya mtu mmoja tu hili baraza wanalizungumziaje na kuna uhakika wa mwanafunzi huyu kuyapata majib yake
 
Kama kawaida yetu wabongo, tunapenda kuchakachua na zima moto. Huyo aliyesema Rais atengue matokeo nadhani kaishiwa busara na hekima au pengine hajui analoongea. Kwa mwendo huu tuna safari ndefu sana watanzania.
 
Mwanahalisi na majira
 
Mtoa mada muongo hakuna gazeti lilioandika hiyo habari, sana sana alichokisema kawambwa ni kuwa kufeli kwa wanafunzi chanzo ni kuwa serikali imedhibiti mitihani
umesoma magazeti yote?
 
Mmmmh utakuwa udhaifu sana.
Je na wale waliochora zombie watarudia?
Je mtu aliefaulu leo kesho akifeli itakuwaje?
Na je matokeo yakiwa yale yale nini kitafanyika na tayari wameingia hasara?
Je hawaoni itakuwa ni sawa na kuandaa taifa la wajinga wengi maana wamefaulu bila jitihada zao?
 
alichokisema kawambwa ni kuwa kufeli kwa wanafunzi chanzo ni kuwa serikali imedhibiti mitihani

Duuh.. Haya ndo sawa na nyumba nzima kuungua na out of that loss unajifariji na panya waliokuwa wanasumbua wamekufa nao kwenye huo moto..! Huyu kawambwa asitake kuwafanya Watanzania wote mambumbu trend ya matokeo ya mitihani yearly yanaonyesha kiwango cha ufaulu kushuka na cha kufeli kinapanda kwa kasi ya ajabu.! Leo anakuja na kijiteteo cha kijinga hivyo..!
 
Tunasubiri kauli ya Raisi,vijana warudie pepa
 
wanahamisha div 0 o-level na kupeleka advance.....................nchi inasikitisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…