Matokeo Tata ya Kidato Cha IV: Mkurugenzi wa NECTA, Bi. Ndalichako Ajitokeza TBC, Ajikanyagakanyaga!


Swadakta...Penye red na yeye ni sehemu ya hiyo serikali.
 
pokea like zangu mia
mkuu tatizo la watanzania ni akili fupi na mitazamo yetu ya maneno mengi kumbe pumba tupu.

yaani watu wanaona kwamba NECTA ndiye mkosaji waksahau NECTA ni test administrator tu ambaye hausiki kwa lolote lile zaid ya kuatibu mitihani bad enough hata watunzi wa mitihani sio wao ni waalimu wenyewe, na hata kusahihisha ni waalimu wenyewe kuhusu kuyapanga ni jopo la mratibu wa elimu tena kulingana na matokeo ya usahihishaji sasa hapa necta inahusika vipi??

tena kwa ujinga na umbumbu wetu, eti mtu anasema mama ndalichako anatafuta public sympathy ...................my foot kwa kitu gani??

wakaulize ofisi ya maktaba inaidhinisha vitabu vyenye ubora gani kwa hawa wanfunzi, waulize mamlaka ya elimu inaratibu vipi ubora wa elimu wa taifa hili kuanzia kwenye mitaala hadi uwezeshwaji kisera. waulize wizara ahusika inasmamia vipi ubora wa elimu y nchi hh kuanzia kwenye miundo mbinu hadi malipo kwa watumish waalimu.

mamlaka ya elimu inachangisha sh ngapi kwa mwaka?? je imewah kusema inatrain waalimu wawe bora?? kuna kozi gani ambazo mwl anakwenda za capacity building zaid ya kukalia ujuzi aliofundishwa na pro Mbise na Katabaro toka akiwa chuo?? tizama mabadiliko ya kisayansi je yanakuwa kulingana na elimu yetu?? je nani anayejali??

kiukweli serikali inamengi ya kujibu hapa, mtihani wa biology ndo kabisaa wanafunzi hawajaufanya wengi wao walitoka kwa kukusanya karaatasi bila kujaza, wakachora na messi wafikiri Necta hapa inahusikaje??

serikali irudi kwa waalimu ituulize tatizo ni nini nasi tutawaambia tatizo lilipo.
 
sitegemei TBC kummuhoji lolote kwa manufaa ya taifa!sanasana anauza sura tu.kama ana guts aje hapa JF kwenye wananchi wenye ujuzi wa mambo!
 
gfsonwin, amini huyu Pasco analo lake binafsi juu ya maneno yake. hoja yake nitaikubali ikiwa tu serikali kupitia wasimamizi wa mitaala ya elimu ya sekondari wakisema kuwa baraza la mitihani lilitunga mtihani ambao haukufanan na walichopaswa/ takiwa kitunga. huyu Pasco anachanganya mambo, eti ni kosa kwa CEO wa baraza la mitihani kuingia na script ya mtahiniwa kwenye chombo cha habari eti alitakiwa kuja na copy, kwani ameacha original pale TBC?.. na anaposema ni siri siri ikiwa kwanani? anataka kutuambia CEO wa baraza la mitihani hatakiwi kushika original scripts za watahiniwa?. hawa wanao lalamika leo kuwa ndalichako a-resign walishindwa kuelewa umuhimu wa madai ya mbatia juzi kuwa Tanzani haina mtaala mmoja uliopitishwa kwaajili ya elimu. walikaa kimya. leo ndo wanajona wanauchungu .. uchungu wanautoa wapi?. hivi ikiwa mtaala walio nao baraza , ni tofauti na wewe gfsonwin unachofindishia, tena tofauti na ule mimi kindimbajuu ninaofundishia huku kiraracha . sasa huu mtihani utakao tungwa na baraza wanafunzi watafaulu vipi? kwamaana hata waliofaulu ni wamefaulu kwa kubahatisha .: haya matokea yalikuwa tayari zaidi ya wiki na ndo yamemfanya Mushi ajihuzuru kule taasisi ya elimu
wizara ya elimu ikiendelea kuleta uhuni wa kuto kujali majukumu yake, kuto kujali walimu inachimba kaburi la kuzika taifa lake, wanazika nguvu kazi ya taifa. na taifa letu litakuwa tegemezi..ndo maana hata leo kazi za kuuza baa, kufundisha shule za watoto wadogo zinafanywa na wakenya... .
 

Mkuu umesema kweli kujituma kwa mwanafunzi nacho ni kichocheo cha kufanya vizuri. Lakini kubwa zaidi ni kwa serikali kupoteza mwelekeo kuhusu elimu. Walimu hawasikilizwi, shule za kata zimejengwa bila mkakati wa kuhakikisha kuwa ubora wa elimu unazingatiwa.
 
sitegemei TBC kummuhoji lolote kwa manufaa ya taifa!sanasana anauza sura tu.kama ana guts aje hapa JF kwenye wananchi wenye ujuzi wa mambo!

Mkuu huku hathubutu kuja... Ataenda kule na kwao na Clouds tuuu
 
Kilaza mkubwa wewe siyo mkurugenzi ni katibu mtendaji wa necta toa ukilaza wako hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…