Matokeo: Vodacom Premier League, Prisons 2 - 0 Yanga SC uwanja wa Sokoine Mjini Mbeya

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya ligi kuu Tanzania Bara VPL, kuendelea leo kwa mechi kali kupigwa kati ya Wajelajela Tanzania Prisons ambao wanawakaribisha Yanga SC kwenye uwanja wa Sokoine Mjini Mbeya.

Hizi ni dakika za mwisho za ubingwa na huenda Wekundu wa Msimbazi Simba SC wakatangaza ubingwa rasmi leo endapo Yanga watashindwa kupata ushindi kwenye mchezo huu wa kiporo dhidi ya Tanzania Prisons.

Kumbuka Azam Sports 2 watakuwa mubashara, huku TBC Taifa ikipeperusha matangazo hayo kwa njia ya redio kuanzia saa 10:30 jioni.

Vikosi vya timu zote ni hivi hapa ambapo Yanga SC mabingwa watetezi wanashuka kwenye dimba hilo huku ikiwa wachezaji wawili pekee wa akiba. Usikose ukaambiwa kaa nasi usiende mbali.

Naam timu zote zipo uwanjani kwa ukaguzi pamoja na kupiga picha za kumbukumbu

==> Wakati wowote mpira utaanza hapa uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.. Tushuhudie yatakayojiri

00' mpira umekwisha anza uwanja wa Sokoine.. Tanzania Prisons Vs Yanga SC

05' Hakuna bao kwa pande zote mbili si Tanzania Prisons wala Yanga SC washambulizi kwa pande zote

Anakwenda mbeleee kwako Juma Abdul.. anagonga pembeni mwa uwanja kwake Akilimali. lakini wanapoteza na kuchukua Tanzania Prisons sasa.

Anagonga katikati ya uwanja kwa kichwa kwake Kamusoko.. Lakini mwamuzi anasema faulo kuelekea lango la Tanzania Prisons

Anapiga shuti mchezaji wa Prisons lakini golikipa anacha utoke nje ili iwe Goal Kick

16' Ni kona kuelekea lango la Yanga SC.. Inapigwa lakini golikipa anaokoa na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda na kuwa kona ya Tatu na mchezaji wa Prisons anapiga kichwa na kuwa Goal Kick

Yanga sasa mbele kwake Juma Abdul akwenda apiga konaaa, inapigwa kona, lakini golikipa anafanyiwa faulo. Na yuko chini baada kupata rabsha

24 ' Ni faulo kuelekea lango la Tanzania Prisons. Inapigwa lakini golikipa Kalambo anadaka

28' Anakwenda Paul wa Yanga lakini golikipa Kalambo anatokea na kudaka mpira ule.. Ilikuwa ni hatari sana

Golikipa wa Yanga yuko chini baada kupata kashikashi.. Ameinuka na Mpira unaendelea

Ni kona kuelekea lango la Yanga. Imepigwa, lakini kona nyingine, inapigwa kona golikipa Kakolanya anadaka

36' Tanzania Prisons 0-0 Yanga SC, mpira umekuwa na mashambulizi kwa pande zote

Ilipigwa shuti kali na mchezaji wa Prisons lakini mpira umekwenda pembeni mwa lango..

43' mchezaji jezi namba 12 anakotroo anapiga shuti na linatoka mita chache ya lango la Tanzania Prisons

Tanzania Prisons 0-0 Yanga SC

44' Yohana Mkomola anapiga kichwa na kutoka nje ya lango la Tanzania Prisons.. Ilikuwa nafasi nzuri kwake kuandika bao la kwanza

45+2' VPL mpira kuelekea kuwa mapumziko uwanja wa Sokoine mjini Mbeya..


Namna mpira ni mapumziko timu zote zinatoka uwanjani bila kufungana kwa kipindi hiki cha kwanza


Tanzania Prisons 0-0 Yanga SC

==> Dakika 45 za kuamua mtanange huu wa VPL zinaanza hapa uwanja wa Sokoine mjini Mbeya kati ya Tanzania Prisons Vs Yanga SC

47' Golikipa Kalambo anafanya kazi ya ziada kwenye lango lake na kuondosha hatari zote.

Kamusoko kwake Akilimali. Lakini anautoa mchezaji Prisons na kuwa wa kurushwa..!

51' Tanzania Prisons 0-0 Yanga SC

Anakwenda mbeleee apiga shuti lakini anaokoa beki wa Yanga. Alikuwa mchezaji wa Prisons ambaye

56' Tanzania Prisons wanapata Painatiiiii baada ya mchezaji wa Yanga kuunawa mpira

58' Goooooaaal Goooooaaal Goooooaaal
Tanzania Prisons wanapata bao la kwanza baada ya mkwaju wa painati kutoka kwa mchezaji Mpepo

60' mchezaji wa Prisons yuko chini baada kupata rabsha

63' Tanzania Prisons wanafanya mabadiliko.. Anatoka James na nafasi yake inachukuliwa na Mwihambi

Mchezaji jezi namba 4 wa Prisons anapewa kadi ya ngano kwa mchezo usikuwa mzuri

Tanzania Prisons wameamka sasa.. Mchezaji Mpepo anapiga shuti kali na Mpira kupaa nje ya lango la Yanga SC na kuwa Goal Kick

Yanga wanakwenda.. Maka kwake Juma Abdul.. Lakini Mkomola anakuwa Offside

75' Tanzania Prisons 1-0 Yanga SC

Ni faulo kuelekea lango la Tanzania Prisons. Inapigwa faulo ile lakini golikipa Aron Kalambo anadaka bila wasiwasi

81' Yanga wanafanya mabadiliko.. Anatoka Akilimali na Paul.. Na nafasi zao wanachukua Yusuf na Amis Tambwe

Goooooaaal Goooooaaal Goooooaaal Goooooaaal
Tanzania Prisons wanapata bao la pili kupitia kwa mchezaji Bosco

Tanzania Prisons 2-0 Yanga SC

Golikipa Kakolanya anapewa kadi ya njano.. Baada ya kubishana na mwamuzi

Kwake Juma Abdul.. Kwake Martin kwake Edwan na inakuwa ni faulo

90+4 ' Tanzania Prisons 2-0 Yanga SC, Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya

90+4 Mchezaji wa Yanga yuko chini baada kupata rabsha

Mpira katikati ya uwanja kwake Mchezaji wa Yanga.. Lakini wanapoteza

90' za mchezo wa kombe la ligi kuu Tanzania Bara VPL umemalizika hapa uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.. Ambapo Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa magoli mawili bila majibu dhidi ya Yanga SC.

Kwa matokea hayo Simba SC wanakuwa mabingwa rasmi wa VPL
 
Duhhh ata kama adui mwombee njaa ila hii ya Yanga inatia huruma, yani sub kuna wachezaji wawili tu na wimbi la wachezaji kuendelea kugoma linawezekana kuendelea kuongezeka

Nina wasi wasi ata match ya shirikisho Yanga atakufa tena uwanja wa nyumbani maana wachezaji wanaodai mafao yao sidhani kama watakuwa washalipwa na ata hawa wanaocheza ni wale wanaodai pesa kiduchu kwakuwa hawachezi mara kwa mara
 
Leo mapema Simba SC wanachukua ubingwa kwenye kochi.. This is Simba SC Brother
 
Akiumia golikipa inabidi mchezaji wa ndani achukue nafasi hiyo.. Kwani kwenye SUB hakuna golikipa
 
Timu zote zipo uwanjani kwa ukaguzi pamoja na kupiga picha za kumbukumbu
 
Mpira umeanza uwanja wa Sokoine.. VPL Tanzania Prisons Vs Yanga SC
 
Mbali na yote tunayopitia bado sikati tamaa. Kila la kheri timu yangu pendwa Yanga.

"DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"
Kweli wewe ni shabiki wa kweli[emoji122] [emoji122] [emoji122]
Rafiki yangu mumu nasikia kaacha kuishabikia [emoji4] [emoji4] [emoji4]
 
Kweli wewe ni shabiki wa kweli[emoji122] [emoji122] [emoji122]
Rafiki yangu mumu nasikia kaacha kuishabikia [emoji4] [emoji4] [emoji4]
Ahsante mdogo wangu.

Hahaaa. Lol mumu hataki presha. Mie huwa naamini siku zote kuna kupanda na kushuka na kwa sasa tumeshuka sina jinsi nitaishangilia tu.

Sababu ni mapito haya Thad.
 
Njaa itawauwa Hawa [HASHTAG]#Ndala[/HASHTAG]!! Nadhani Karibuni Yanga itatangaza Kufilisika.
 
Ahsante mdogo wangu.

Hahaaa. Lol mumu hataki presha. Mie huwa naamini siku zote kuna kupanda na kushuka na kwa sasa tumeshuka sina jinsi nitaishangilia tu.

Sababu ni mapito haya Thad.
Kabisa, asikubali kushindwa si mshindani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…