kabulimvos
Member
- Feb 28, 2021
- 20
- 41
Mimi nataka kujua ni kwa nini matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2008 yamefichwa hayaonekani ila miaka mingine kama 2007 na 2009 yanaonekana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watu walifeli sana ACSEE 2007,kuliko ACSEE 2008Watu walifeli sana, 2008, mtihani ulikuwa mgumu sana nasikia
Mimi mwenyewe ni mmojawapo wa watahiniwa wa PCM ACSEE 2008, kiukweli mtihani ulikuwa mgumu mpaka nashangaa siku hizi wanaofaulu ni wengi kulinganisha miaka hiyoWatu walifeli sana, 2008, mtihani ulikuwa mgumu sana nasikia
Yani unamaanisha phy na pure ya 2008 ilikua ngumu? Ulifanikiwa kuona phy ya 2007 kweli? Kama uliona mwaka 2008 ilikua ngumu kuna uwezekano ungemaliza 2007 ungezungusha kabisa.Mimi mwenyewe ni mmojawapo wa watahiniwa wa PCM ACSEE 2008, kiukweli mtihani ulikuwa mgumu mpaka nashangaa siku hizi wanaofaulu ni wengi kulinganisha miaka hiyo
Katika historial ya mitiahani ya science (hasa kombi zenye pure na phy) hakuna pepa ilikua ngumu kama ya 2007. Hizo pepa za 2008 kuja 2010 zilikua simple naona waliamua kulegeza baada ya kuona maafa waliyo fanya 2007.Watu walifeli sana, 2008, mtihani ulikuwa mgumu sana nasikia
Na kuanzia kipindi hicho naona mitihani imekuwa simple sana madogo yanafaulu tu kirahisiNi kweli tupu,nilifanya huu mtihani,PCM,matokeo yalikuwa mabaya sana,wenzangu wengi walizungusha. Niliishia kupata D,D,D tu
Twende mbele turudi nyuma ACSEE 2008 ulikuwa balaaMkuu uko serious kweli? Mtihani wa 2007 ulikuwa na ugumu gani ule?
Mimi nlifanya 2008 lakin ungenipa wa 2007 na hakika marks zisingepishana
Mtihani ulikuwa mgumu sana , ila nashukuru nilifaulu sana kuliko hata o level, yaani division one point zangu 6Mimi mwenyewe ni mmojawapo wa watahiniwa wa PCM ACSEE 2008, kiukweli mtihani ulikuwa mgumu mpaka nashangaa siku hizi wanaofaulu ni wengi kulinganisha miaka hiyo
SanaaaaaTwende mbele turudi nyuma ACSEE 2008 ulikuwa balaa
Hii ni fact mkuu. Hali hii ipo hata katika vyuo, kila mtu akiona chuo chake ndio kina shule ngumu sana kuliko kwingine!Mbonaa haukuwa na ugumu wowote sema ni Ile Hali ya mtu yeye kujiona Kama wakati wake kuwa ni mgumu Sana Ila kwa wengine ni mayai yai.
Yaani mtu utakuta hata ni mjeda anayasifia mafunzo yake anadai sio Kama nyie mnaofanya.
Kinachosumbua hapa ni ego Ile kujiona kuwa wewe ni mwamba wengine ni udongo ama ni yai.
Yaani mtu akipitia njia zake za maisha anajiona Kama yeye pekee ndiye akapitia magumu kuliko wengine so anahitaji salute.
Kuna uzi humu unaongelea kuwa ni magumu gani umeshawahi pitia ambayo hutosahau.
Binafsi nishawahi kaa ndani siku mbili bila ya kula nikakutana na mwamba anadai alimaliza siku tatu so hata sikuandika kitu kuwa Kuna gumu nimeshapitia
Hongera sanaMtihani ulikuwa mgumu sana , ila nashukuru nilifaulu sana kuliko hata o level, yaani division one point zangu 6
Iyo ukiwa ulitokea shule Fulani nadhani hata madogo hawakuafuatilii. Yaani wanacheki mwisho nne labda zikiwa chache ndio wanakaribia kucheki za tano kidogo Ila sio sana. Yaani nikiwa olevo nahitaji kujua waliofaulu kwa single digit basi. Unakuta Saba nane mpaka Tisa. Yaani mtu akitokea huko ndio unauliza hii Tisa huyu Juma abdalah ndio yupi huyo so unakumbushwa unampatia salute yake.Hongera sana
Huu mwaka ni shida mkuu nakumbuka Kuna PCB division III za 13 zilienda kusoma Medicine yaani ilikua taabu, TO alikua na C ya physics2013 pia matokeo yalikuwa mabaya mno pia..huu ulikuwa mwaka mbaya mno..matokeo yametoka tupo jeshini, watu ilikuwa ni kilio tuu.