Matokeo ya darasa la 7 ni kituko na ni aibu kwa taifa

Matokeo ya darasa la 7 ni kituko na ni aibu kwa taifa

Watoto hawa ambao wengi wana wastani wa d wakiingia sekondari taifa linataka wasipate divison 0!!!!

Ebu fanya projection ya matokeo ya Form IV mwaka2016, itakuwa ni aibu juu ya aibu!! Namwonea huruma atakayekuwa Waziri wa Elimu mwaka huo!
 
Lazima hawa wataalamu wetu wizara wawe na lengo flani, sio bure!!!!
 
Tatizo ni kuwa nchi yenyewe inaongozwa na watu walioferi darasani na hata maisha ya kawaida wakaja kuibukia kwenye upigaji debe wa siasa za maji taka. Na haya ndiyo matokeo yake.
 
zamani wakati tunacheza chandimu (football ya mchangani), tulikuwa tunaweka vijigoli vidogo kama vile vya handball au hockey.

ikifika mahali timu zetu zinashindwa kufungana tulikuwa tunaamuaga kupanua magoli.

shukuru kawambwa & co wanacheza chandimu!!

Badala ya kuongeza stamina za kufunga nyie mnapanua magoli! Like mkuu! Natumia simu,
 
Angalia MULUGO mwenyewe kwanza kabla ya kuangalia watoto hawa,nasikia hata yeye shule yake amepindisha majina,muulize SUGU mbunge mbeya mjini wamesoma nae MBEYA DAY.Alifeli sec.
 
Siasa mpaka kwenye elimu;inaboa sio siri maana watoto wanazidi kupotezwa,hisabati kama kawa kuchagua a,b,c...duuuh!
 
Hii ndiyo Tanzania tuitakayo. Ukitaka kumtawala mtu utakavyo mnyime Elimu.
 
Nadhan wana andaa kaul ya kuwa laumu chadema kwamba ufaulu upepungua coz chadema ndo itakua ina Run selikari (mwaka 2016)
 
Hizo takwimu za uchaguzi wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Sekondari mwaka 2013 ni kwa ajili ya Wahisani au Wafadhili wa sekta ya Elimu na sio kwa Watanzania. Hii ndio hali halisi ya Serikali kutufanya Watanzani ubongo wetu haupandi kwenye uchambuzi wa data.Mitihani yenyewe ilikuwa na utata,usahihishaji nao usiseme ndio maana hata matokeo yalichelewa kutolewa lakini Waziri hakutaka kusema ukweli kwa hofu ya kuchokoza kidonda namna wanafunzi hao walivyoteseka vipindi vya mgomo wa Walimu na kipindi cha sensa. Hata hivyo akumbuke kuwa kila lenye mwanzo lina mwisho.
 
Back
Top Bottom