Matokeo ya Darasa la Saba 2022 yametoka rasmi

Matokeo ya Darasa la Saba 2022 yametoka rasmi

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya Darasa la Saba ya mwaka 2022. Matokeo yanaonesha watahiniwa zaidi ya Milioni 1.07 kati ya Milioni 1.34 waliofanya Mtihani ambayo sawa na asilimia 79.62 wamefaulu kwa kupata madaraja A, B na C.

Bonyeza hapa kuona matokeo darasa la saba 2022

Kati ya hao wasichana ni 558,825 ambao ni sawa na asilimia 78.91 na wavulana ni 514,577 sawa na asilikia 80.41.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Almasi ametangaza matokeo hayo leo Alhamisi Desemba Mosi, 2022 wakati akizungumza na wanahabari jijini hapa kuhusu mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi uliofanyika Oktoba 5 na 6 mwaka huu.

Almasi amesema katika matokeo ya mwaka 2021 watahiniwa walikuwa 907,802 sawa na asilimia 81.97.

Amesema kitakwimu kuna kupungua kwa ufaulu kwa asilimia 2.35 ingawa idadi ya watahiniwa waliofaulu imeongezeka kwa watahiniwa 165, 600 sawa na asilimia 18.24 ikilinganishwa na mwaka jana.
 
1.07 million walimaliza class seven? Aisee mbona ni wengi namna hii?

Soko la ajira tayari lipo saturated, wahitimu kila siku wanamaliza shule na vyuo. Scary!!
 
EDUCATION IN TANZANIA... IS POLITICAL DEMONSTRATION OF GOVERNMENT RESPONSIBLE TO EDUCATE ITS PEOPLE...

Hakuna cha zaidi... Watakaa na toto lako weee... Mwisho wa siku watakurudishia washamlemaza...hajiwezi kwa lolote maisha ya mtaani kwake.
 
1.07 million walimaliza class seven? Aisee mbona ni wengi namna hii?

Soko la ajira tayari lipo saturated, wahitimu kila siku wanamaliza shule na vyuo. Scary!!
uko siriaz kweli mkuu? hakuna nchi duniani inayoweza ajiri graduates wote
 
Karibuni sekondari, karibuni form one
Wachache mtakaoenda vyuo vya ufundi pia Mungu awatangulie. Wanaoolewa na wanaoenda kufanya biashara mbalimbali hali kadhalika Mungu awe nanyi.
 
Kiukweli wengi ni mizigo Tu elimu yetu bado changamoto siasa nyingi Santa aisee
 
Kiukweli wengi ni mizigo Tu elimu yetu bado changamoto siasa nyingi Santa aisee
Jamani hao ni wahitimu wa Elimu ya msingi. Tangu lini wameshanza kuwa mizigo?? Hao si bado watoto au!!!! Au hawakupaswa kupata Elimu ya msingi?
 
Siyo wao. Ni sisi wazazi kupunguza kufyatua.
Ishu sio kufyatua tu hata mifumo ya elimu ibadilike.

Mtoto anasoma masomoo meengi mwisho wa siku anakuja kuwa machinga au fundi makenika.
 
Jamani hao ni wahitimu wa Elimu ya msingi. Tangu lini wameshanza kuwa mizigo?? Hao si bado watoto au!!!! Au hawakupaswa kupata Elimu ya msingi?
Mkuu huo ndio msingi lazima huku kuwe imara Sasa kama mtoto hajui kusoma Huko mbele atajifunza Nini kwenye lugha ya jaazi
 
Leo matokeo ya Darasa la Saba yametoka nimeona ufaulu umepungua,tumezoea kusikia ufaulu umeongezeka,Kwa mtizamo wangu huu ni ufaulu WA halali,
 
kwa sasa JPM hayupo ukweli ulikuwa usemwi
 
Naona walimu wameamua kupiga mishe zao za bodaboda (urefu wa kamba zao) hali sio nzuri hata kidogo kwenye hizi shule zetu za kubeba mfagio na kidumu cha maji!
 
Back
Top Bottom