BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya Darasa la Saba ya mwaka 2022. Matokeo yanaonesha watahiniwa zaidi ya Milioni 1.07 kati ya Milioni 1.34 waliofanya Mtihani ambayo sawa na asilimia 79.62 wamefaulu kwa kupata madaraja A, B na C.
Bonyeza hapa kuona matokeo darasa la saba 2022
Kati ya hao wasichana ni 558,825 ambao ni sawa na asilimia 78.91 na wavulana ni 514,577 sawa na asilikia 80.41.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Almasi ametangaza matokeo hayo leo Alhamisi Desemba Mosi, 2022 wakati akizungumza na wanahabari jijini hapa kuhusu mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi uliofanyika Oktoba 5 na 6 mwaka huu.
Almasi amesema katika matokeo ya mwaka 2021 watahiniwa walikuwa 907,802 sawa na asilimia 81.97.
Amesema kitakwimu kuna kupungua kwa ufaulu kwa asilimia 2.35 ingawa idadi ya watahiniwa waliofaulu imeongezeka kwa watahiniwa 165, 600 sawa na asilimia 18.24 ikilinganishwa na mwaka jana.