Matokeo ya Darasa la Saba mwaka 2012 yatangazwa rasmi

Matokeo ya Darasa la Saba mwaka 2012 yatangazwa rasmi

Naona BRN imeanza kufanya kazi, mwezi mmoja matokeo tayari! Hiyo machine imesaidia xana, swali kwa anaejua, kuanzia grade ipi ndo watachaguliwa kujiunga masomo ya kidato cha kwanza? Maana hajaweka marks ni grade tu.
 
My name is shule ya kata,darasa la saba nilipita tu..,nikaingia form one niliposoma hadi form form nikapata division 5 ya kuingia form V,form since finally nikafaulu kwa division VI,now niko chuo nasoma niki graduate nikafundishe divbision 7
 
My name is shule ya kata,darasa la saba nilipita tu..,nikaingia form one niliposoma hadi form form nikapata division 5 ya kuingia form V,form since finally nikafaulu kwa division VI,now niko chuo nasoma niki graduate nikafundishe divbision 7
Aaaaaaaah acha hizo mwekundu !
 
Jamani, nimeamini Tanzania tunaweza. Kumbe ufaulu upo juu kiasi hiki! Naipongeza Serikali kwa mpango huu wa BRN kwani umerahisisha hata usahihishaji. Lakini nashauri Serikali ihakikishe kuwa wanafunzi waliofaulu wote wamekwenda Sekondari, na pia walimu hongera sanaaaa! Kwa kazi nzuri. wahabari Dar es Salaam jana, wakati wa kutangaza matokeo ya mtihani huo wa mwaka huu.


Dar es Salaam. Zaidi ya asilimia 50 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba Septemba mwaka huu, wamefaulu.
Matokeo hayo yalitangazwa jana na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde aliyesema ufaulu huo ni ongezeko la asilimia 19.89 ikilinganishwa na mwaka jana.
Alisema jumla ya watahiniwa 844,938 walifanya mtihani huo na kati yao 427,606 sawa na asilimia 50.61, wamefaulu kwa zaidi ya alama 100 kati ya 250.
Dk Msonde alisema kati ya watahiniwa hao waliofaulu, wasichana ni 208,227 sawa na asilimia 46.68 na wavulana ni 219,379 sawa na asilimia 55.01.
Matokeo hayo pia yanaonyesha kuwa, wan
 
Ingia hapa!
http://www.necta.go.tz/matokeo_html_2013/psle.htm
 
Kweli wanajua kusoma hao watoto wote au wanaenda wajaza shule za kata tu
 
WIZARA YA ELIMU IMEACHIA MATOKEO YA DARSA LA SABA HUKU WAVULANA WAKIWAGALAGAZA WASICHANA,AIDHA SHULE YA ROCKEN HILL YA WILAYA YA KAHAMA MKOANI SHINYANGA IKIENDELEZA UBABE KWA MIAKA MINNE MFULULIZO IKIFUATIWA NA TUSIIME YA TABATA DAR ES SALAAM,NA ZINGINE NI KWEMA PRIMARY PIA YA HUKO WILAYANI KAHAMA MKOA WA SHINYANGA.zaidi tembelea tovuti ya Baraza ambayo ni www.necta.go.tz
 
Tusiime kinara wa matokeo ya mtihani darasa la saba Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla 2013

Kwa mujibu ya matokeo yalitotangazwa na naibu katibu mtendaji wa baraza la mitihani la taifa (NECTA), Dr. Charles Msonde shule ya Tusiime imekua katika nafasi kama ifuatavyo,

Number 1 kwa wilaya ya Ilala kati ya shule 99
Number 1 kwa mkoa wa Dar es Salaam kati ya shule 486
Number 2 kitaifa kati ya shule 15656

katika wanafunzi 158 waliofanya mtihani huo, ...

157 wamepata wastani wa daraja A na mmoja daraja B
124 wamepata alama A kwa masomo yote matano (straight A)

katika wanafunzi 158,Shule imepata wastani wa alama 230.0063 kati ya 250
ambapo shule ya kwanza kitaifa yenye wanafunzi 50 imepata wastani wa alama 230.8800
191750_285929034863884_815922324_o.jpg
 
je wanafunzi hawa ktk elimu zingine za juu, wataonekana au? ndio kale kamchezo kaliko wapoteza st. MARYS
OTHERWISE hongereni sana waalimu na wanafunzi TUSIIME 2013/14
 
je wanafunzi hawa ktk elimu zingine za juu, wataonekana au? ndio kale kamchezo kaliko wapoteza st. MARYS

Swali hili tujiulize sana! Inapofika kwenye elimu isiyo ya kulishwa, hawa hawa vipanga wanageuka kuwa watu wa kawaida kabisa. Ukifika vyuo vikuu na taasisi za juu utagundua hamna tofauti , isipokuwa kule chini mazingira ya shule hizi za kulipia yako vizuri, lakini kiukweli kiuwezo wa kupambanua mambo hamna gape lolote kati ya St. Kata na St. English Medium hasa munapokutana sehemu ambayo hamna tuition au kulishwa elimu!
 
je wanafunzi hawa ktk elimu zingine za juu, wataonekana au? ndio kale kamchezo kaliko wapoteza st. MARYS
OTHERWISE hongereni sana waalimu na wanafunzi TUSIIME 2013/14
Itategemea baada ya hapo wataenda shule zipi za Secondary, kama wataenda huko MadongoKwinama usitegemee watafanya chochote. Kama una uwezo mpeleke mtoto wako shule nzuri aisee, huo nao ni "uzalendo", by Lemma.
 
Hongera sana waalimu,utawala na wanafunzi wa Tusiime. Hivi shule ya kwanza kitaifa ni ipi?
 
Hivi zamani kulikuwa na grading kweli?

Manake nakumbuka enzi zetu ilikuwa ni pass na fail tu.

Walianza lini ku grade?
 
Back
Top Bottom