Jamani, nimeamini Tanzania tunaweza. Kumbe ufaulu upo juu kiasi hiki! Naipongeza Serikali kwa mpango huu wa BRN kwani umerahisisha hata usahihishaji. Lakini nashauri Serikali ihakikishe kuwa wanafunzi waliofaulu wote wamekwenda Sekondari, na pia walimu hongera sanaaaa! Kwa kazi nzuri. wahabari Dar es Salaam jana, wakati wa kutangaza matokeo ya mtihani huo wa mwaka huu.
Dar es Salaam. Zaidi ya asilimia 50 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba Septemba mwaka huu, wamefaulu.
Matokeo hayo yalitangazwa jana na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde aliyesema ufaulu huo ni ongezeko la asilimia 19.89 ikilinganishwa na mwaka jana.
Alisema jumla ya watahiniwa 844,938 walifanya mtihani huo na kati yao 427,606 sawa na asilimia 50.61, wamefaulu kwa zaidi ya alama 100 kati ya 250.
Dk Msonde alisema kati ya watahiniwa hao waliofaulu, wasichana ni 208,227 sawa na asilimia 46.68 na wavulana ni 219,379 sawa na asilimia 55.01.
Matokeo hayo pia yanaonyesha kuwa, wan