Setuba Noel
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 426
- 210
Wametangaza kuwa ufaulu umeongezeka kutoka 43% ya mwaka jana hadi 88%. Lakini hili ni changa la macho, hali ni ile ile. Ngojeni nikuonesheni walichofanya.
- Wamechomeka grades nyingine katikati. Miaka iliyopita kulikuwa na grades A, B, C, D na F, na points zake zilikuwa 1,2,3,4,5 respectively. Mwaka huu grades ziko 7 ambazo ni A, B+, B, C, D, E na F, na points zake ni 1 hadi 7 kwa mfuatano huo. Hizi grades za mwisho kuanzia D zimevutwa, zile marks zilizokuwa F wamezigawanyia kwenye E, halafu ile F ikawa na marks za chini sana.
- Divisions zimebadilika katika mgawanyo wa points. Hapa chini oneni ilivyokuwa kabla na sasa:
- [TABLE="width: 500"]
[TR]
[TD]kabla[/TD]
[TD][/TD]
[TD]Sasa[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Division[/TD]
[TD]Points range[/TD]
[TD]Division[/TD]
[TD]Points range[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]I[/TD]
[TD]7-17[/TD]
[TD]I[/TD]
[TD]7-17[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]II[/TD]
[TD]18-22[/TD]
[TD]II[/TD]
[TD]18-24[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]III[/TD]
[TD]23-25[/TD]
[TD]III[/TD]
[TD]25-31[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]IV[/TD]
[TD]26-33[/TD]
[TD]IV[/TD]
[TD]32-45[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]0[/TD]
[TD]34-35[/TD]
[TD]0[/TD]
[TD]46-49[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Siri iko kwenye hizo divisions 4 na zero, utaona katika jedwali hapo juu kuwa wigo wa zero ni mdogo sana, na ule wa division four ni mkubwa kuliko zote. Maana yake ni kuwa wengi ambao wangepata division zero wamezawadiwa division four, na hii ndio iliyotumika kutupiga changa la macho kuwa ufaulu umeongezeka. - Sasa tazameni na matokeo ya jumla hapa chini muyasome sambamba na maelezo hapo juu, halafu judge for yourselves kama kweli ufaulu umeongezeka: