Matokeo ya Kidato cha Nne 2012 NECTA (CSEE)

Matokeo ya Kidato cha Nne 2012 NECTA (CSEE)

Kweli mwaka huu kimeeleweka na sijui Rais atasema ni malezi mabaya kama alivyosema First Lady? Hivi hizi shule zote ambazo zimefelisha watoto wetu ni kwamba wanaidai Serikali kwa madai yao ambayo hayajathibitishwa?
 
There are currently 10597 users browsing this thread. wote mnaangalia sifuri Tanzania is amazing
 
Na shule kumi za mwisho (zilizofanya vibaya zaidi) zinatoka Unguja, Pemba, Lindi, Tanga, Dar na Pwani.

Tupunguze kukariri juzuu, na kunywa gahwa.
 
SABABU ZA KUFELI
Dk. Kawambwa alitaja sababu ya kutofanya vizuri kwa shule nyingi hasa za vijijini kuwa ni kukosekana kabisa kwa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati na upungufu wa walimu wa masomo mengine.

Aidha alitaja sababu zingine kuwa ni kukosekana kwa maabara kwa shule za mikondo ya sayansi na maktaba za kujisomea pamoja na upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada katika baadhi ya shule.
MKAKATI WA SERIKALI

Dk. Kawambwa alitaja baadhi ya mikakati ya serikali katika kukabiliana na changamoto hizo kuwa ni kuajiri walimu kila mwaka ili kuondoa upungufu uliopo.

Alisema mikakati mingine ni ile ya kuboresha miundo mbinu iliyoko katika shule kwa kujenga nyumba za walimu, madarasa na maabara na kuendelea kutoa ruzuku ya Sh. 25,000 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka, nusu yake ikitumika kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

Aidha alisema kwamba wizara itaendelea kuzishauri halmashauri kuweka mgawanyo mzuri wa walimu waliopo baina ya shule na shule na kuimarisha Idara ya Ukaguzi wa shule na kuwawezesha Waratibu Elimu kata na Wakuu wa shule kufanya ukaguzi wa ndani katika shule za sekondari katika maeneo yao.

CHANZO: NIPASHE

My take: Anajikaanga?
 
Tuseme hayo matokeo ndo effects za mgomo wa walimu wa mwaka jana? Inawezekana mgomo bado unaendelea kimya kimya au vipi?
 
Matokeo ya mwaka huu ni huruma kwa wadogo zetu. Bora shule zenye majina ya wakuu wa nchi yetu huenda wakapata nafasi ya upendeleo ili waende form V
 
Hizi habari za nipa waswasi kubwa. Najiulizaa What is the future of our country?What is wrong with our education system? Whatever is wrong needs to be addressed immediately. It is a national crisis PERIOD!!!!!!
 
Kifupi matokeo ni mabaya sana natumaini sasa kuanza kupitia mtaala yetu mapema na wala tusione aibu kwani bila shaka kuna wakati umefika tuamue mtazamo wa elimu yetu bila shaka serikali ya ccm imeshidwa kutufikisha pale tunapoitaji kufika imetosha ni lazima ccm iondoke madarakani mapema sana 2015 bomu kama ili ni mwiba hakuna one ya 7 hakuna one 8 tisa ni za kuesabu hata 5 ni ndoto tunawajibu wa kutetea elimu yetu haya ni matokeo mbaya kutowahi kutokea.
 
Jamani kweli Walimu nao wameamua KUMWAGA MBOGA. Malezi ya watoto Je? Mtoto anaandika Matusi kwenye karatasi ya majibu?????????? Wana wazazi kweli? Jamani Vijana hatuaminiki tena siku hizi ndo maana ajira zimekuwa pia ngumu kutokana na elimu zetu za kubrashi. Let us be serious? Wazazi tuepuke kuiga western life kwenda beach kuoga na watoto! let us be serious with our children. Taifa nalo liko wapi? Hatuoni wageni wamevamia even in the most important areas. Tutakuwa kama Botswana!:tape2:
 
Hii wizara u-Mulugo umezidi sasa. Kweli Kawambwa anahakika waliopata zero ni asilimia 60.1 kweli? Jamani mimi nimechua namba ya waliopata zero nikagawanya na idadi ya wote nimepata 52.8% sasa hizo 60.1 kazipata wapi?
Tatizo wewe umechukua jumla yote wakiwemo private candidates, wakati hiyo 60.7% ni ya wanafunzi wa shule school candidates tu soma vizuri mchanganua utaelewa
 
Pale bungeni kina ndugai na makinda walimtukana sana mbatia. Haya ndo majibu ya nyongeza. Kuna haja ya tume? Kila mkikaa mnamuona mwigulu ndo ana akili. Juzi juzi tu kati ya 2001 to 2004 anaongoza migomo pale hostel mabibo na kutukana viongozi wa kitaifa na kupewa suspension leo ndo mshauri wa taifa kwa mambo mhm km elimu! Aaaaaaaaaaaha. Kweli hii ndo nchi ya majuha!
 
Back
Top Bottom